Kuna kitu kibaya Wema Sepetu kafanyiwa(mtazamo wa jicho la tatu)

Mshana Jr, mimi katika kupitia mada zako nikimtazama huyu dada naona hayuko kawaida. Pamoja na kupenda attention au kuathiriwa na tabia za mzazi. Kuna wakati unamuona kama vile anataka kurudi kuwa wema lakini inakuwa ngumu.
Mkempia na hili ndilo ninaloliona kwake
 
Maybe kafanyiwa ubaya lakini pia ni lazima tukumbuke kuna msemo "mchawi mzuri ni NAFSI yako mwenyewe".

Hata mie nilisikia kuna kipindi alikiri kuwa hana uwezo wa kubeba mimba. Sijui kwenye kipindi cha mkasi au mahali pengine ila ilikuwa ni live interview...
 
Hata mie nilisikia kuna kipindi alikiri kuwa hana uwezo wa kubeba mimba. Sijui kwenye kipindi cha mkasi au mahali pengine ila ilikuwa ni live interview...


Maneno huumba! Binaadam tukiwa tunapumua vizuri bila adha yoyote tunajisahau sana, Wema option aliyonayo kwa sasa ni kukaa chini na kujitafakari yeye binafsi maybe akianzia hapo atauona mwanga at the end of the tunnel!
 
Huyo demu hana lolote ni feki na hatokuja kupata raha ya dunia kwa sababu yeye mwenyewe muda mwingi anautumia ili awanyime wengine furaha,yeye mwenyewe kutwa anawaongelea wenzake vibaya sasa ni mungu gani atakayemkubalia ombi lake la mtoto wakati kuna watoto aliowaleta huyo mungu yeye anawakosoa.
 
Kwani huyu Mungu huwa anafurahishwa na jinsi yeye anavyoishambulia familia ya DIAMOND, kwa mfano alivyokuwa anang'ang'ania DNA, je yeye ni nani kwa DIAMOND hadi adai hiyo DNA. Au anaposema mtoto m'baya yeye inamuhusu nini ndio azae mzuri sasa sio kufanya fake wacha yamkute hayo na mengine na bado labda aache kufuatilia maisha ya wenzake ashike mambo yake.
 
Mkuu nakubaliana na mtazamo wako. Lakini kaa ufahamu kua wema anapenda sana tena sana kukaa kwenye Headlines zA magazeti. Na sio mtazamo wangu salama jabir aliwahi alimuuliza na Wema akakiri kua anapenda kuandikwa. Japo sometimes anaumia. So nahisi kwenye swala LA kupamba habari kwake sio tatizo kabisa. Tatizo lake nadhani linaweza kua ni mambo Binafsi ya kimaisha anayopitia especially love life
 
Mungu amjaalie tu basi apate japo mtoto mtoto mmoja...! She is dying for this. ..
 
Mungu amjaalie tu basi apate japo mtoto mtoto mmoja...! She is dying for this. ..
Mkuu
mshana jr,
you have a point, na kiukweli nimeguswa!, huyu dada 'has powers', she uses her powers and misuses them kwa kujijua au bila kujijua!, she needs help na sio ridicule!.
Mungu amsaidie!.

Pasco
Kwa wasiojua kuhusu powers, karibuni mnitembelee mitaa hii
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo bila kujiua!.
 
Hakuna aliye thibitisha kuwa ana mimba, ni kutafuta umaarufu tu na matangazo ya biashara.
 
Wema pamoja na kukaa hapa town lakini bado sana mi nafikiri tumpotezee sababu hana jipya.
 
Kama ulivyo andika pasco kama ni upendo wapo die harder fans wake kwa hiyo tutasema anao upendo na nguvu pia ila tatizo anachimba shimo kwa mikono yake mwenyewe na kwa miguu yake mwenyewe anajitumbukiza.Ukijiweka katika nafasi ya kaka au baba kwa wema ni lazima kama binadamu uumie but why kila siku awe yeye tu?kuna mamiss wangapi wamepita ambao japo hatuwezi kujiridhisha kuwa hawana viscandal scandal ila hawa make headlines kama yeye kwanini?hajitambui?au anapenda?au watu wanamtumia?
 
Ana nyota ya kizungu labda iliyomtransform kutoka maji ya kunde beauty to white monster
 
Mkuu Pasco first page nimeona like yako nikajikuta nafika mpaka page ya 7 si kwa kuifutlia hii thread la hasha bali nijue maoni yako kuhusu huyu binti...I lost my time kupekua pages na sijaona comment yako zaidi ya ma likes tu! For god sake weka maoni yako hapa
 
Mungu amjaalie tu basi apate japo mtoto mtoto mmoja...! She is dying for this. ..
mshana jr unaniangusha mkuu,hivi wewe huyu wakuitwa wema umemjua baada ya hii mimba feki au ??? unawezaje kumsaidia kuomba dua mtu aliyekwisha kumkashifu huyo mungu unayemuombea huruma yake ??? ( maana unaposema mtoto fulani m'baya ni kuingilia uumbaji wake mungu hata kama una mgomvi na wazazi wake bado mtoto hausiki na ugomvi wenu ) hayo maneno aliwahi kusema wema.
 
Wema ana malipo yake kwenye hilo na atalipwa accordingly lakini sisi kama binadamu tuna jukumu la kuwaombea watu kama hawa kwakuwa nasi tuna mapungufu yetu na tunaombewa na wengine
 
Lakini jamani mimba alikuwa kabeba kweli
Picha zake za hivi karibuni akiwa kavaa gaun nyeus kama ile ya anty ezekiel alikuwa amenenepa sana.Pole yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…