Kuna Kitu Rais Samia Amekisema Kuhusu Kurejea Kizimkazi “Post 2025”. Nashauri na Nasisitiza Wenye Uwezo Kusaidia, Tumsaidie Kumshauri Ukweli!

Yapo mambo yanaonekana na Kuna mambo hayaonekani. Mambo mawili makubwa yanaweza kutokea 2025. Mh Rais kukubali wosia wa wazee kuwa hakuwa ktk mnyororo wa kuwa Rais na mbele yake Kuna miba ambayo akitaka kuendelea basi akubali kuikanyaga ila maumivu yake yatakuwa makali kiasi atajisemea laiti ningesikiliza nikashuka nikapumzika. Nadharia ya pili ni conspiracy ambapo jambo lolote laweza kutokea 2025 yaani hakuna atakaye weza kuamini kama vile ilivyotokea huko USA. Bila kupepesa macho kuongoza nchi sio lelemama wala sio jambo la jinsia ukweli nikwamba utashi wakisiasa nimuhimu sana kwa kule tunaelekea. Sioni kwa uwezo wangu Mungu kanipa kama Mh Rais miaka 5 itakuwa rahisi kwake itakuwa ni miaka migumu sana kiasi anaweza kusema naomba kushuka ila ataambiwa huwezi kushuka ulisha shauriwa 2025 sasa maliza kiapo chako naogopa sana maana utakuwa usiku mzito sana. Well Sina uwakika kama majasusi ya Taifa hili kongwe yatashindwa pindua meza 2025 kuweka wanaye mtaka mambo ni mengi Muda mchache ila Mungu ibariki Tanzania na watu wake🕊️🙏
 
Mimi baada ya kuisikia hiyo kauli ya kwamba "mpaka 2028 nikijiandaa kwenda kupimzika kizimkazi "nilishituka sana inaonesha ameshahakishiwa
Tanzania Raha sana unapofikiri unajuwa nchi ndipo inakujuwa zaidi. Nikikumbuka mwamba na Urais wa Milele nachoka kabisa. Hakuna alie amini is the same 2025 hakuna atakaye amini🤐
 
Unajidanganya . Wezi wa kura ndio watakao iharibu nchi , Mbeya itakauka na kugeuka kuwa jangwa .
Narudia tena nafasi ya kuharibu Nchi Ili mkimbilie Kwa bwana zenu Ulaya haipo na hamtakuja kuipata so usipotexe mda na Nguvu na jambo ambalo huna uwezo nalo.

Mtaishia kutoa matamko kama kina Mwambukusi wa TLS 😂😂
 
Kwa hiyo Pasco unamaanisha TANGANYIKA KUPATA Uhuru Hadi 2030???!!!

Na ikitokea RAIS 2030 akawa Hussein Mwinyi au Mchengerwa maana yake WATANGANYIKA/WADANGANYIKA au MACHOGO KUPATA Uhuru Hadi 2040.
Hahahaaaa, nimecheka sana. Na zanzibar itafikia level ya mauritius, kisha watavunja muungano tuanze upya na Tanganyika yetu
 
Mkuu Paskali, ukiitwa ukaambiwa uthibitishe hizi kauli zako, je utaweza?
 
MAYALA kadiri yangu hili andiko kuandika vizuri sana, free from bias.

Amekuwa very objective, anasomesha wazi kuwa inawezekanaje mtu ajadili habari ya 2028 -2029 ?? ili Hali 2025 ni mwakani ambapo patakuwa na uchaguzi, kwa kauli ya Rais ni kwamba ana uhakika wa kushinda uchaguzi hata kabla ya uchaguzi!!

Maana nyuma yake Kuna wizi wa kura, matumizi ya vyombo vya Dora, plus watanzania wasiojitambua.

Lakini katika free and fair election, atarudi KIZIMKAZI misa ya kwanza tu.

Ni kazi ya watanzania kuamka na kuzuia kiongozi ambaye anauza maliasili, na rasilimali za Tanganyika.

Mama huyu akifaulu 2025, Urais wake utakuwa wa damu,watu kutekwa na kupotezwa,ambao watakuwa wanamkosoa.

Atakuwa anatumia rasilimali za BARA kujenga Zanzibar akishirikiana na kakake HUSSEIN.

Andiko la Paschal Mayala ni alarming sign, anatuamsha watanzania tukatae kwa matendo kauli ya Rais, kujitangaza indirect kuwa yeye atakuwa Rais 2025.🤔🤔🤔

Hii inatafakarisha sana,
Mama anakuwa kama ameagana na MUNGU ambaye ameshikilia hatima ya maisha UHAI.

Namaliza kwa kusema "ANAYELIRUKA SHIMO AMEAGANA NA NYONGA"
Cc:KIZIWI 🐸
Cc😛askal Mayala
 
Uchaguzi wa Tanzania ni sawa na WA Maduro wa Venezuela, yaani mtu anjiteua kabla hata ya uchaguzi na chaguzi hizi za maigizo it's just a waste of time and money
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…