Kuna Kitu Rais Samia Amekisema Kuhusu Kurejea Kizimkazi “Post 2025”. Nashauri na Nasisitiza Wenye Uwezo Kusaidia, Tumsaidie Kumshauri Ukweli!

Unajichanganya. Umeshasema tayari amehakikishiwa ushindi. Waliomhakikishia ushindi ni wanawake au wanaume? Ni wanaume. Sasa huyo jibaba ahofie nini wakati hapambani na huyo mwanamke ambaye anaonekana kuwa ni bendera tu. Huyo jibaba anapambana na nguvu zilizoko gizani. Yaani nguvu za giza. Yani hao wanaomweka huyo mwanamke. Hivyo jibaba popote alipo atembee kifua mbele na asiache kwenda mbele ya wananchi palipo na nguvu za mwanga kuomba ridhaa ya kuongoza taifa hili
 
Mtasewma mtachoka na usiku mtalala.

Hamuijuwi Tanzania yenukuwa ni Republic na wanaofanya maamuzi Tanzania ni 'aristoctats" siyo washauri wala rais.

Anaekiuka hilo, muulize rais wa malaika akupe jibu.
 
Kaka Mayala salam, nimesoma andiko lako na nimekuelewa, mimi binafsi nina swali je ni nini kusudio la kila aliyemadarakani ? nafikili tunajibu sawa ni kwamba kurudi tena kwa kipindi chake lakini pia kwa mujibu wa taratibu za chama chake yeye ndio anapwa kumalizia awamu yake so kwa hile kauli aliyoisema mimi sijaona kosa mpaka wewe mishipa ikakutoka namna hiyo. hili la kusema wanawake 2025 ndio muda wao mimi nakuunga mkono kabisa hu ndio muda wa wanawake so ni jambo la kuungwa mkono
 
Mkuu unatuchanganya au unajichanganya inawezekana ni uzee au huamini taarifa zako , kwa mujibu wa wewe na maandiko yako huko nyuma umeshaandika na Kusema 2025 Rais ni Mpango , yaani Mpango Mzima , Je ni nini tena kimekubadilisha mbona unakosa consistency ya mambo , kama Kuna mabadiliko ungeandika kwanza ili ku pre empty hili andiko lako
 
Naunga mkono hoja
 
Mkuu baro , kwenye mtaala wa hesabu shule za msingi kuna topic ya hesabu za yumkini, probability, shule nyingi huwa zina skip hii topic hivyo wangi hawajui yumkini, na kwenye yumkini ya kuyumkinika naweza kukutajia majina hata 10 na bado nikawa right
1. Baada ya Rais Samia kusema 2025 twende na mwanamke, nilipandisha bandiko hili na kusema, mwanamke huyo sio lazima awe Samia, anaweza kuwa Dr. Tulia!. Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

2. Nikasema anaweza kuwa Dr. Mwinyi. Kuelekea 2025 - Kinyang'anyiro cha Urais 2025 kwa tiketi ya CCM: Dkt Mwinyi kuwania Urais wa Muungano?

3. Nikasema anaweza kuwa Dr. Mpango. Kama Sauti Hii ni Sauti ya Kweli, Nimeelezwa Mpango Ndio Mpango Mzima!. Swali ni... Akiwa Mkristo, Kwanini ni Lazima Awe Mkatoliki?!

Kwa hesabu za probabilities za yumkini ya kuyumkinika, bado niko right!.

P
 

Mtu anatakiwa kweli kusoma kwa jicho la tatu ndipo akuelewe.
Mimi nimekuelewa kuwa Mama hafai kuendelea baada ya 2025.Kwamba amteue mwanamke mwezake mwingine agombee.
Naunga mkono kuwa Mama uwezo wake umefikia ukomo.Ajikongoje hadi 2025 halafu CCM imsimamishe mwingine.Lakini sikubaliani na wewe awe mwanamke.Nadhani mwanaume atafaa zaidi kwa urais wa TZ.
Unauliza kama wasaidizi wake wanamsadia kwa kumpatia ushauri wa uhalisia.
Kuna wasaidizi wa aina mbili;

1. Hawa ni wale ambao wanamuaminisha kuwa anakubalika na Watanzania.Hawa wanataka waendelee kulinda masilahi yao binafsi.Wanamhadaa kwa sababu yeye hana uwezo wa kuchunguza ili kubaini hisia halisi za Watanzania.

2.Wasaidizi wa aina hii ni wale wasiomkubali Mama.Wanachofanya ni kumharibia kwa kufanya utekaji,kuzuia maandamano ya Chadema nk
 
naunga mkono mia kwa mia kuhusu Dr.samia na uchaguzu mkuu2025

kuhusu chadema kua na mgombea urais mwanamke, sidhani kama linaweza kutokea kwa mazingira yale ya uongozi wao yalivyo,

na ukitazma vizuri kwa undani unaweza kuhitimisha kwamba, chadema na wanawake ni kama maadui fulani hivi wakubwa, mithili ya paka na panya tu, au israel na hamasi
 
Huu udokta wa kupeana kichawa ipo siku utawaumbua.
Eti Dr.clock100😁, wakati kichwani zimejaa taarabu tu.
 
Kuna mkubwa mmoja anasema mama yenu ameshindwa kazi, na yeye binafsi analielewa hilo,tatizo ni kwa chawa ambao wananufaika sana na uwepo wake pale kitini.

Hao chawa wanamwambia kuwa bila yeye mama kuendelea 2025, miradi yote ambayo ni kama legacy yake ambayo haijaisha, haitakamilika, hakutakuwa na alama yake.

Pia chawa hao wanamwambia kuwa wananchi wengi wanapenda na kutaka aendeee kwani amefanya mambo makubwa sana baada ya miaka 6 ya uharibifu wa yule jamaa.
Yaani amelijenga upya Taifa, hivyo wananchi wanataka aendelee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…