Kuna kitu tunafichwa Simba SC kuhusu hizi sajili

Kuna kitu tunafichwa Simba SC kuhusu hizi sajili

Timu imekua na usajili wa hovyo sana, wacheza wanaosajiliwa wengi ni free agent, nina mashaka kama ni pendekezo la kocha. Sijui kama kuna kitengo cha scouting kinafanya kazi yake vizuri.

Hapa ndipo ninapomkumbuka marehemu Zakaria Hans Poppe ni kama simba mzigo (pesa) hakuna.

Siku hizi wanachezesha kamari ya shabiki bingwa muda sio mrefu ukweli utajulikana.
Mashabiki sometimes watapiga kelele kwanini timu zinachukua Wachezaji walioachwa? Wachezaji waliomaliza mikataba ama wachezaji ambao wametemwa sehemu na wengine wataenda mbali kuwa labda wanatoka Ligi dhaifu ama hazina ushindani mkubwa, lakini Shabiki huyo anasahau nae ana jukumu lake la msingi.

Mashabiki wa Kariakoo hizi timu zenu haziwezi kufanya mambo kama Mamelodi Sundowns wala Al Ahly kwakuwa ninyi hamna sifa hizo, Mamelodi anamtaka Kiungo mwingine mwenye thamani ya Billion 6.2 ukijumlisha na Marco Allende aliyepo pale ni sawa na Billion 12 ambazo ni bajeti za Simba na Yanga kwa msimu, mwenzako kalipia usajili, imagine.

Kuingia kwenye soko la ushindani Afrika ni labda Simba na Yanga zimilikiwe na Mtu binafsi kama Sundowns ama Mazembe lakini kwa mfumo wa Wanachama ni lazima uwe imara kama Al Ahly na Zamalek, ambapo hapa kwetu ni kama bado elimu haijafika vizuri, hatujaelewa na bado hatutaki kuelewa.

GSM na MO hawana cha kulaumiwa, imagine suala la Wanachama, Yanga waliochukua kadi na kulipia ada zao za Wanachama kwa taarifa nizonazo hawafiki 25,000 nchi nzima jaribu tu kufikiria Al Ahly mtoto mdogo analipa ada 105,000 kwa mwaka, huyu unaenda kushindana nae vipi? Hapo Simba wangapi wana kadi za Mashabiki?

Matajiri wanabeba mzigo mkubwa na ni kama Mashabiki wameziacha timu mgongoni mwao, wapo pembeni wanasubiri Kariakoo Giants waishi kama Giants wa Afrika, hiyo ni ngumu bila Mashabiki kubadilika basi timu zitaishia kugombania wachezaji wa Ligi Kuu, watapishana kubeba Ligi Kuu na watakuwa na vikosi vya pili ambavyo vitashindwa hata kubeba Mapinduzi Cup.

Wachezaji wakubwa na wa maana wapo, wachezaji wenye thamani wapo ila pesa yote anatoa nani? Upande wa Mashabiki na wanachama wana support gani? Zaidi ya kusubiri vipaza sauti ya waandishi kuwakosoa Matajiri mambo yasipoenda sawa.

Yaani tununue pikipiki kutoka India halafu tuliite Mercedes Benz??___ Utasikia WATUACHIE TIMU ZETU, hamna cha kufanya bwana Masela, mara ngapi mlibaki nazo hizo timu zenu tukaona Yanga ya bakuli na Simba ile ya usafiri wa Coaster mpaka Songea.

By.Farhan JR
 
simba walipewa $ 1m kwa ajili ya maandalizi ya african football league, jiulize hizo pesa zilienda wapi.......

yani $ 1m usajili waliofanya sijui kama walitumia hata tshs 300m,....... pale simba kuna wahuni wanapiga sana pesa!
Timu ya MO ile lazima avune faida

Sent from my SM-N975U using JamiiForums mobile app
 
Tupunguze lawama jamani! Tusubiri wacheze hata nusu msimu
 
Naona thank you zimechachamaa cha ajabu John Boko ataachwa..
 
Back
Top Bottom