Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Kama heading inavyojieleza,
Kwa siku hizi mbili nimeshuhudia nyuzi pamoja na post nyingi katika mitandao ya kijamii yenye malengo ya kumchafua Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa Kassim wakimtuhumu kuwa ndiye anayemwangusha namba moja.Baadhi ya post zimekuwa zikimtuhumu kwamba amekuwa huchukui hatua pale inapompasa.Binafsi ninasimama upande wa PM kwa hoja zifuatazo:
Kwanza kabisa kwa mujibu wa katiba ya JMT mwenye mandate ya kuteua na kuunda baraza lote la mawaziri ni Rais wa JMT, PM hana mamlaka ya kuteua au kuwajibisha mawaziri, Mwenye mamlaka hayo ni Rais.PM hupatiwa baraza akiwa kama mtendaji mkuu na msimamizi. Hana nguvu ya kuwawajibisha mawaziri kikatiba, ni sawa na kiranja mkuu, hawezi kumfukuza mwanafunzi shule, Mwenye uwezo huo ni mkuu wa shule. Je, kama Mwalimu mkuu hana uwezo kiutendaji wa kuwawajibisha na kuchukua hatua dhidi ya wale aliowateua, PM atafanya nini?
Pili, kuna ule msemo wanasema "Never outshine your master" ikiwa na maana kwamba kamwe usiwe mtendaji au usitende vyema kumzidi 'boss' wako. Nadhani hiyo ndiyo mindset inayotawala katika serikali kwa sasa.Sote tunafahamu utendaji wa aliyekuwa waziri wa fedha na sasa VP Mh Philip Mpango, alipoingia katika kiti chake alianza kwa spidi kali wengi wakasema anaonekana yeye ndiye Rais lakini sote tunafahamu kilichofuatia, Hatimaye akanywea ghafla na ile kasi yake ikapotea kabisa. Kwa mentality hii ni vigumu kwa PM kutenda kazi zake katika 100% capacity kwa kuhofia kibarua chake.
Tatu, Hakuna asiyejua kwamba hivi sasa genge la walamba asali limerejea kwa kasi kubwa, Aidha Namba moja huenda hafahamu au anafahamu au naye analamba asali pamoja nao. Unapofanya kazi katika mazingira haya inakulazimu kuwa makini mno ili kulinda kibarua chako! Wengi wanafahamu utendaji wa PM na ni wazi kabisa kasi yake ni kubwa hata imani, uzalendo na utendaji wake ni zaidi ya boss wake na namna ya utendaji wake ni tofauti kabisa na Boss wake hivyo inamlazimu kupunguza kasi ili kwenda sambamba.Rejea aliyekuwa spika alipozungumza ukweli sote tunafahamu yaliyomkuta.
Hitimisho, Bila kupepesa macho ni wazi kwamba kati ya awamu ambayo inaonekana kufeli na kutokukubalika miongoni mwa watanzania wengi isipokuwa wale walioweka vidole vyao katika buyu la asali, Ni awamu hii ya Sita.Kwa utafiti usio rasmi, watanzania 9 kati ya 10 wanaonekana kutoridhishwa na utendaji wa serikali iliyopo.Kwa kutambua hili baadhi ya vijana walamba asali wametumwa kumchafua na kumuangushia jumba bovu PM ili kumsafisha namba moja kwa madhumuni ya kisiasa.
Kuna msemo wa kiswahili "mfa maji haishi kutapatapa" Nadhani mpango wao umeshafeli kwa maana hakuna mtanzania mjinga asiyetambua yanayoendelea. Tangu lini kiranja mkuu akaacha shule kisa wanafunzi wamelala njaa? Katiba imempa madaraka Rais kuisimamia na kuiongoza serikali yake na si PM inashangaza kuona mnataka kumtupia lawama PM! Hii inaonyesha udhaifu na kutowajibika kwa uongozi wa ngazi ya juu. INASIKITISHA