PostGE2025 Kuna kundi ndani ya Serikali linamuharibia Samia ili achukiwe na wananchi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Ndugu yangu hujawahi kuona mtu unachochewa ukaseme hivi,kumbe wanaokwambia lengo lao uzidi kujialibia,omba Mungu akupe maisha marefu mwisho wake utauona

Sasa hapo mjinga ni nani? Wachochezi wanakuchochea au wewe unaokubali ushauri wao. Kwanini usiwabadilishe?

Samia akiambiwa aue watoto wake Abdul, Wanu, Mwanaenzi, Mchengerwa atakubali kisa umepewa ushauri?
 
Hakuna washauri wala nini. Hata mimi mwanzoni niliamini hivyo. Ila kwa sasa nimegundua ana sifa ya kutojiamini! Ana uwezo mdogo kwa nafasi anayolazimisha kuikalia! Na pia ana roho mbaya.
Inashangaza kwa mtu kuibuka wakati huu na kudai Samia anashauriwa vibaya! Lakini ndio hivyo tena, watu tumeumbwa tofauti tofauti sana. Hata hivyo, ni jambo la kushangaza dunia, iwapo kuna mtu anaweza kuibuka na kuona rangi nyeupe ambayo binaadam wote wanaiona ni nyeupe; halafu yeye anakomaa kabisa kuwa hiyo rangi ni nyeusi!

Kuna mambo ya kawaida ambayo binaadam hushirikiana kuyakubali yalivyo. Hili la Samia "kuwa na washauri wabaya" linakuwa karibu zaidi na mfano wa hizo rangi hapo juu.

Huyu mleta mada, kaamua tu, aone hivyo anavyoona, huku vielelezo vyote vipo wazi kabisa kumwonyesha Samia mwenyewe akiwa ni mtu mwovu kabisa.
 
Ndugu yangu sisi watu wa ulimwengu wa kiroho kazi yetu ni kufikisha ujumbe kama ulivyo,iwe ujumbe utakuwa mbaya au mzuri sana na kusema nimekwambia mwisho wake mama ila wewe unajua alipotoka na alipo sasa,nikauliza hivi Samia ndiye yule mpole aliyependwa na wapinzani mpaka wakamkaribisha kwenye shughuri zao? Nini kilichomfanya mpaka kukataliwa na watu akabaki kutumia nguvu kubwa za kuuwa watu ili apendwe,nazani mpaka hapo unaweza kupata jibu
 
shangaa na wewe..
maana yake basi hatoshi na ni kilaza
 
Mkuu lile kumbato la furaha la Samia kumkumbatia Kikwete baada ya Samia kumaliza kufanya kiapo cha urais linaonyesha Samia kunogewa na utamu wa madaraka na hakuamini kama lile zowezi lingefanikiwa.
 
Nimewaza hivi pia...
Ila nilichogundua uraisi ni taasisi.... Kwamba inawezekana raisi haamui yeye kama yeye Ila maamuzi ya watu flani wanaomzunguka.
Sitaki kuamini niliyoshuhudia kwa Mara ya kwanza tangu nizaliwe kwamba yameidhinishwa na mwanamke ambaye kila mwezi anapokea mshahara kama Mimi.
Lakini pia mbona JK utawala wake unasifika kwa kuwapa wapingaji nafasi ya kutosha bila kuwakwaza imekuwaje awamu hii wakati mnasema yeye ndiye remote?
 
Sasa hapo mjinga ni nani? Wachochezi wanakuchochea au wewe unaokubali ushauri wao. Kwanini usiwabadilishe?

Samia akiambiwa aue watoto wake Abdul, Wanu, Mwanaenzi, Mchengerwa atakubali kisa umepewa ushauri?
Urais ni tasisi kubwa sana,huyu ni mwanamke tofauti na Magufuri naamini mambo mengi anategemea kufanyiwa madhara yake ndiyo hayo wakati kuna kundi linafurahia aharibikiwe yeye anabaki kuwa mnyonge wa nafsi anapokumbuka anaiachia inchi doa ambalo halitafutika milele kwa mambo yaliyoshauliwa na wengine na lawama zinamludia mwenyewe
 
Wanaomuharibia bila kujua ni masheikh wake na kikwete. Wewe hukuona siku ya UAPISHO wake walivyokumbatiana na Kikwete; ni kana kwamba aisee kumbe ulisema kweli-tumetoboa!
Na wapili hao masheikh wake ambao kila kukicha wanamuaminisha kuwa unapigwa vita kwa ajili wewe ni mama wa Kiislamu
 
Asante sana kama yupo hai Mungu amlinde
 

Hakuwahi kuwa na nia ya dhati ya maridhiano, kulipeleka mbele hili Taifa kwa kujenga umoja na ushirikiano.

Alifikiri akitoa hongo kwa wapinzani wote watatulia kama ACT, Chaumma, Mbowe. Kusudi lake kuu lilikuwa kufisadi Tanganyika yeye na Kikwete taifa bila shida.

Mambo yaliharibika kidogo Lissu, Heche waliposhinda Chadema dhidi ya Mbowe,Wenje. Polepole akajiuzulu, Tesha akatoa kauli.

Ameanza kuiba, kuteka, kuweka familia yake toka siku ya kwanza alipofika ikulu.
 
Mkuu lile kumbato la furaha la Samia kumkumbatia Kikwete baada ya Samia kumaliza kufanya kiapo cha urais linaonyesha Samia kunogewa na utamu wa madaraka na hakuamini kama lile zowezi lingefanikiwa.
Sasa watu ndiyo wanazidi kusukuma kete sasa hivi yuko kwenye kilele cha maumivu ya nafsi kesho atakuwa kwenye majuto na kiti chake watakuwa wamekalia wengine wakati yeye yuko gerezani au kaburini,
unakumbuka hotuba yake aligusia kwamba kuna watu wanautaka Urais,basi yajayo yanakuja,inabidi uwe na jicho la tatu
 

Kwanini asiwasikilize na kuomba ushauri kutoka kwa wanawake wenzake mahiri kama Netumbo Nandi-Ndaitwah, Mia Amor Mottley au Ellen Sirleaf?

Hawa ni watu waliojali haki za watu wao na watu wote duniani.
 
Ukweli ni kwamba ndio kund lililosababisha watu waandamane na ndio kund lenye jambo lao 9desember ndio kund lililompinga mama kwe uchaguz wa ndan wa chama kuchagua mgombea.urais gafla wakaibuka k8na mpina polepolegwajima na nk hawa ni speaker tu nyuma kuna wazee wa plan a be che na de mpaka ke
 
Kwa sasa Samia hana majuto yoyote hivyo lolote linalomtokea au litakalomtokea mbeleni ni matokeo ya alichokipanda tu, Samia wakati wa Magufuli hadi ilivuma kwamba alitaka kujiuzuru ila leo hii mpaka anasema wasiomtaka wasisubiri hadi kipindi chake kiishe.
 
Mkuu, hayo maswala ya kiroho nayo naona ni mkanyagano tu, maana hueleweki!

Kama hadi sasa humjui Samia halisi, wewe utakuwa ni mtu wa kipekee sana kama alivyo yeye.

Muda wote huu wa miaka minne bado mtu humjui asili yake ikoje?
Mtu anayeigiza upole mwanzoni ili akulaze akili, akirudia tabia yake ya kiasili bado utakuwa huamini kuwa kakufanyia ulaghai?

Hayo mambo mazuri yooote unayoyakumbuka wewe, pengine hayo ndiyo yaliyokuwa yanatoka kwa washauri wake wazuri, waliomtakia mema, kama wewe unavyofikiria hapa. Ushauri huo mzuri kashindwa kuendelea nao, kwa sababu hulka yake ya asili ni mtu mwenye uovu.

Sasa hao washauri wazuri wa mwanzo mbona huwataji hapa, badala yake unatafuta wabovu ambao wanaendana na tabia zake mbaya.
 
Hii desturi ya kuwaweka watawala kama vile hawakosei ni ya wapi?! Hilo kundi ndilo limewaweka ndugu zake vilaza kwenye baraza haramu la mawaziri?!
Hilo kundi ndilo lilimtuma mtu ambaye alikuwa mwenyekiti mwenza wa bunge maalum la katiba akebehi uhitaji wa katiba mpya?!
 
View attachment 3511071
Huyu ndio anaumia?? Mnyonge huyu???🤣🤣🤣
Ndugu yangu ungejua hali anayopitia mama katika ulimwengu wa kiroho inasikitisha sana,ingawa kwa macho ya kawaida mmnaweza kumuona yuko jasiri kwa matendo na maneno,lakini moyo unaumia na siri zake,
Ullisikia kisa cha Magufuri na bene sanane?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…