Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Mimi ni mkazi wa Mtaa wa Masimba upo karibu na maeneo ya Uwanja wa Ndege wa hapa Tabora, miaka kadhaa nyuma sisi wakazi wa hapa tulishuhudia mamlaka ya Uwanja wa Ndege ikipita na kuzungushia uzio maeneo yote ya Uwanja huo.
Lengo lao kuu ilikuwa ni kuweka angalizo ili Wananchi wasije wakaingilia maeneo ambayo walisema ni ya Mamlaka ya Airport lakini ajabu ni kuwa miezi ya hivi karibuni kuna watu walikuja waliojitambulisha kuwa ni Maafisa wa Wizara ya Ardhi wakatangaza kuwa wanataka watu wahame kwa kuwa walikuwa ndani ya eneo la Uwanja wa Ndege.
Ajabu ni kuwa walisema hivyo na kueleza maeneo hay oni yale ambayo yapo ndani ya umbali wa Kilometa 2 kutoka pale ambapo awaliishia awali.
Sisi Wananchi tukaenda hadi kwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini akaingilia na kusema kuwa Mamlaka hiyo inatakiwa kuzungumza vizuri na Wananchi kwa kuwa kama waliwaacha wakajenga na kuendelea maeneo hayo inakuwaje sasa hivi wanawaambia wameingilia maeneo ya Airport.
Ndipo Maafisa hao wakarudi na gia mpya wakasema wale wote ambao hawajaendeleza maeneo yao kwa maana ya kujenga wanatakiwa kujitokeza na ili wao wayachukue yawe yanamilikiwa na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege.
Hivi jaribu kufikiria hicho kinachoendelea hapo, bila shaka kuna upigaji, tunavyohisi ni kuwa kuna watu wachache kwenye Idara ya Ardhi wana nia yao ovu ndio maana wanaangaika wanakuwa hawana msimamo.
Jambo lingine linalotia shaka ni kuwa wakisikia kuna Wananchi wanataka kulifikisha suala hili kwenye Vyombo vya Habari wanakuwa wakali kwelikweli na hawataki kusikia hizo taarifa.
Tunachojiuliza kama ni kweli wao wanafuata haki na wana nyaraka zote za umiliki wa ardhi eneo hilo kwa nini wanaogopa Wanahabari na kwa nini wanataka kuchukua maeneo ya wananchi ambao hawajajenga tu baada ya awali wale waliojenga kugoma.
Tunaomba Serikali ngazi ya Mkoa iingilie kati hili suala kwa kuwa Wananchi wa hali ya chini tunaelekea kupokwa haki zetu kwa kuwa hatuna pa kusemea.
DC ASEMA AMEUNDA KAMATI NA AMEIPA WIKI MBILI
Akijibu hoja hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini, Mhandisi Deusdedit Katwale amezungumza na JamiiForums na kusema “Hilo suala nalijua, nimeshaunda Kamati Maalum inafuatilia itanipa ripoti ndani ya wiki mbili, inawezekana anayelalamika hivyo ni Dalali kwa kuwa nilifika eneo la tukio na kutoa maelekezo.”

==================================