Kuna madhara yoyote kula nyama ya mnyama aliyeuawa kwa sumu?

Kuna madhara yoyote kula nyama ya mnyama aliyeuawa kwa sumu?

hata mimi

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2017
Posts
1,356
Reaction score
1,442
Kuna kuku wangu hapa amekula sumu ya panya nikamkuta amelegea nikamuwahi kumchinja sasa hapa mguu nje mguu ndani kuhusu kumla.

Yaani kuna akili inanijia nimuepuke wakati huo si mara ya kwanza kula nyama ya namna hiyo basi nachanganyikiwa tu.

Nimeshakula nyama zilizotokana na ajali ya kugongwa na nyoka sana ila sumu ya panya sijawahi.
 
Achana nae usile nyama ambayo unajua imetokana na kusababishwa ni sumu.
Nasema tena usile vumilia na chimba shimo ufukie kabisa.

Umesoma na kuelewa vizuri?
 
Maisha magumu mpaka kwa wauza majeneza niamini mimi huwezi kufa kaanga na kakonyagi kahusike
 
Huyo hapo kuku mwenyewe halafu hapa nimeingiwa na mawazo mengine zaidi...

Nahisi amegongwa na nyoka kwa sababu;

1.Hivi hivi natafakari hapa nimeona bonge la mjoka wa kijani linajimwambafy maeneo yale yale nilipomuokota kuku

2.Kuku walikula sumu tangu asubuhi sana mara tu walipofunguliwa kutoka bandani

3.Ameacha watoto hao ambao bila shaka walikula wote sumu ila vifaranga ndo hao wanaendelea kupiga misele

4.Juzi pia kuku walikula sumu ya panya kwa macho yangu nikiwaangalia na hakuna aliyekufa

5.Hatahivyo, sina hakika ni kuku yupi alikula sumu asubuhi ya leo ila maeneo hayo nilimwona kuku huyo na vifaranga vyake ndomana nikahisi ni yeye ingawa...

6.Nilimfuatilia asubuhi yote nikajiridhisha yupo salama kabisa ndipo nikaondoka na ndipo...

7.Muda naandika huo uzi ndo nimetoka kumchinja na hakufurukuta wala kelele wala nini zaidi ya damu tu hiyo iliyomwagika...

Aidha, sijaona jeraha lolote katika kagua kagua yangu hivyo nimebakia on the horns of a dilema...

Jamani nyama ya kuku hii simnaijua wenyewe inavyokuwa, tena kuku wa kienyeji loo! Hebu nishaurini fasta mimi nisije nikapoteza au nikapotea bure
JPEG_20210705_131358_-239417294.jpg
JPEG_20210705_132011_1196255956.jpg
 
Achana nae usile nyama ambayo unajua imetokana na kusababishwa ni sumu.
Nasema tena usile vumilia na chimba shimo ufukie kabisa.

Umesoma na kuelewa vizuri?
Loh! Sawa nimesoma na nimekuelewa bosi
 
Inafikirisha sana, haya ndio mawazo ya baadhi ya watanzania!!!! We have a long way to go. Sijui ni kwa sababu ya umaskini au ni ujinga?
 
Back
Top Bottom