Kuna madhara yoyote kula nyama ya mnyama aliyeuawa kwa sumu?

Kuna madhara yoyote kula nyama ya mnyama aliyeuawa kwa sumu?

Wewe ndie mtu careless zaidi niliewahi muona toka nizaliwe. Kua serious kijana usipo angalia utakuja sababisha majanga kwa familia na majirani pia.

Nimesikitishwa na namna ulovyochinja huyo kuku na kumwaga damu yake namna hiyo ( hata kama hujali atleast chukua tahadhali kuepusha magonjwa kwa kuku wengine) na kikubwa zaidi unavyohandle hiyo sumu hapo. Kama kuku wameweza kula hiyo sumu inamaana hata wanyama wengine wanaweza kula pia ukiwemo wewe mwenyewe ( maskini sijui ndiyo hiyo iko kwenye matembele?).

Ningekua karibu ningekutandika makofi, How can a person be this stupid. Aisee! yani ukimla huyo kuku lazima utakua unamatatizo ya akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muache huyo kuku uliemchinja nje ya friji kwa siku zaidi ya tano, kama hakuna nzi na funza waliozaliana basi bado ana sumu mtupe. Kama kuna funza na mainzi yamejazana basi sumu imeisha ila nyama imeharibika,itupe. Hiyo kwa betting tunasema both time to score mtupe tu huyo kuku kwa usalama zaidi 🤣🤸🐒
 
Ukichinja damu ikamwagika, hilo moja, pili ukamkosha vizuuuri.. Sumu inapungua kama kuisha kabisa, ile concentration yake inapungua hatimae inakuwa haina madhara kwako.
 
Huyo kuku analiwa isipokuwa maini na firigisi. Halafu, ukimnyonyoa unaweza kuona alama kama amegongwa na nyoka. Ukiona hivyo, ondoa sehemu hiyo na uendelee na mambo yako. Usiache mboga kirahisi mkuu.
 
Kuna kuku wangu hapa amekula sumu ya panya nikamkuta amelegea nikamuwahi kumchinja sasa hapa mguu nje mguu ndani kuhusu kumla.

Yaani kuna akili inanijia nimuepuke wakati huo si mara ya kwanza kula nyama ya namna hiyo basi nachanganyikiwa tu.

Nimeshakula nyama zilizotokana na ajali ya kugongwa na nyoka sana ila sumu ya panya sijawahi.
Wewe Mzaramo unayekula na utumbo mkuu?

Sumu za kuulia wadudu, panya nk vikiua mnyama hubakia kwenye matumbo ni vema ukala nyama 'kavu', vya ndani unaachana navyo.

Mnyama ikifa kwa sumu ya nyoka wa aina yoyote ile, mle ummalize kila kiungo kwa kuwa sumu inayomdhuru ikiingia kwenye mzunguko wa damu ya mwili wake hugeuka na kuwa protine.
 
Watu wanakula ng'ombe aliyekunywa solution ya Sodium Cyanide na hawafi, WaTz tupo kama 56m kaza mzee Baba usitupe nyama
 
Huyo hapo kuku mwenyewe halafu hapa nimeingiwa na mawazo mengine zaidi...

Nahisi amegongwa na nyoka kwa sababu;

1.Hivi hivi natafakari hapa nimeona bonge la mjoka wa kijani linajimwambafy maeneo yale yale nilipomuokota kuku

2.Kuku walikula sumu tangu asubuhi sana mara tu walipofunguliwa kutoka bandani

3.Ameacha watoto hao ambao bila shaka walikula wote sumu ila vifaranga ndo hao wanaendelea kupiga misele

4.Juzi pia kuku walikula sumu ya panya kwa macho yangu nikiwaangalia na hakuna aliyekufa

5.Hatahivyo, sina hakika ni kuku yupi alikula sumu asubuhi ya leo ila maeneo hayo nilimwona kuku huyo na vifaranga vyake ndomana nikahisi ni yeye ingawa...

6.Nilimfuatilia asubuhi yote nikajiridhisha yupo salama kabisa ndipo nikaondoka na ndipo...

7.Muda naandika huo uzi ndo nimetoka kumchinja na hakufurukuta wala kelele wala nini zaidi ya damu tu hiyo iliyomwagika...

Aidha, sijaona jeraha lolote katika kagua kagua yangu hivyo nimebakia on the horns of a dilema...

Jamani nyama ya kuku hii simnaijua wenyewe inavyokuwa, tena kuku wa kienyeji loo! Hebu nishaurini fasta mimi nisije nikapoteza au nikapotea bureView attachment 1842195View attachment 1842199
Huku ni wapi?Location imenivutia
 
Kuna kuku wangu hapa amekula sumu ya panya nikamkuta amelegea nikamuwahi kumchinja sasa hapa mguu nje mguu ndani kuhusu kumla.

Yaani kuna akili inanijia nimuepuke wakati huo si mara ya kwanza kula nyama ya namna hiyo basi nachanganyikiwa tu.

Nimeshakula nyama zilizotokana na ajali ya kugongwa na nyoka sana ila sumu ya panya sijawahi.
Test kula halafu uje utuambie inanogaje.Omba tuu usijegeuka panya
 
Back
Top Bottom