Kuna madhara yoyote kula nyama ya mnyama aliyeuawa kwa sumu?

Kuna madhara yoyote kula nyama ya mnyama aliyeuawa kwa sumu?

Kuna kuku wangu hapa amekula sumu ya panya nikamkuta amelegea nikamuwahi kumchinja sasa hapa mguu nje mguu ndani kuhusu kumla.

Yaani kuna akili inanijia nimuepuke wakati huo si mara ya kwanza kula nyama ya namna hiyo basi nachanganyikiwa tu.

Nimeshakula nyama zilizotokana na ajali ya kugongwa na nyoka sana ila sumu ya panya sijawahi.
Toa utumbo firijisi na maini tupa hivyo vingine kula tuu bwashee.
Kwa mfano kidari au paja sasa sumu huko inafikaje sasa.
Kidaftari kikipita mi ntatoa 2000
 
Huyo hapo kuku mwenyewe halafu hapa nimeingiwa na mawazo mengine zaidi...

Nahisi amegongwa na nyoka kwa sababu;

1.Hivi hivi natafakari hapa nimeona bonge la mjoka wa kijani linajimwambafy maeneo yale yale nilipomuokota kuku

2.Kuku walikula sumu tangu asubuhi sana mara tu walipofunguliwa kutoka bandani

3.Ameacha watoto hao ambao bila shaka walikula wote sumu ila vifaranga ndo hao wanaendelea kupiga misele

4.Juzi pia kuku walikula sumu ya panya kwa macho yangu nikiwaangalia na hakuna aliyekufa

5.Hatahivyo, sina hakika ni kuku yupi alikula sumu asubuhi ya leo ila maeneo hayo nilimwona kuku huyo na vifaranga vyake ndomana nikahisi ni yeye ingawa...

6.Nilimfuatilia asubuhi yote nikajiridhisha yupo salama kabisa ndipo nikaondoka na ndipo...

7.Muda naandika huo uzi ndo nimetoka kumchinja na hakufurukuta wala kelele wala nini zaidi ya damu tu hiyo iliyomwagika...

Aidha, sijaona jeraha lolote katika kagua kagua yangu hivyo nimebakia on the horns of a dilema...

Jamani nyama ya kuku hii simnaijua wenyewe inavyokuwa, tena kuku wa kienyeji loo! Hebu nishaurini fasta mimi nisije nikapoteza au nikapotea bureView attachment 1842195View attachment 1842199
Mbula hapo ndio kwako?
 
Kwanini ule vitu vilivokufa kwa sumu una njaa Sana au shida Nini?
Maisha ni muhimu kuliko kula vibudu
Kwa madai yake alimuwahi akiwa amekegea [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Wewe ndie mtu careless zaidi niliewahi muona toka nizaliwe. Kua serious kijana usipo angalia utakuja sababisha majanga kwa familia na majirani pia.

Nimesikitishwa na namna ulovyochinja huyo kuku na kumwaga damu yake namna hiyo ( hata kama hujali atleast chukua tahadhali kuepusha magonjwa kwa kuku wengine) na kikubwa zaidi unavyohandle hiyo sumu hapo. Kama kuku wameweza kula hiyo sumu inamaana hata wanyama wengine wanaweza kula pia ukiwemo wewe mwenyewe ( maskini sijui ndiyo hiyo iko kwenye matembele?).

Ningekua karibu ningekutandika makofi, How can a person be this stupid. Aisee! yani ukimla huyo kuku lazima utakua unamatatizo ya akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] anastahili makofi mengi sana
 
Kula ila maziwa yawe jirani jirani.

Hapo ni wapi. Aise jf iko kote kote, its good environment
Kwamba akihisi tumbo linaanza kukoroga atupie kitu Cha maziwa.....😂😂😂😂😂
 
Huyo kuku analiwa isipokuwa maini na firigisi. Halafu, ukimnyonyoa unaweza kuona alama kama amegongwa na nyoka. Ukiona hivyo, ondoa sehemu hiyo na uendelee na mambo yako. Usiache mboga kirahisi mkuu.
Mkuu maini na firigisi si ndo vit venyewe ivo vit vizuri,,
Mi mnavyohubiri kumtupa siwaelewi kbsa,
Hizi kuku kafa na sumu namkaanga vizuri na mafuta sumu bado inakuwepo wakuu,,
 
Back
Top Bottom