Huyo hapo kuku mwenyewe halafu hapa nimeingiwa na mawazo mengine zaidi...
Nahisi amegongwa na nyoka kwa sababu;
1.Hivi hivi natafakari hapa nimeona bonge la mjoka wa kijani linajimwambafy maeneo yale yale nilipomuokota kuku
2.Kuku walikula sumu tangu asubuhi sana mara tu walipofunguliwa kutoka bandani
3.Ameacha watoto hao ambao bila shaka walikula wote sumu ila vifaranga ndo hao wanaendelea kupiga misele
4.Juzi pia kuku walikula sumu ya panya kwa macho yangu nikiwaangalia na hakuna aliyekufa
5.Hatahivyo, sina hakika ni kuku yupi alikula sumu asubuhi ya leo ila maeneo hayo nilimwona kuku huyo na vifaranga vyake ndomana nikahisi ni yeye ingawa...
6.Nilimfuatilia asubuhi yote nikajiridhisha yupo salama kabisa ndipo nikaondoka na ndipo...
7.Muda naandika huo uzi ndo nimetoka kumchinja na hakufurukuta wala kelele wala nini zaidi ya damu tu hiyo iliyomwagika...
Aidha, sijaona jeraha lolote katika kagua kagua yangu hivyo nimebakia on the horns of a dilema...
Jamani nyama ya kuku hii simnaijua wenyewe inavyokuwa, tena kuku wa kienyeji loo! Hebu nishaurini fasta mimi nisije nikapoteza au nikapotea bure