Kuna madhara yoyote ukiachana na mtu ambaye ushamlipia mahari na kumvisha pete ya uchumba?

Kuna madhara yoyote ukiachana na mtu ambaye ushamlipia mahari na kumvisha pete ya uchumba?

Wana JamiiForums hope mko poa kabisa

Naomba kuuliza hili maana linanitesa sana. Mimi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye nimemlipia mahari na nikamvalisha pete.

Ila mimi baada ya kuona haeleweki nikampotezea. Swali ni kuna madhara yoyote ukiachana na mtu ambaye ushamlipia mahari na kumvisha pete ya uchumba.
Pole Sana..
 
Huyu ni msumbufu, muacheni msipomjibu ataondoka mwenyewe. Ndiyo mtu anayemiliki ID's nyingi JF. Nyingi zimepigwa Ban na kila leo anaanzisha mpya. Huyu ndiyo yule huwa anadislike kila comment. Kipensili huyu...
Walishe hawa matonya wa JF mamalishe usiwafanyie hivyo wengine Mchana wao unapita kwa tabu sana usiku ndio balaa zito badala ya Vocha nasuggest uwakusanye eneo 1 uwapigishe hata pilau Kuku wakienyeji utabarikiwa sana tena ukiweza piga tour Mkoa kwa Mkoa
 
Wana JamiiForums hope mko poa kabisa

Naomba kuuliza hili maana linanitesa sana. Mimi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye nimemlipia mahari na nikamvalisha pete.

Ila mimi baada ya kuona haeleweki nikampotezea. Swali ni kuna madhara yoyote ukiachana na mtu ambaye ushamlipia mahari na kumvisha pete ya uchumba.
Madhara ni gharama ulizokwisha toa, maana haziwezi kurudishwa ama kurudishwa kwa mafungu tena kwa kipendaroho cha wazazi, maana wanakuona kama unawaletea 'salala' kwa binti yao.

Lakini kuna tukio mimi nililishuhudia kama la kwako, hapo kasoro na tofauti ni dhamira zenu tu.

Kuna jamaa alifanya process zote hizo kama ulizofanya wewe, kishika uchumba na mahari kabisa kumbe lengo lilikuwa ni kumvua tu chupi huyo binti.

Binti aliposhawishika 'kutoa' kabla ya ndoa ndiyo ikawa kantolee.

Tena jamaa likawaacha tu na maandalizi yao ya harusi, ndoa kuandikishwa wakaenda wote kanisani na mambo yote kufanyika, lakini siku ya ndoa, jamaa ndiyo likatokomea kusikojulikana.

Gharama za mahari kitu gani bhana?
 
Ukifanikisha kumwacha,,Tafadhali! Nipasie namba za huyo binti kama hutojali lakini,,kwa maana Mimi mwenyewe sielewi pia
 
Walishe hawa matonya wa JF mamalishe usiwafanyie hivyo wengine Mchana wao unapita kwa tabu sana usiku ndio balaa zito badala ya Vocha nasuggest uwakusanye eneo 1 uwapigishe hata pilau Kuku wakienyeji utabarikiwa sana tena ukiweza piga tour Mkoa kwa Mkoa
Wewe ni mwanaume kwanini usifanye hivyo? Una uhakika gani nje sifanyi makubwa? Hunijui so relax acha kuniquote kila nachoandika kwenye nyuzi za watu, unaharibu mijadala. Mbona imekuuma sana, ulikosa vocha mtandao gani nikutumie PM mkuu. Vitu vidogo sana hivyo. Watu wanawaza kwenda kuishi sayari mpya wewe uko na mambo ya chakula. Kuna jela mkuu
 
Walishe hawa matonya wa JF acha kujitetea
 
Hapana hamna madhara kwa mwachaji ila mwachwa.
Juzi Mheshimiwa Gwajima amempongeza kaka aloamua Fanya sherehe ya harusi bila bibi harusi. Jamii ina matukio mengi ya kiza (siku Moja kabla ya harusi unamkuta mwenzio Yuko na love bites shingoni Ili hali hamjaonana kimwili wiki/mwezi hahaaaa)
 
Nimekushangaaa zaidi ya mara7000!!!

Yaani umegundua haeleweki kisa machozi uingie naye kwenye ndoa?

Aisee heri nusu Shari kuliko Shari kamili mkuu. Mwache alie ajutie ujinge wake na aambiwe nimeamua kukuacha Kwa sababu ABC sitaweza.

Wanawake wanatuacha hata kama kesho ni harusi yenu anatoroshwa na mwingine!!
Nimeandika kama kosa ni lako, lakini, kama yeye ndiye mwenye makosa huna hatia.

Elewa nilichokiandika mkuu.
 
Wana JamiiForums hope mko poa kabisa

Naomba kuuliza hili maana linanitesa sana. Mimi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye nimemlipia mahari na nikamvalisha pete.

Ila mimi baada ya kuona haeleweki nikampotezea. Swali ni kuna madhara yoyote ukiachana na mtu ambaye ushamlipia mahari na kumvisha pete ya uchumba.
Unlesss kama atakufanyia kitendo kibaya na cha hovyo - vinginevyo Pete ya uchumba ni KIAPO.

Viapo vina maana sana katika ulimwemngu wa roho.
 
Tena shukuru Mungu kakuepusha na tatizo muache haraka sana, andaa sababu zako nenda kaombe mahari yako wakikupa au wakigoma achana nao kikubwa ww umejiepusha na tatizo ambalo lingekugharimu maisha yako yote.
 
Mi mwaka jana nilienda uchumba na tukakubaliana mahali lakini baadae nafasi yangu iligoma kabisa... Nikaachana nae japo ilikua ngumu lakini niliweza

Sasa nimeoa na Nina mwanamke ninayempenda sana na mtoto kanizalia
 
Back
Top Bottom