Wacha wenye meno wasuguane mpaka tupate Jibu.
1.Hata mm hapo kwnye Sensa kutumia Mafuta badala ya umeme sikumuelewa huyu Bandugu.
2.Nadhani kinachodertermine ulaji wa mafuta ni uchomaji wa mafuta kupitia Nosel kwnye plug na hii inatokana na kuminya acellerater ambapo Utupwaji wa mafuta ya Pressing ya acellerater inaonekana kwenye RPM... kama RPM ipo low Basi mafuta pia hutupwa kidogo.
Maana yake Basi Netraul hupelekea RPM kua Chini na matokeo yake mafuta kutumika kidogo. (Akili zangu binafsi/bila mwalimu).
Haishauriwi kueka Gari Neutral ukiwa kwenye mteremko, kwa sababu gari iyashuka kwa haraka sana, unapokuwa katika gia wakati unateremka, speed ya ushukaji inakuwa controlled, inasaidia kusimama haraka na breki, ila ikiwa inashuka fasta wakati unabrake utachelew kusimama na breki zitalika na kupata moto fasta.
Tumia neutral pale ambapo gari inahitaji kuvutwa ikiwa imekuharibikia.
Sensor zinahusika sana kwenye suala zima la unywaji wa mafuta. Kuna Mass Airflow Sensor na nyengine Oxygen Sensor.
MAF inakaa maeneo yanayoingiza hewa kwenye mashine, utaikuta maeneo ya Air cleaner na O2 inakaa kwenye exhaust manifold/maffler ya mwanzo kutoka kwenye engine. Unapokanyaga accelerator, thottle body inafungua mdomo kupitisha hewa kwenda kwenye combustion chamber, hapa hii MAF inaiambia ECU kuna hewa kiasi fulani imeingia, baada ya information hio ECU inajua ni kiasi gani cha mafuta yanahitajika kwenye engine. Baada ya mripuko kwenye engine, hewa ilokuwemo ndani inatolewa kwenda kwenye Exhaust, huku ndio kuna O2 sensor, ambayo itaiambia ECU ya gari kiasi cha oxygen kilichomo kwenye hewa ilotolewa, hapa ECU itatambua uripuaji uliofanyika kama Hew ilikuwa nyingi kuliko mafuta au mafuta yalikuwa mingi kuliko hewa, na kuifanya ECU hio kufanya marekebisho ili hew na mafuta yawe sawa. Sensor hizi mbili zikifeli, Gari litakunywa mafuta na perfomance itakuwa mbaya.
Plug ama coils zikiwa mbaya, gari itakuwa ina miss, hii ni kwa sababu kwenye engine, cylinder yenye plug/coil mbovu itakuwa haichomi mafuta yanayoingia, In theory, mafuta yanayokwenda ndio yale yale, ila yanakuwa wasted bila ya kupatikana nguvu yoyote, itakuwa inakunywa mafuta bila sababu. Pia chengine kinachochangia unywaji wa mafuta, ni fuel injectors, hizi zinatakiwa zikipuliza mafuta ni mfano kama vapor tu, lakini ikianza kutoa mafuta mfano wa mkojo, gari litakuwa lina mripuko mbovu na mafuta yatakuwa yanakwenda mengi sana. kama umelaza gari, asubuhi ukaliwasha, utakuja kuona gari linatoa moshi mwingiiiiiii, hii ni kwa sababu kwenye hio cylinder mafuta yalikuwa yakichuruzika ndani kdg kdg, ila usiogope, once they are all burned out gari haitotoa moshi (ukiwa umebadili injector).