Kuna madhara yoyote ya kuweka "Neutral Gear" kwenye magari Automatic?

Kuna madhara yoyote ya kuweka "Neutral Gear" kwenye magari Automatic?

Habari

Wajuzi ni wengi humu hivyo naomba tuhabarishane
1. Je, kuna madhara yeyote yataweza kuikumbuka Gear Box ama Engine kwa ujumla kama ukiwa unaweka "N"/Neutral Gear wakati unaendesha sehemu yenye mteremko?

2. Je kuna uhalisia wa kusave mafuta kwa kuweka Neutral Gear? Na kama kweli inasaidia je ni kiasi gani cha mafuta hupunguzwa wakati wa gari ikiwa kwenye gear hiyo?

Ahsanteni.

Kuna siku nilitaka kufa niliweka Neutral aisee huwezi irudisha wakati gari inatembea ilibidi nipunguze mwendo na kulizima kwanza gari, na unaweza kuua gear box
 
Ndio, hili ni jambo zuri. Unapunguza kuisha kwa breki. Kama unataka kushuka kwa spidi mlimani, hukutakiwa kuweka neutral in the first place.

Ukiweka neutral gari inakuwa unbalanced/unstable na kuwa kama jiwe linaloroll mlimani na ni rahisi kupoteza control hasa ukitakiwa kuswerve.

Kama unataka kushuka mlima kwa spidi kanyaga mafuta na acha gari ichague gia kubwa zaidi ishuke nayo. Kama unataka kushuka mdogo mdogo achia mafuta na acha gari ifanye engine braking na kupunguza kuisha kwa breki zako.
Nmekusoma kiongozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini nikanyage mafuta wakati lengo langu ni kuokoa mafuta kwa kutumia available potential energy ya slope iliyopo badala ya kuunguza mafuta yangu unnecessarily?
Mkuu legeza ubongo, nilichoelewa mm ni kwamba hizi gari sio Auto kwenye gear tu! Kumbe yaezekana inapokua kwenye down la maana/mteremko mkali ina ji-auto pia na vitu vngine ikiwemo fuel consumption, kuieka "N"/neutral ukiwa kwenye motion ni kuibadili gar kutoka Auto kwenda manual jambo ambalo sio zuri/sahh kwa usalama wa gari na dereva/watumiaji wengine wa barabara.Tusiendeshe kwa mazoea jaman

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku nilitaka kufa niliweka Neutral aisee huwezi irudisha wakati gari inatembea ilibidi nipunguze mwendo na kulizima kwanza gari, na unaweza kuua gear box
Ulizima gari wkt inatembea?,hahah bro shukuru sana Mungu.
 
Gari umeshaambiwa inakula lt1 kwa km10 mfano sasa we ukiweka neitral au usiweke consuption iko palepale.kuna watu wanaamin kwamba AC inakula mafuta.AC inawezekana inakula mafuta lakini si zaidi ya kuendesha gari vioo viko wazi!vioo vikiwa wazi upepo unakusukuma nyuma na we unaongeza mafuta kwenda mbele hapo ulaji utaongezeka sana tu
Kufungua vioo upepo ufanye ukinzani ni kuanzia speed 60 kwenda mbele ndo hyo dragg itafanya kaz,below that dragg haina effect

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hivi gearbox ya auto hufanya shifting kwa kuzingatia pressure ya oil kwenye gearbox, ambayo presha hutengenezwa nanaccerelation ya gari inayotoka kwenye matairi yanapozunguka. So unapoweka neutural unatenganisha engine na gearbox hivo engine inabaki iddle huku speed inakuwa kubwa. Na engine ikibakia iddle maana yake geabox nayo inazunguka kufuata mizunguko ya engine hivyo ukiweka kwe nye D wakati gari ina speed. 60+ basi utailazimisha gari itoke no1 hadi 3 kwa lazima coz pressure inakuwa ndogo kwenye oilm labda ukitaka kurudi D basi piga breki gari isimame kabisa halafu ndo uweke D uendelee na safari. Vinginevyo una shorten maisha ya gearbox yako
Hii ndo point sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa unashuka mlima na ukaweka D si RPM sawa na ukiweka N, N ni kwamba engine inaenda kwenye Idle kabisa, kuna tofauti kubwa sana; na ukisema inakata mafuta maana yake inazima? Si kweli huwa haizimi, au unamaanisha inaounguza RPM? Sasa ikipunguza RPM na ikiwa iko connected na gear box (ipo kwenye D) maana yake engine ina act kama brake na kupunguza speed, solution ni kuweka N ili upate maximum speed with minimum RPM (idle)
Kama hujawai endesha manual, kuna mambo mengi yatakusumbua, gear ikiwa engaged D inaslow down gari
 
Unawekaje N kwenye jam Mzee baba, apo P ndo mahali pake, ukiweka N gari unakuwa iko free, at a mtu akisukuma unaenda, hujawah endesha manual??
Ukiwa kwa foleni 'N' kuitumia ni sahihi, masuala ya mtu kukusukuma mpaka gari ikamove hayo ni mengine sasa maana sio rahisi tu eti upo Neutral kwa foleni mtu akaja sukuma gari kidog ikaanza mwendo, lakini vile vile kuweka 'N' haimaanishi gari haitakuwa na brake (ikiwa 'N' bado na brake unaweza shika).
Brake hukosekana pale tu gari inapokuwa imezimwa on motion (ingawa kuna muda huwa gari inazimika na bado naweza kanyaga brake) zaidi ya hapo uweke 'P' or 'N' bado brake zitakuwepo tu!.
 
Wala haisev mafuta kivile, iache gari kwenye D then teremka mteremko ukiwa hujakanyaga moto huku ukiaangalia rpm, then rudi juu weka kwenye N teremka ukiangalia rpm utakuta tofauti ndogo sana so ili usev nusu lita labda gari itembee 20km ikiwa N. Ukilinganisha kusev mafuta na uharibifu utakaotokea in logrun utaona damage ni kubwakuliko mafuta utakayobana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom