Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Salam,
Tunaendelea katika episode nyingine ya 'MZINDUE AWESO MAJI YAREJEE', na leo tumpe mbinu nyingine ya kujua uhalisia wa kinachotokea mtaani. Yaani hii wiki inaenda kuisha kule Mbezi Beach maji yametoka haijazidi siku moja, afu Waziri Wizara ya Maji huko anajitapa tu maji yapo na chawa wake wajinga wanamwambia maji yapo aachane na kelel za mtandaoni, useless kabisa!
Sasa Aweso Wizara ya Maji mbinu hii nakupa uache kutupa majibu yako yenye 0 research, kwenda kwenye maeneo ya wananchi physically unaweza kusema huwezi kujigawa, hamna tabu, basi tumia njia hii itakayokusaidia kupata taarifa za ukweli katika maeneo yote kwa wakati mmoja.
Kwenye maeneo yetu tuna groups za WhatsApps za DAWASA, ambayo kote mameneja wa DAWASA wapo ambao wanasimama kama wawakilishi wako na ndio ambao wanakulisha taarifa za uongo na wewe unazibeba kama utafikiri huna uwezo wa kuzihakiki.
Omba links zote za group za WhatsApp kwenye maeneo yote yenye malalamiko halafu unakuja kujitamba maji yapo, ingia kwenye group hizo zote kwa kutumia namba tofauti ambayo watendaji hawa hawana, waambie waseme kero zao sababu umeona wananchi wanasema maji hayapo wakati kwa ufahamu yako unajua maji yapo ya kutosha. Wizara ya Maji
Wananchi watafunguka utapata uhalisia wake, ukipata majibu tunaomba pia uje useme umegundua nini na nani anakwamisha wananchi tuspate maji. Ukiendelea kukaza fuvu na njia zote unazo za kupata habari za uhakika utakuwa umeamua mwenyewe kujiharibia.
Kwenye malalamiko ya wananchi hao machawa wako wanaokaa kusifia kwenye kila kitu waweke pembeni ufanye kazi, hata ukiondolewa wao hawana hasara, watahamia kwa Boss mpya.
Ukishupaza shingo na hapa utakuwa sikio la kufa Wizara ya Maji