Tayana-wog
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 24,844
- 29,126
Shukuru Mungu mkuu, anakuonyesha yajayo Halafu ww hutaki.Ni ndoto ambayo sintasahau sijui kwa nin
Ni matokeo yangu ya kidato cha sita
Usiku mmoja nliota ndoto matokeo yametoka na nikaona daraja nililopata na point kadhaa ndotoni nikashtuka usingizini na jasho kama nimenyeshewa na mvua
Ndoto ilinitesa sana na baada ya week tatu mbele matokeo yalitoka nikiwa na daraja lile lile na point zile zile
Sijui mpaka leo ni nini kile hua sitaki kuamini na siamini ndoto ni maisha yetu ila ile sijui ni nin kilitokea huu ni ukwel mtupu
Hii ndoto inanisumbua kweli, imeshajirudia rudia mpaka nashindwa kuelewa ni nini....
Naota mafuriko afu eneo lile lile, wakati mwingine yananichukua lakini ghafla yanakauka. Wakati mwingine nakimbia hayanikuti, wakati mwingine nahangaika lakini nafanikiwa kutoka katika hayo mafuriko.
Msaada wenu ni wa muhimu sana kwangu, hata hii leo nimeota kuhusu mafuriko...
Nilikuwa na rafiki yangu (tena ni member hapa JF) akiendesha gari nami nilikuwa upande kwa kiti cha abiria. Ghafla mafuriko yakaja barabarani na kuibeba gari tuliyokuwemo ila bahati nzuri tukafanikiwa kutoka salama...
JAMANI HIZI NDOTO ZINANIKOSRSHA RAHAAAA.... NINI MAANA YAKE?? MAKE ZINAJIRUDIA MPAKA KEROOOO....
C.c
. Mzizikavu, mshana jr, Pasco, NDUKI, Rakims na wengine wenye uelewa kuhusu ndoto...
Vijana wataota ndoto na wezee maono, heri wewe umejionea mafuriko, nikusihi kuwa Mungu wetu ni wa utaratibu, naye huwajibu wamwombao. Je uliwahi kukutana na Nguvu ya Mungu katika ndoto, maono yako!? Endelea kubisha hodi Roho Mtakatifu afungue, kwa usikivu, utafunguliwa na kuona yote kwa uhalisia wake na tafsiri yake,... Basi Daniel akaitwa mbele ya Mfalme ili atoe hesabu ya yale mfalme aliyoyaona,,, tegemegea muijiza wake Mungu kutua Kwako live,,,,
Nashukuru Mkuu kwa mchango wako... Ndio huwa kuna ndoto nikiota huwa zinakuwa kweli, na kuna nyingine huwa zinakuwa na ishara flani. Nikiota najua kuna jambo. Ila hii imenishinda kuelewa....
Naifanyia kazi ntakachoona will let you know mamiii. HONGERA.
Msaada wenu ni wa muhimu sana kwangu, hata hii leo nimeota kuhusu mafuriko...
Nilikuwa na rafiki yangu (tena ni member hapa JF) akiendesha gari nami nilikuwa upande kwa kiti cha abiria. Ghafla mafuriko yakaja barabarani na kuibeba gari tuliyokuwemo ila bahati nzuri tukafanikiwa kutoka salama...
JAMANI HIZI NDOTO ZINANIKOSRSHA RAHAAAA.... NINI MAANA YAKE?? MAKE ZINAJIRUDIA MPAKA KEROOOO....
C.c
. Mzizikavu, mshana jr, Pasco, NDUKI, Rakims na wengine wenye uelewa kuhusu ndoto...
Habari wana jf
Naomba niwashirikishe ndoto yangu
Nikiwa chuo mwaka wa pili semister ya kwanza tulikuwa katika chumba cha mtihani mchana,tulikuwa tunafanya Financial Accounting kiukweli yale maswali nilikuwa nayafahamu ajabu wakati naanza kufanya ule mtihani ilinitokea hali ya tofauti,nilifanikiwa kufanya swali moja tena ilikuwa ni nusu tu swali na nikashangaa masaa 3 yameisha bila kumaliza maswali ya mtihani.Wakati natafakari cha kuandika nilishtuka hali ya kujisikia kufika kileleni kama vile nilikuwa nafanya mapenzi ili hali nimekaa kwenye kili tena chumba cha mtihani.Nilifanikiwa kupata supplimentary na Mungu alisaidia nikaclear.
Tokea hapo nimekuwa nikiota nafanya mtihani ila mtihani wenyewe unakuwa ni mgumu kupita maelezo na huwa sifanikiwa kujibu swali hata moja,halafu nashtuka najisikia kama nilikuwa nafanya mapenzi basi nachukia najikagua kama nimechafuka lakini hamna kitu.
Hii ndoto imekuwa ikinisumbua sana mambo ya kufanya mtihani ndotono kwa kweli sipendi
Je hii ndoto ina mahusiano gani na maisha ya kawaida kwa wale wanaofahamu
Hii ndoto inanisumbua kweli, imeshajirudia rudia mpaka nashindwa kuelewa ni nini....
Naota mafuriko afu eneo lile lile, wakati mwingine yananichukua lakini ghafla yanakauka. Wakati mwingine nakimbia hayanikuti, wakati mwingine nahangaika lakini nafanikiwa kutoka katika hayo mafuriko.
Hayo ni maono ya jambo lingine tofauti kabisa linalokuja kwa njia ya fumbo la ndoto hiyo sio ndoto kama ndoto nyingine za kawaida
Ndoto za kawaida hazinaga mwisho na mara nyingi haziko clear
Mi nahisi hiyo ni ndoto ya kawaida ila huenda inajirudia kwasababu huwa unaifikiria sana
Wakati mwingine ndoto ni mkusanyiko wa mawazo yetu, yale mawazo ambayo tungekuwa tukiyawaza ubongo huwa bado unayafanyia kazi ndomana tunaota.
Huwa unaota muda gani?
sasa naomba hapa kuuliza kidogo.. . kwan kuna uhusiano gani kati ya ndoto na mda???
aretasludovick njoo umsikie Jimena
Watu wanaoamini maswala ya nyota huwa wanasema kuna muda ukiota ndoto inakuwa na maana na kuna muda ukiota inakuwa ya kawaida. Sasa nimeuliza ili akishajibu nimuitie MziziMkavu
Jambo hilo laweza kuwa zuri au mshana jr unaonaje
Ni ndoto ambayo sintasahau sijui kwa nin
Ni matokeo yangu ya kidato cha sita
Usiku mmoja nliota ndoto matokeo yametoka na nikaona daraja nililopata na point kadhaa ndotoni nikashtuka usingizini na jasho kama nimenyeshewa na mvua
Ndoto ilinitesa sana na baada ya week tatu mbele matokeo yalitoka nikiwa na daraja lile lile na point zile zile
Sijui mpaka leo ni nini kile hua sitaki kuamini na siamini ndoto ni maisha yetu ila ile sijui ni nin kilitokea huu ni ukwel mtupu
Kuna baadhi ya situations sio ndoto hasa kuwangiwa lakini pia kuna baadhi ya ndoto ni maagizo au maelekezo kamili
Ndoto hii iliwahi kuwa kweli kwangu. Babu yangu alinitokea usiku nikiwa nimelala akanichukua tukaenda kukaa mahali ambapo ndio alikuja kuzikwa
Tulikaa pale tukaongea sana lakini sikumbuki mengi tuliyoongea zaidi ya mwishowe kuniaga. Kulipopambazuka simu ya kwanza ilikuwa ya kuniarifu msiba wa babu yangu niliyempenda sana na alikuja kuzikwa pale tulipokaa na yeye usiku