Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Ndoto ya aina hii uliwahi kumtokea mume wangu.
Yeye hakuwa na uhusiano mzuri na bibi yake, anasema wakati wako wadogo yeye alikuwa mtundu sana hivyo bibi yake alikuwa hampendi na mpaka alivyokuwa hali hiyo iliendelea ila hakujali na wala haikumsumbua. Siku moja alillala akaota bibi yake amekuja amemuomba msamaha na kumwambia amsamehe kwasababu anataka kwenda mbali ila hakusema wapi. Wakasameheana ndotoni. Aliposhtuka usingizini akasema hii sio ndoto ni kweli, akampigia simu mama ake na kumwambia nenda ukamuage bibi ila sijui kama utamkuta. Kesho yake asubuhi mama ake ndo aliepiga simu na kutoa taarifa ya msiba.
Hizi ndoto kweli zipo ila haziwatokei watu wote.
Zinaitwa ndoto maono au ndoto taarifa