Kuna mahusiano kati ya ndoto na maisha ya kawaida?


Zinaitwa ndoto maono au ndoto taarifa
 
Zinaitwa ndoto maono au ndoto taarifa

How I wish niwe naota kama hivyo. Yani ndoto zangu ni za tamthilia au series nazoziangalia, stori ikiwa ya kutisha sana pia naweza kuiota kama ilivyo na mbaya zaidi Mimi ndo nnaekuwa mhusika mkuu. Na mara nyingine huota ndoto za kawaida ambazo hazijawahi kuwa na maana yoyote katika maisha yangu wala ya yoyote yule na nyingine ndo huwa sizikumbuki kabisaa.

Nahisi nahitaji kupractice lucid dreams
 

Practice meditation ufungue mlango wa sita, hii ni level nzuri kuliko lucid dreams
 

Huwa naota usiku na alfajiri sana sana
 
Sali kabla ya kulala. Pia angalia ni vitu gani huvipitisha kichwani kwako kabla ya kupata usingizi.
 
ndugu zanguni naomba mnisaidie maana ya ndoto hii maana nimeiota mara kwa mara, huwa naota niko kwenye mto mkubwa sana smtyms nakuwa nimekaa pembeni, wakati mwingine navuka huo mto ,wakati mwingine naogelea na naweza ota nahangaika tu mtoni hapo...plz wat doez t mean jmn? Honestry inanitesa sana.
 
Ndoto ni kile unachokiwaza mara kwa mara kutwa.. Ndoto hubeba uhalisia
Kama lile unaloota halitakutokea leo bas sku nyingne

Mnashauriwa kusali kabla ya kulala kuepeuka kuota ndoto mbaya maana unaweza ukaita unaliwa na simba porini na kufa na kweli ukafa kweli asubuh usiamke teh
 
Mimi toka niko Pre-form one imekuwa kawaida yangu sana kuota nafanya mtihani na wakati wote nikiingia kwenye pepa naikuta vivyo hivyo na kila kitu kinaenda kama kilivyokuwa kwenye ndoto.
Ndoto ambayo sitaisahau ni pale nilipoota nafanya mtihani wa Kemia maswali yote yalikuwa mboga kabisa ila sikuweza kumaliza maswali kwa kuwa nilichelewa kuingia kwenye pepa; sasa baada ya kuona nimeota kuwa nimechelewa kuingia kwenye pepa ile tu nilivyostuka toka kwenye ndoto niliamua kukaa hadi asubuhi ili nisichelewe pepa na kweli sikuchelewa ila nilivyingia kwenye chumba cha mtihani na kukuta maswali yote ni simple na ni yale yote niliyoota nikawa dharau kwa pepa ile cha ajabu muda uliisha kabla sijamaliza mtihani-lilibaki swali moja na niliscore 97% ila nilijuta japokuwa kwa upande mwingine nilifurahi kwa kuwa nilikuwa nimeota kuwa sikuweza kumaliza mtihani wangu huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…