Kuna maisha baada ya kifo au tukifa ndio mwisho wa kila kitu

Kuna maisha baada ya kifo au tukifa ndio mwisho wa kila kitu

Ile ni reaction tu ya ubongo kwa matukio tunayopitia pamoja na kumbukumbu halafu tofautisha kuota ndoto na kufa..kufa maana yake kwishnei hutoota ndoto hutohisi njaa hutohisi nyege halafu kuhusu ndoto sio kitu cha ajabu ukumbuke hata mahindi nayo yanaota.
pole
 
ni circle ukifa anazaliwa mwingine exactly mwenye gins zako kwahiyo ndio hivyo hiyo ndio Siri kubwa until then na ukitaka kujua fuatilia kikazi chako cha mama au baba koo hutomaliza ..... kamwe meaning yaani baba yako alikuwa na baba yake na babu yako alikuwa na baba yake etc... fuata hivyo kama utamaliza
 
Nani yupo free tufanye majaribio ya swali la mtoa mada tujue ukifa inakuwaje unazaliwa au kwenda jumla baada ya majaribio tuje tutoe na ushahid
 
Imani yangu inanituma kwamba ukifa ndo mwisho wa kila kitu

Ukifa ndo mwisho wa dunia umefika kwako

Kama kuna anaebisha anyooshe mkono afanye kama anajikuna
 
Kuna maisha baada ya kufa, au tukifa ndiyo mwisho wa kila kitu?

Hili ni swali ambalo limekuwa likiwagawa watu kwa karne nyingi. Wapo wanaoamini kuwa kifo ni mwisho wa kila kitu, hakuna fahamu wala maisha mengine. Wengine wanaamini kuwa kifo ni mlango wa kuingia katika maisha mengine, ambako matendo ya duniani yanaendelea kuwa na maana.

Sasa hebu tufikiri.
Kama tukifa ndiyo mwisho wa kila kitu, je, kuna sababu ya kujinyima sana? Je, tuishi kwa kutumia na kufurahia mali zetu kadiri tuwezavyo kwa sababu baada ya kifo hakuna tena nafasi nyingine?

Lakini kama kweli kuna maisha baada ya kifo, je, si busara kuishi kwa tahadhari? Tuilinde miili yetu, tusiiharibu kwa makusudi, na tufe tukiwa na nguvu na afya kadiri inavyowezekana, kwa imani kwamba huenda kuna safari nyingine inayotuhitaji baada ya maisha haya.

Wewe unaamini nini? Je, kifo ni mwisho wa kila kitu, au ni mwanzo wa maisha mengine? Na kwa nini unaamini hivyo?
Kuna maisha baada ya kifo ambayo yanategemea maamuzi na matendo yetu tukiwa hai.

Naamini hivyo kwa sababu zifuatazo;
1. Aliyetupa uhai(mwanzo wetu) automatically ndiye mwenye Mamlaka juu ya hatma zetu(mwisho wetu)
2. Tumeumbiwa dhamiri ya kusense ubaya na wema hata kabla hatujatenda(hii kimsingi ni tahadhari kabla ya hatari)
3. The Law of cause and effect. Kila kinachopandwa kina mavuno yake!. Bila kujali nguvu alizo nazo mtu,kila afanyalo akiwa hai lina mavuno yake akiwa hai na akiwa mfu. Hata kama mtu huyo yupo juu ya sheria na Mamlaka za wanadamu. Hata kama hapa duniani yeye ni untouchable. Lazima yupo wa kumtouch akiwa nje ya dunia hii(baada ya kifo chake). Na huyo wa kumtouch lazima atakuwa ni mwenye nguvu kuu zaidi ya yeyote yule lakini pia lazima atakuwa ni Mtakatifu kweli kweli(asiye na hatia hata kidogo) hivyo automatically anakuwa na uhalali wa kumuhukumu kila mtu kwa HAKI bila ubaguzi wala upendeleo!
 
Hakuna cha wana wa Mungu Wala wa shetani sote ni wa Mungu ila issue ya kuchomwa moto huenda haipo. Hii dunia ina zaidi ya miaka bilioni kadhaa. Kwa mfano tuamue kutumia tu kalenda ya Sasa tuko mwaka 2026 sasa ukichukua mwaka WA kwanza mpaka mwaka 1790 hakuna hata binadamu mmoja anayeishi leo hii hata wa 1800 kamili waliopo hawafiki hata 200 dunia nzima. Unaniambiaje Kuna wakati tutachomwa moto wakati waliokufa mabilioni kwa mabilioni wametelekezwa tu hivohivo
Unadhani huo Moto upo makaburini?
 
Nani yupo free tufanye majaribio ya swali la mtoa mada tujue ukifa inakuwaje unazaliwa au kwenda jumla baada ya majaribio tuje tutoe na ushahid
Aliye free kwa ajili ya kuuana au kumuua?
 
Je, kifo ni mwisho wa kila kitu, au ni mwanzo wa maisha mengine? Na kwa nini unaamini hivyo?
Kukujibu, kifo sio mwisho wa kila kitu kutokana na facts zifuatazo.

Fact ya kwanza unapaswa kujua ni kwamba hapa Duniani ndio Jehanamu kwenyewe, Dunia ni jehanamu kutokana hakuna mwanadamu anayewezaridhika hata awe na hela au nguvu za kisiasa katika maisha haya.
hivyo hapa Duniani tupo baada ya kufa kutoka ulimwengu mwingine, Tukahukumiwa tukaja tukazaliwa hapa. Kwa nini wengi hawakumbuki past life! Ni kwa sababu kumbukumbu zinatunzwa kwenye ubongo na tukifa kinachotoka ni roho, mwili na ubongo unabaki kuoza.
Hata hivyo tukija kwenye nadharia za kImani ni wanadamu watatu tu ambao waliweza faulu na hawakuhumiwa kuzaliwa tena hapa duniani, ambao ni Enock, Eliya na Yesu. Hivyo, ingawa sisi tumezaliwa tukiwa na asili ya uovu, mwenyezi anatupa nafasi nyingine tena kuweza kuishi maisha ya kumpendeza ili atupeleke Paradiso, ila mpaka sasa humu Jf sijaona na sijasikia mtu ambaye ataweza ponyoka.
DUNIA ndio jehanamu tena ipo sustainable kwani wala Mwenyezi hana haja ya kuchochea moto wa adhabu mwenyewe bali sisi binadamu kwa binadamu tunapeana adhabu za kutosha, kusalitiana kimapenzi, kutapeliana, kula rushwa, kutamani na mambo mengi ya kuumiza kwa makusudi.
Kwanza ishi yetu tu ni unyama tosha tunakula nyama ya viumbe wengine ili kuishi, tunapora maziwa ya wanyama tunakunywa. Tunaharibu mazingira kwa kasi ya ajabu, watalamu wanakuambia huko porini wanyama walikuwa wanabalance automatic na mazingira ila mwanadamu ndo kiumbe pekee ambacho hakibalance na mazingira hakika mwisho wetu au watoto wetu watapata changamoto kubwa sana.

DUNIA ndio jehanamu. Hatukumbuki ya zamani kwa sababu ubongo wetu ulibaki. Tutaendelea kuzaliwa mpaka pale tutakapopatia kusudi la uwepo wetu hapa Duniani.
 
Kama kuku, mbuzi hawaendi mbinguni bas ata ww sku ukifa na habari yako imeishia apo

Ila huwa wanasema ni bora uamini ili ukikuta sio isiwe tatizo kuliko kuto kuamini zen ukakuta ni kwel utatesema zaidi

So amini vile una amini ww na sio kufuata au kuskiza maoni ya watu maana ata wao pia hawajui kama ww ambavyo ujui
 
Kuna maisha baada ya kufa, au tukifa ndiyo mwisho wa kila kitu?

Hili ni swali ambalo limekuwa likiwagawa watu kwa karne nyingi. Wapo wanaoamini kuwa kifo ni mwisho wa kila kitu, hakuna fahamu wala maisha mengine. Wengine wanaamini kuwa kifo ni mlango wa kuingia katika maisha mengine, ambako matendo ya duniani yanaendelea kuwa na maana.

Sasa hebu tufikiri.
Kama tukifa ndiyo mwisho wa kila kitu, je, kuna sababu ya kujinyima sana? Je, tuishi kwa kutumia na kufurahia mali zetu kadiri tuwezavyo kwa sababu baada ya kifo hakuna tena nafasi nyingine?

Lakini kama kweli kuna maisha baada ya kifo, je, si busara kuishi kwa tahadhari? Tuilinde miili yetu, tusiiharibu kwa makusudi, na tufe tukiwa na nguvu na afya kadiri inavyowezekana, kwa imani kwamba huenda kuna safari nyingine inayotuhitaji baada ya maisha haya.

Wewe unaamini nini? Je, kifo ni mwisho wa kila kitu, au ni mwanzo wa maisha mengine? Na kwa nini unaamini hivyo?
Ndiyo kuna maisha baada ya kifo lakini sio ktk mwili.Yesu alisema ktk yohana 11.25. "Yeye aniaminie ajapokufa atakuwa anaishi" maisha katika mwili hapa duniani ni ya kitambo:lakini ya kiroho ni ya milele kutegemea matendo ya mtu kumpeleka hukumuni au peponi
 
Kabla ya kujadili maisha baada ya kifo, tujiulize swali la msingi:
📍 Chanzo cha kifo ni nini?
Sio sababu ya mtu kufa kama ugonjwa, ajali au kujiua. Hayo ni sababu.
Chanzo ni nini kilichofanya kifo kiwepo kabisa?
 
Kifupi kwa maisha ya itakuwa imeisha baada ya kufa ,kabuli pia ni njia,njia pia huwa Ina mitihan yake.
Mbinguni kuna pepo na moto (sehemu zote ni kuishi milele)
 
Back
Top Bottom