Kuna Maisha Nyuma ya Hizi 'ID' Zetu, Tusiache Kupendana ❤️

Kuna Maisha Nyuma ya Hizi 'ID' Zetu, Tusiache Kupendana ❤️

mshana JF haina tofauti na maisha halisi tunayoishi mitaani, kukwazana na kupatana ni sehemu ya maisha hayo kutegemeana na mada iliyopo mezani.

Sasa isijetokea unamuomba mtu msahama leo kwa tofauti zenu zilizopita, kisha kesho mkakosana tena, binafsi nina wasiwasi kama naweza patana forever na Tlaatlaah na ndugu yake Lucas Mwashambwa.

Anyway muhimu tuishi tukijua haya ni mapito.
 
Amri iliyo kuu ni UPENDO! Basi tupendane..
Leo nimekaa nikitafakari kwa kina kuhusu jukwaa letu.

Mara nyingi tunakutana humu kuchangamsha akili, kubishana, na wakati mwingine kupeana changamoto za kimaisha.

Lakini ukweli ni kwamba, nyuma ya kila jina unaloliona humu (hata yale ya kufikirika), kuna binadamu halisi.

Kuna mtu anasoma posti yako huku yuko wodini anaumwa, mwingine ananuka madeni, mwingine kaachwa...

Mwingine kapoteza kazi, mwingine ana msongo mkubwa wa mawazo na JF ndio kimbilio lake pekee la kupoteza muda ili asijisikie mpweke.

Humu ndani wengi hatujuani kwa sura, lakini mioyo yetu inagusana kupitia maandishi yetu.

Huu uzi sio wa ligi wala malumbano. Ni uzi wa faraja. Kama kuna mwana-JF uandishi wake umewahi kukufariji siku ukiwa na upweke, mtag hapa umwambie "Asante". Kama uliwahi kumkwaza mtu kwa maneno makali humu ndani, omba msamaha hapa.

Maisha ni mafupi mno, na hatujui kesho yetu.

Tuigeuze JF kuwa sehemu salama (safe space) ya kupendana, kufarijiana, na kuinuana kiroho.

Mimi nawaombea heri na baraka ninyi nyote mnaosoma ujumbe huu. Mungu awabariki na kuwapa amani ya mioyo yenu. Nawapenda sana! 🙏🌹
Mimi napenda zile picha picha zako unazopost sijui Huwa unazitoa wapi nazipenda 😜
 
Back
Top Bottom