Kuna Maisha Nyuma ya Hizi 'ID' Zetu, Tusiache Kupendana ❤️

Kuna Maisha Nyuma ya Hizi 'ID' Zetu, Tusiache Kupendana ❤️

Ni kweli usemayo
IMG-20260809-WA0509.jpg
 
Amri iliyo kuu ni UPENDO! Basi tupendane..
Leo nimekaa nikitafakari kwa kina kuhusu jukwaa letu.

Mara nyingi tunakutana humu kuchangamsha akili, kubishana, na wakati mwingine kupeana changamoto za kimaisha.

Lakini ukweli ni kwamba, nyuma ya kila jina unaloliona humu (hata yale ya kufikirika), kuna binadamu halisi.

Kuna mtu anasoma posti yako huku yuko wodini anaumwa, mwingine ananuka madeni, mwingine kaachwa...

Mwingine kapoteza kazi, mwingine ana msongo mkubwa wa mawazo na JF ndio kimbilio lake pekee la kupoteza muda ili asijisikie mpweke.

Humu ndani wengi hatujuani kwa sura, lakini mioyo yetu inagusana kupitia maandishi yetu.

Huu uzi sio wa ligi wala malumbano. Ni uzi wa faraja. Kama kuna mwana-JF uandishi wake umewahi kukufariji siku ukiwa na upweke, mtag hapa umwambie "Asante". Kama uliwahi kumkwaza mtu kwa maneno makali humu ndani, omba msamaha hapa.

Maisha ni mafupi mno, na hatujui kesho yetu.

Tuigeuze JF kuwa sehemu salama (safe space) ya kupendana, kufarijiana, na kuinuana kiroho.

Mimi nawaombea heri na baraka ninyi nyote mnaosoma ujumbe huu. Mungu awabariki na kuwapa amani ya mioyo yenu. Nawapenda sana! 🙏🌹
Asante kwa kutukumbusha wajibu mwema .
Binafsi hakuna hata mmoja nimewahi kuchukizwa na andiko lake isipo kuwa upande wa siasa kuna watu sikupendezwa na maoni yao, sasa ili nisikwazike sana na wao ilibidi kwa mara ya kwanza ni wa ignore.
Vinginevyo kila mmoja kwa namna fulani amekuwa faraja, amekuwa tumaini, amekuwa furaha amekuwa mwalimu nk kwa mwingine nawe mleta mada ni mmoja wao.
 
Mkuu,

Hii ni kweli tuvumiliane huenda miaka 40 ijayo wengi wetu zitabaki ID tu humu na michango tuliyowahi itoa🥲.

MOLA wetu awafanyie wepesi kila mmoja wetu na changamoto apitiazo.

Nikumbuke min -me BICHWA KOMWE - DIVISHENI FOO adriz de mbusii Mbaga Jr

Wafuatao sasa wageni waalikwa🤣🤣

Tlaatlaah
@LucasMwashambwa

🙏🏻🙏🏻🙏🏻
🙌🏿🙌🏿🙌🏿.
 
Back
Top Bottom