Kuna mbegu nimenunua eti inasafisha tumbo na kuondoa sumu, bado sijaitumia nataka ushauri kwanza

Kuna mbegu nimenunua eti inasafisha tumbo na kuondoa sumu, bado sijaitumia nataka ushauri kwanza

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,623
Reaction score
8,442
Salaam wana JF

Kwa wale wasafiri wa kanda ya ziwa hasa kutokana Mwanza kwenda mikoa mingine mtakua mashahidi kwa hili.

Kuna watu wanapanda kwenye basi kuanzia pale Shinyanga na kushukia Tinde au Nzega, watu hawa wamekua wakiuza Dawa mbalimbali za asili(Tiba mbadala).

Sasa Jana wakati nasafiri aliingia jamaa mmoja Ustadhi kwenye basi letu na kuanza kutangaza kuhusu Dawa anazouza.

Kuna moja ilinivutia, ni mbegu fulani kwa jina nimesahau,vmuuzaji akadai mbegu hiyi unaitafuna na kushushia na maji baada ya muda utaanza kuhisi hali tofauti mdomoni na tumboni kutaanza kuunguruma hapo sasa utaenda chooni kuharisha na utashuhudia uchafu mwingi ukitoka.

Akaenda mbali zaidi na kusema ili uamini jitahidi uharishie kwenye beseni uone mavitu yatakayotoka tumboni.

Abiria wengi walinunua nami nikashawishika kuinunua hiyo mbegu.

Sasa bado sijaitumia naomba kama kuna ambaye aliwahi kutumia hii mbegu atiririke hapa uzoefu alioupata baada ya kuitumia.

Ni hayo tu wakuu.
 
Kuna Mzee moja mjita wa pande hizo alinipa dawa moja ya unga hatari sana!
 
Naijua ial jina nimesahau, ni kweli inasafisha kuhusu kuondoa sumu sijui ila unaharika sana na unaweza harisha vitu ambavyo hukumbuki kuvila mda uliopita, this means unaharisha deposits ya wastes kwenye colon kitu ambacho ni kizuri , naana kwenye wall ya bowel kwa sisi tunapenda mafuta mafuta sio yote hotoka na yakikaa kwa muda mrefu yazalisha sumu , ila angalizo sizijui side effects zake ila nimesha tumia zaidi ya mara mbili

Colon cleansing can help improve your body's overall health and wellness, and may even reduce your risks for colon cancer.
  • Makes the digestive system more effective.
  • Maintains regularity and prevents constipation.
  • Increases energy.
  • Increases the body's absorption of vitamins and nutrients.
  • Improves concentration.
 
Kama sijakosea inaitwa "halo ya punda" hiyo mbegu ukila utahara sanaaaa... Kwa kukushauri tu inabid siku hiyo ushinde nyumbani siku nzima..

Pia kunywa maji ya kutosha maana unaweza ukadondosha "puru" kama mdau alivyosema hapo juu...
 
Ushauri wangu binafsi

Hakikisha ukiinywa uwe huna ratiba nyingine zaidi ya kushinda kwako...
Mkuu inachukua muda gani kumaliza manake nataka kutumia mida hii. Kesho niingie kazini au nitumie weekend? Ushauri please
 
Hiyo itakuwa habbat mulk ujipange sawasawa kwa kazi ya kuhara ponda kimbegu pata unga weka hata kwenye uji au chai ukiweza tafuna kama si mvumilivu unaweza acha usia maana koki inafunguka haichukui robo saa utaenda chooni mpaka basi mpaka utatamani ukae hukohuko kama hauna choo private usitumie utakuwa kero na kama ni mfanyakazi usiende siku nzima na kila utakachokula kitatoka papohapo,tumia tupe mrejesho.
 
Mkuu inachukua muda gani kumaliza manake nataka kutumia mida hii. Kesho niingie kazini au nitumie weekend? Ushauri please
Vema ukatumia weekend

Kwa experience yangu na jamii ya dawa hizo ili nifanya nishinde home a whole day sijui ili nikataa.!?

Honestly sijawahi kuharisha kama that day
 
Back
Top Bottom