Kuna mbegu nimenunua eti inasafisha tumbo na kuondoa sumu, bado sijaitumia nataka ushauri kwanza

Kuna mbegu nimenunua eti inasafisha tumbo na kuondoa sumu, bado sijaitumia nataka ushauri kwanza

Mtaalam, ukinunua kimbegu.... bila kwenda kununua msuli na kigoda... dozi inakuwa haijakamilika...
Nenda kanunue msuli....ili ni vazi ambalo litakuwa la muhim sana siku ukitafuna hiko kimbegu, lakin pia utahitaji kigoda kwa ajil ya kukalia maeneo ya karibu na choo...
Kila la kheri mkuu.
 
Mkuu inachukua muda gani kumaliza manake nataka kutumia mida hii. Kesho niingie kazini au nitumie weekend? Ushauri please
Jitahidi usiharishe zaid ya Massa 6.
Ukinywa maji baridi na pia ukioga maji baridi inafunga yenyewe.
Hakika mwili hudhoofu kwa hiyo siku 1 tu
 
Kama shida yaku nikusafisha tumbo, kanunue Castor oil, haimizi tumbo, utaharisha vyakutosha kulingana na kiasi ulicho kunywa,

Vijiko viwili vikubwa vinakutosha, haya mafuta yanauzwa maduka ya dawa baridi na bei yake ni poa tu,
 
Niliwahi kutumia hii dawa. Halafu nilimeza vimbegu viwili jamani mwenzenu. Nilikaa chumbani kwangu naingia chooni kila baada ya sekunde kumi mwishowe nikavua nguo zote nikawa uchi muda wa kuvua hata kanga mwilini ulikuwa hautoshi unaweza shtukia vitu vimeshuka mapajani .

Tena niliambiwa niandae na yale madawa maalum ya watu wanaohara yanaitwa "oral" sijui nilikuwa na jug mbili zimejaa hayo maji. Yaani nikimaliza kunywa glass moja ni safari ya kukimbia chooni Baada ya masaa matatu nilihisi naaga dunia nguvu ziliisha na sauti ikagoma.

Nikitazama sink la chooni naharisha maji meupe kama kipindupindu hata hayana harufu. Nikajua hapo sasa namaliza stock ya maji ya mwilini nilitambaa hadi jikoni uchi kutafuta maji ya baridi kwenye fridge ndio pona yangu.

Ile kama utani tu unaweza kuondoka duniani kiulaini tu [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Niliwahi kutumia hii dawa. Halafu nilimeza vimbegu viwili jamani mwenzenu. Nilikaa chumbani kwangu naingia chooni kila baada ya sekunde kumi mwishowe nikavua nguo zote nikawa uchi muda wa kuvua hata kanga mwilini ulikuwa hautoshi unaweza shtukia vitu vimeshuka mapajani...
Ulipaswa kukaa na maji baridi karibu

Nilikunywa hii dawa kimbegu kimoja nikakaa 10 mnts hamna kitu nikaongeza cha pili jaman sitasahau kuanza kuhara tu naflash maji yameisha kwenye tank na umeme ulikatika sasa kuna choo ha public ila mpka ushuke ngazi uende gorofa ya chin aisee nilitaman kulia hyo siku nilihara nikitoka nakaa pemben ya choo nikanywa maji barid ila mpka vikate siku hata na nguv ya kupandisha ngazi
Ilikuwa miaka 3 iliyoisha mpka leo sithubut
 
ni moja ya dawa bora sana, na ukitaka ujue tumbo ni jalala Zaidi ya dampo, kunywa hii kitu, just be alone at home with a private toilet, hii dawa kiboko, the good thing is ukinywa maji ya baridi tu, inakata mda huohuo, lakin shughuli yake si mchezo
 
Niliwahi kutumia hii dawa. Halafu nilimeza vimbegu viwili jamani mwenzenu. Nilikaa chumbani kwangu naingia chooni kila baada ya sekunde kumi mwishowe nikavua nguo zote nikawa uchi muda wa kuvua hata kanga mwilini ulikuwa hautoshi unaweza shtukia vitu vimeshuka mapajani...
Mkuu nimejikuta nacheka tu tena Sana yaani ulivoandika nikawa navuta picha mbavu Sina eti unaeza vuta kilaini,daaah mkuu umeniongezea siku jioni hii nikiwa nasubiria mechi ya Simba na Al masry,hivo vimbegu ninavo viwili nilinunua mwezi uliopita ,naogopa ht kuvimeza , aisee ila nitameza tuu!
 
Ushauri wangu binafsi

Hakikisha ukiinywa uwe huna ratiba nyingine zaidi ya kushinda kwako

Uwe na maji ya kunywa zaidi ya Lita 3 pembeni ikiwezekana na glucose pia
Hakikisha unakuwa na tunda la Chungwa karibu yako, ili hali ya kuharisha ikizidi kiwango uweze kuistopisha. Utakapoona unaharisha maji baada ya uchafu kula chungwa.
 
Back
Top Bottom