Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kwanza hiyo taarifa tayari imekanushwa nimeona kwenye twitter tangu majuzi.Kwa ukubwa wa Serengeti kama 10% tu ya eneo lake litakuwa na madini either dhahabu au madini ya Vito kama safire n.k basi ni heri yachimbwe tu. Mapori yako mengi. Artificial safari ya Dubai haitaweza kushindana na Tanzania yenye hifafhi kama utitiri.
Hawa vijana wamejaa msisimkokwanza hiyo taarifa tayari imekanushwa nimeona kwenye twitter tangu majuzi.
Pili nashangaa watu wanaokomalia ati artificial park ya Dubai itashindana na mbuga zetu za wanyama. Nadhani ni ushamba tu na ulimbukeni wa mawazo. Mfano, nimewahi kufika Bronx Zoo Marekani ni kubwa sana na kila aina ya wanyama kutoka ecosystems tafauti duniani - africa, asia, south america na kadhalika, na bado wamarekani wanakuja hapa kutembelea mbuga za wanyama. Wanadhani artificial park ndiyo itakuwa sawa na natural ecosytem?
Hiyo migodi yote iliyosambaa nchi nzima imeleta pesa kiasi gani mpaka sasa?Nakwenda mbali zaidi ni kwamba kama 10% ya eneo la Serengeti litachimbwa madini basi itapatikana pesa nyingi sana itakayoweza kuendesha nchi bila kuyumba kwa miaka kadhaa, na kama asilimia zitazidi na pesa itaongezeka hivyo ustawi katika jamii utaongezeka.
Tuna hifadhi nyingi sana. Tuna mapori tengefu mengi , Dubai mwenye kieneo kidogo tena artificial hataweza kukompiti na Tanzania kwenye wild tourism labda tu kwasababu ya ujinga wa watu wachache watakaosomamia hizo hifadhi zetu
hivi kibusara tu hata kama wewe ni rais wa JMT unapataje ujasiri wa kuuza kila kitu upande ambao hujatokea(tanganyika)hata kama hao watanganyika ni wapole kama njiwa?!Na hiyo asilimia 10% ya Serengeti ni kakipande kadogo pembeni mwa Serengeti tutakapochimba, kwa hiyo hakuna tatizo? Ndani ya mbuga ya Serengeti, hata kama ni eneo la 2% ya mbuga, haifai kabisa kuchimba. Suala sio kuchimba tu, ni pamoja na logistics za kuendesha mradi wa uchimbaji kutia ndani wafanya kazi, nyumba za kuishi, magari, mitambo, uwanja wa ndege, umeme, maji, vumbi, sumu za ku process madini, nk! Kuna sababu za msingi kwa nini TANAPA walisema ni marufuku! Na kumbuka, Serengeti ya wanyama itaishi muda gani, na madini ndani ya Serengeti yatachimbwa kwa muda gani? Is it worth it kuharibu kitu cha kudumu kwa ajili ya kitu cha faida ya muda mfupi?
Waulize wachumi wakufanyie hesabu net present value ya Serengeti kama mbuga ya Wanyama, na Serengeti kama mradi wa madini!
Lakini swali la msingi, ni kwa kiwango gani Tanzania inafaidika na madini tuliyonayo ambayo inabidi yachimbwe na kampuni za kigeni? Dhahabu, almasi, Tanzanite, gesi nk, ni kwa kiasi gani vimetunyanyua sana kiasi kwamba leo tukivikuta ndani ya Ngorongoro ni afadhali tuharibu Ngorongoro ili kuvipata?
Waarabu wamewekeza sana Serengeti? Huko kuwekeza sana Serengeti ni katika nini, kujenga hoteli? Hivi kwa akili za Mtanzania, mtu anakuambia nataka kujenga hoteli ndani ya Serenegeti, na unamwona ni mwekezaji muhimu kawekeza sana?Unaouongea ni ujinga wa kujitungia.
Dubai safari park siyo safari park ya kwanza duniani. Zipo nyingi tu duniani. Watu wanawachana na zoo duniani ili wanyama wajifaraguwe.
Serengeti ipo na itaendelea kuwepo na hao EWaarabu wamewekez sana Serengeti.
Unafahamu kuwa moja ya hoteli za gharama kubwa duniani ipo Serengeti na Waarabu wana hisa zao humo?
Kweli kabisa. Ndio maana nilisema wazi humu JF, maamuzi makubwa kama haya yanayohusu bara, Samia ayaache hadi tutakapokuwa na raisi kutoka bara. Sio ayafanye akiwa anatoka Zanzibar, na waziri wa miundo mbinu ni wa Zanzibar, na waziri wa mambo ya nje ni wa Zanzibar sijui nk. Inakuwa kama maamuzi haya yanafanywa viongozi toka Zanzibar wakiwa wamejipanga ili yapite. Lengo lao ni nini?hivi kibusara tu hata kama wewe ni rais wa JMT unapataje ujasiri wa kuuza kila kitu upande ambao hujatokea(tanganyika)hata kama hao watanganyika ni wapole kama njiwa?!
Habari ipi imekanushwa, kuchimba madini Serengeti na mbuga nyingine? Maana kuna video clip zimo humu JF Samia akiongea hilo.kwanza hiyo taarifa tayari imekanushwa nimeona kwenye twitter tangu majuzi.
Pili nashangaa watu wanaokomalia ati artificial park ya Dubai itashindana na mbuga zetu za wanyama. Nadhani ni ushamba tu na ulimbukeni wa mawazo. Mfano, nimewahi kufika Bronx Zoo Marekani ni kubwa sana na kila aina ya wanyama kutoka ecosystems tafauti duniani - africa, asia, south america na kadhalika, na bado wamarekani wanakuja hapa kutembelea mbuga za wanyama. Wanadhani artificial park ndiyo itakuwa sawa na natural ecosytem?
Kumbe umelala usimgizi wa pono, si ya leo wala jana hayo.Waarabu wamewekeza sana Serengeti? Huko kuwekeza sana Serengeti ni katika nini, kujenga hoteli? Hivi kwa akili za Mtanzania, mtu anakuambia nataka kujenga hoteli ndani ya Serenegeti, na unamwona ni mwekezaji muhimu kawekeza sana?
Sasa kwa taarifa yako, jiulize, nani kamwambia Samia ndani ya Serengeti kuna madini, wakati TANAPA wanakataza katakata aina yeyote ya exploration ndani ya mbuga? Huyo mtu aliemwambia Samia kuna madini huko alipataje kibali cha kwenda kufanya exploration ndani ya Serengeti na mbuga nyingine? Unamkaribisha mwarabu, anakuambia nakuja kuwekeza ndani ya mbuga, kumbe ana lengo jingine na you are too myopic kuona hilo, unafurahia zawadi zake za vidani nk. Huko kuwekeza sana unakokuona amefanya mwarabu ndani ya Serengeti, kwake ni gharama ndogo sana ili kupata access ndani ya Serengeti na mbuga njingine kwa malengo makubwa zaidi - it is a small operational cost. Hoteli waliyojenga Serengeti wanaweza kukupa zawadi wakisha realize long term objectives zao.
Watanzania, kwa nini mnakuwa vipofu kiasi hiki, mnakuwa so easily duped? Bado mpaka leo mnauza utu na rasilimali zenu kwa zawadi za shanga za mwarabu, anazowaambia mnavutia mkivaa kiunoni?
Kwani kuchimba madini kwa mbuga nyingine kumeanza leo, mbona Selous imeanza zaidi ya miaka 10 nyuma mchakato wa kuchimba Uranium na mpaka EIA walishafanya tayari, au huna taarifa hiyo?Habari ipi imekanushwa, kuchimba madini Serengeti na mbuga nyingine? Maana kuna video clip zimo humu JF Samia akiongea hilo.
Pia kuna swali limeulizwa hapa, kwamba kwa sababu Dubai Safari Park ni ndogo kwa sasa, kuna mtume aliwakataza kuipanua hapo baadae? Umefika Dubai safari Park? Kwa akili yako ili Dubai Safari Park iwe tishio lazima iwe kubwa kama Serengeti?
Halafu watu wenye point za kijinga kama wewe wanajibiwa kwa takwimu;
Dubai Safari Park
The park hopes to become to become part of the top 5 best safari parks in the world within a span of 5 years and attract 10,000 visitors per day. The parking lot will allow for 3,600 cars.
Kwa hiyo wakati Serengeti ikiwa na wastani wa visitors 500 kwa siku, Dubai Safari Park ina lenga visitors 10,000 kwa siku, halafu unaongelea puani kuwa Safari Park haiwezi kushindana na Serengeti! Hadi sasa Dubai Safari Park inatengeneza hela kubwa sana zaidi ya Serengeti
Lengo lako lilikua kujidadavua umefika Marekani, sivyo? Obviously mshamba hapa ni wewe.
God have mercy...Jana Stroke kanistua kuhusu hili jambo nilishangaa sana yaani tumefikia kutaka kugawa kila kitu kwa wahuni ambao hatupati kitu hivyo vitu vingine walivyogawa tunafaidika nini wakati huduma za jamii kupata bado mtihani kila kitu unanunua kina 18% VAT mpaka nguo za watoto chini ya miaka 4 wanazipiga kodi harafu madini,bandari,gesi na sasa Mbuga wanataka kuwapa wahuni tena..
Serengeti yote chini kuna madini nani kakwambia ni 10% tuKwa ukubwa wa Serengeti kama 10% tu ya eneo lake litakuwa na madini either dhahabu au madini ya Vito kama safire n.k basi ni heri yachimbwe tu. Mapori yako mengi. Artificial safari ya Dubai haitaweza kushindana na Tanzania yenye hifafhi kama utitiri.
Nadhani hivi karibuni kila Mtanzania na ulimwengu mzima kwa ujumla, wameshangazwa na kufadhaishwa na kauli ya Raisi Samia kutoa agizo kwamba madini yaliyoko Serengeti yachimbwe, kwa sababu simba na tembo hawali madini.
Tangazo la raisi Samia
View attachment 3048586
Sasa labda watu wengi wasichoelewa ni kwamba, kwa miaka kadhaa, UAE wamefanya jitihada kubwa ya kutengeneza mazingira ya "Serengeti" huko Dubai, kwa lengo la kukuza utalii wa wanyama pori huko Dubai. Na kila mtu anajua kwamba wengi wa wanyama waliopelekwa Dubai Safari Park wametoka Tanzania, na bado hadi leo wanapelekwa. Hii ni kutia ndani na tembo, simba, viboko, vifaru, nyoka, vinyonga, fisi, ndege, swala, duma, nyani, twiga, kenge, mamba, sokwe, chui, nk. Dubai walichofanya ni kutengeneza kwa gharama kubwa mazingira kama ya Serengeti huko Dubai, kutia ndani na mito, misitu, miamba nk, na kuingiza wanyama kwenye mbuga hii "artificial savanna".
Baadhi ya picha katika Dubai Safari Park ni hizi
View attachment 3048584
Lengo la UAE ni kuteka biashara ya utalii wa wanyama pori, hasa kutoka Afrika, ambayo ndio mshindani mkubwa wa Dubai Safari Park. Hivyo, kwa namna moja au nyingine, Serengeti ikifa, basi Dubai Safari Park itakuwa mdadala mkubwa wa Serengeti.
Athari ya kuchimba madini ndani ya Serengeti ni kuiua Serengeti, na siyo Serengeti tu, bali pia Masai Mara ya Kenya, kwa sababu Masai Mara ni sehemu ya Serengeti. Hivyo hili ni jambo ambalo litaathiri sana utalii wa wanyama pori Tanzania na Kenya, na atakaefaidika ni UAE na Dubai. Kwa hiyo basi, ni jukumu la Watanzania na ndugu zetu Wakenya kuungana na kukosoa na kupinga kwa nguvu zote uamuzi huu wa raisi Samia, kwamba hauna manufaa ya muda mrefu ya nchi zetu, bali manufaa ya muda mrefu ya Dubai. Madini yeyote katika Serengeti yakichimbwa, sana sana yatadumu kwa mika 20-30, na yatakapoisha hakutakuwa tena na Serengeti wala Masai Mara.
Kumbuka, mazingira ya utalii katika Dubai Safari Park ni ya kisasa sana, luxury, lakini bado hawajaweza kutoa ushindani mkubwa kwa Serengeti na Masai Mara. Sasa je, kuna mbinu za makusudi za kuziua Serengeti na Masai mara ili kusiwe na ushindani mkubwa kwa Dubai Safari Park?
Sasa ndio maana tunajiuliza, hili wazo la kuchimba madini katika mbuga ya Serengeti, ambalo kwa muda mrefu TANAPA wamelipinga kwa nguvu zote, ni la raisi Samia mwenyewe, au ushauri kutoka Dubai? Na mnafikiri nani atapewa mikataba ya kuchimba madini ndani ya Serengeti, kampuni toka Dubai? Je atachimba madini hayo kwa lengo la kutoathiri wanyama wa Serengeti?
Jambo hili kwa sasa linahusishwa pia na mabadiliko ya baraza la mawaziri la hivi karibuni, hususa kumuondoa Jerry Slaa katika wizara ya ardhi ambako ameonekana kama kero kwa baadhi ya watu kutia ndani "wawekezaji" toka nchi fulani fulani ambazo sitaki kuzitaja. Pia limemgusa Makamba wizara ya mambo ya nje. Je, wamekuwa kikwazo katika mipango kama hii ambayo inahusishwa na kuiua Serengeti na Masai Mara kwa manufaa ya Dubai?
Tukumbuke documentary ya TANAPA - Serengeti Shall Never Die, chini ya raisi yeyote wa Tanzania.
Kwa wale msioijua Dubai Safari Park bofya hapa
View: https://www.youtube.com/watch?v=us8Sl-w9n20
Nani amezuia? Sina habari.Nafurahi sana walivyozuiwa, kitendo cha kuanza kuchimba madini hifadhi ni dalili ya kutawanya wanyama, ambao milipuko itakuwa kero kwa wanyama. Lakini pia kutakuwa na ongezeko la ujangiri ndani ya hifadhi kiasi kwamba usalama wa wanyama utakuwa hatari maana sura zitakuwa nyingi ndani ya hifadhi.
Niombe, tu watanganyika tuendelee tu kuomba juu ya nchi yetu, sisi ndio inayotuhusu,. Nina uchungu sana na nchi yangu kwa kweli
Nadhani hivi karibuni kila Mtanzania na ulimwengu mzima kwa ujumla, wameshangazwa na kufadhaishwa na kauli ya Raisi Samia kutoa agizo kwamba madini yaliyoko Serengeti yachimbwe, kwa sababu simba na tembo hawali madini.
Tangazo la raisi Samia
View attachment 3048586
Sasa labda watu wengi wasichoelewa ni kwamba, kwa miaka kadhaa, UAE wamefanya jitihada kubwa ya kutengeneza mazingira ya "Serengeti" huko Dubai, kwa lengo la kukuza utalii wa wanyama pori huko Dubai. Na kila mtu anajua kwamba wengi wa wanyama waliopelekwa Dubai Safari Park wametoka Tanzania, na bado hadi leo wanapelekwa. Hii ni kutia ndani na tembo, simba, viboko, vifaru, nyoka, vinyonga, fisi, ndege, swala, duma, nyani, twiga, kenge, mamba, sokwe, chui, nk. Dubai walichofanya ni kutengeneza kwa gharama kubwa mazingira kama ya Serengeti huko Dubai, kutia ndani na mito, misitu, miamba nk, na kuingiza wanyama kwenye mbuga hii "artificial savanna".
Baadhi ya picha katika Dubai Safari Park ni hizi
View attachment 3048584
Lengo la UAE ni kuteka biashara ya utalii wa wanyama pori, hasa kutoka Afrika, ambayo ndio mshindani mkubwa wa Dubai Safari Park. Hivyo, kwa namna moja au nyingine, Serengeti ikifa, basi Dubai Safari Park itakuwa mdadala mkubwa wa Serengeti.
Athari ya kuchimba madini ndani ya Serengeti ni kuiua Serengeti, na siyo Serengeti tu, bali pia Masai Mara ya Kenya, kwa sababu Masai Mara ni sehemu ya Serengeti. Hivyo hili ni jambo ambalo litaathiri sana utalii wa wanyama pori Tanzania na Kenya, na atakaefaidika ni UAE na Dubai. Kwa hiyo basi, ni jukumu la Watanzania na ndugu zetu Wakenya kuungana na kukosoa na kupinga kwa nguvu zote uamuzi huu wa raisi Samia, kwamba hauna manufaa ya muda mrefu ya nchi zetu, bali manufaa ya muda mrefu ya Dubai. Madini yeyote katika Serengeti yakichimbwa, sana sana yatadumu kwa mika 20-30, na yatakapoisha hakutakuwa tena na Serengeti wala Masai Mara.
Kumbuka, mazingira ya utalii katika Dubai Safari Park ni ya kisasa sana, luxury, lakini bado hawajaweza kutoa ushindani mkubwa kwa Serengeti na Masai Mara. Sasa je, kuna mbinu za makusudi za kuziua Serengeti na Masai mara ili kusiwe na ushindani mkubwa kwa Dubai Safari Park?
Sasa ndio maana tunajiuliza, hili wazo la kuchimba madini katika mbuga ya Serengeti, ambalo kwa muda mrefu TANAPA wamelipinga kwa nguvu zote, ni la raisi Samia mwenyewe, au ushauri kutoka Dubai? Na mnafikiri nani atapewa mikataba ya kuchimba madini ndani ya Serengeti, kampuni toka Dubai? Je atachimba madini hayo kwa lengo la kutoathiri wanyama wa Serengeti?
Jambo hili kwa sasa linahusishwa pia na mabadiliko ya baraza la mawaziri la hivi karibuni, hususa kumuondoa Jerry Slaa katika wizara ya ardhi ambako ameonekana kama kero kwa baadhi ya watu kutia ndani "wawekezaji" toka nchi fulani fulani ambazo sitaki kuzitaja. Pia limemgusa Makamba wizara ya mambo ya nje. Je, wamekuwa kikwazo katika mipango kama hii ambayo inahusishwa na kuiua Serengeti na Masai Mara kwa manufaa ya Dubai?
Tukumbuke documentary ya TANAPA - Serengeti Shall Never Die, chini ya raisi yeyote wa Tanzania.
Kwa wale msioijua Dubai Safari Park bofya hapa
View: https://www.youtube.com/watch?v=us8Sl-w9n20izo ni ndoto za kuota mchana kabisa.