Kuna mbinu za makusudi za kuiua Serengeti ya Tanzania na Masai Mara ya Kenya ili kukuza Dubai Safari Park kwa ajili ya utalii wa wanyama wa porini?

Awamu ya Chura Kiziwi kweli mambo πŸ”₯πŸ”₯ safari hii kila kitu kitauzwa au huenda hata sisi tumeuzwa
 
mimi naona sawa wauze wasiuze watajjua wenye,acha nidnae unga wangu na dagaa nile mchana
bila kusahau MB 240 za jero nirudi jf kujiliwaza
 
Kwa ukubwa wa Serengeti kama 10% tu ya eneo lake litakuwa na madini either dhahabu au madini ya Vito kama safire n.k basi ni heri yachimbwe tu. Mapori yako mengi. Artificial safari ya Dubai haitaweza kushindana na Tanzania yenye hifafhi kama utitiri.
kwanza hiyo taarifa tayari imekanushwa nimeona kwenye twitter tangu majuzi.

Pili nashangaa watu wanaokomalia ati artificial park ya Dubai itashindana na mbuga zetu za wanyama. Nadhani ni ushamba tu na ulimbukeni wa mawazo. Mfano, nimewahi kufika Bronx Zoo Marekani ni kubwa sana na kila aina ya wanyama kutoka ecosystems tafauti duniani - africa, asia, south america na kadhalika, na bado wamarekani wanakuja hapa kutembelea mbuga za wanyama. Wanadhani artificial park ndiyo itakuwa sawa na natural ecosytem?
 
Hawa vijana wamejaa msisimko
 
Hiyo migodi yote iliyosambaa nchi nzima imeleta pesa kiasi gani mpaka sasa?
 
hivi kibusara tu hata kama wewe ni rais wa JMT unapataje ujasiri wa kuuza kila kitu upande ambao hujatokea(tanganyika)hata kama hao watanganyika ni wapole kama njiwa?!
 
Waarabu wamewekeza sana Serengeti? Huko kuwekeza sana Serengeti ni katika nini, kujenga hoteli? Hivi kwa akili za Mtanzania, mtu anakuambia nataka kujenga hoteli ndani ya Serenegeti, na unamwona ni mwekezaji muhimu kawekeza sana?

Sasa kwa taarifa yako, jiulize, nani kamwambia Samia ndani ya Serengeti kuna madini, wakati TANAPA wanakataza katakata aina yeyote ya exploration ndani ya mbuga? Huyo mtu aliemwambia Samia kuna madini huko alipataje kibali cha kwenda kufanya exploration ndani ya Serengeti na mbuga nyingine? Unamkaribisha mwarabu, anakuambia nakuja kuwekeza ndani ya mbuga, kumbe ana lengo jingine na you are too myopic kuona hilo, unafurahia zawadi zake za vidani nk. Huko kuwekeza sana unakokuona amefanya mwarabu ndani ya Serengeti, kwake ni gharama ndogo sana ili kupata access ndani ya Serengeti na mbuga njingine kwa malengo makubwa zaidi - it is a small operational cost. Hoteli waliyojenga Serengeti wanaweza kukupa zawadi wakisha realize long term objectives zao.

Watanzania, kwa nini mnakuwa vipofu kiasi hiki, mnakuwa so easily duped? Bado mpaka leo mnauza utu na rasilimali zenu kwa zawadi za shanga za mwarabu, anazowaambia mnavutia mkivaa kiunoni?
 
hivi kibusara tu hata kama wewe ni rais wa JMT unapataje ujasiri wa kuuza kila kitu upande ambao hujatokea(tanganyika)hata kama hao watanganyika ni wapole kama njiwa?!
Kweli kabisa. Ndio maana nilisema wazi humu JF, maamuzi makubwa kama haya yanayohusu bara, Samia ayaache hadi tutakapokuwa na raisi kutoka bara. Sio ayafanye akiwa anatoka Zanzibar, na waziri wa miundo mbinu ni wa Zanzibar, na waziri wa mambo ya nje ni wa Zanzibar sijui nk. Inakuwa kama maamuzi haya yanafanywa viongozi toka Zanzibar wakiwa wamejipanga ili yapite. Lengo lao ni nini?

Kama kuna madini ndani ya mbuga za bara, acha tukiwa na raisi wetu wa bara tufanye huo uamuzi wa kuchimba au kutochimba, kwa sababu kuna uwezekano muungano ukaja kavunjika na masuala ya bara hayatakuwa yanawahusu watu wa Zanzibar tena. Kwa hiyo Samia hapaswi kutu -lock in kwenye maamuzi ya bara ambayo baadaye yanaweza yakawa hayamuathiri yeye kama Mzanzibar. Sisi ndio tutabaki na athari za maamuzi yake, kutia ndani na bandari.
 
Habari ipi imekanushwa, kuchimba madini Serengeti na mbuga nyingine? Maana kuna video clip zimo humu JF Samia akiongea hilo.

Pia kuna swali limeulizwa hapa, kwamba kwa sababu Dubai Safari Park ni ndogo kwa sasa, kuna mtume aliwakataza kuipanua hapo baadae? Umefika Dubai safari Park? Kwa akili yako ili Dubai Safari Park iwe tishio lazima iwe kubwa kama Serengeti?

Halafu watu wenye point za kijinga kama wewe wanajibiwa kwa takwimu;



Dubai Safari Park
The park hopes to become to become part of the top 5 best safari parks in the world within a span of 5 years and attract 10,000 visitors per day. The parking lot will allow for 3,600 cars.

Kwa hiyo wakati Serengeti ikiwa na wastani wa visitors 500 kwa siku, Dubai Safari Park ina lenga visitors 10,000 kwa siku, halafu unaongelea puani kuwa Safari Park haiwezi kushindana na Serengeti! Hadi sasa Dubai Safari Park inatengeneza hela kubwa sana zaidi ya Serengeti

Lengo lako lilikua kujidadavua umefika Marekani, sivyo? Obviously mshamba hapa ni wewe.
 
Kumbe umelala usimgizi wa pono, si ya leo wala jana hayo.
 
Nchi tajiri tumepewa tukanyimwa akili acha wenye akili watutomb.
 
Kwani kuchimba madini kwa mbuga nyingine kumeanza leo, mbona Selous imeanza zaidi ya miaka 10 nyuma mchakato wa kuchimba Uranium na mpaka EIA walishafanya tayari, au huna taarifa hiyo?

Na hiyo kuwa safari park inazalisha fedha nyingi zaidi la ajabu ni lipi? Si tumelala wenyewe hatutangazi vivutio vyetu hapa nchini, kila jambo ni siasa? Unashangaa nini wakati hapo Kenya tu wametupita kwa mbali na hiyo mbuga yao ya Masai Mara wakati sehemu kubwa ya Serengeti ecosystem iko kwetu. Hata mlima Kilimanjaro walitangaza kuwa uko kwao na sisi tulikuwa tunachekelea tu mpaka hivi karibuni ndiyo tumeanza kujitutumua.

Mjinga ni wewe hapo unayepiga kelele bila kufanya analysis, mimi nimefika nchi nyingi sana siyo marekani tu wacha ushamba ukadhani watu wote ni kama wewe.

Endelea na kushindana Simba na Yanga na mechi sijui European Super League labda Mwenyezi Mungu siku moja atakukumbuka akuondoe kwenye giza la ushamba.
 
God have mercy...
 
Kwa ukubwa wa Serengeti kama 10% tu ya eneo lake litakuwa na madini either dhahabu au madini ya Vito kama safire n.k basi ni heri yachimbwe tu. Mapori yako mengi. Artificial safari ya Dubai haitaweza kushindana na Tanzania yenye hifafhi kama utitiri.
Serengeti yote chini kuna madini nani kakwambia ni 10% tu
 
Wanataka Madini wanataka Wanyamapori lakini hawawataki WAMASAI.
 
Nafurahi sana walivyozuiwa, kitendo cha kuanza kuchimba madini hifadhi ni dalili ya kutawanya wanyama, ambao milipuko itakuwa kero kwa wanyama. Lakini pia kutakuwa na ongezeko la ujangiri ndani ya hifadhi kiasi kwamba usalama wa wanyama utakuwa hatari maana sura zitakuwa nyingi ndani ya hifadhi.

Kitu kingine JK Nyerere aliweka makusudi yaan kuextend eneo la serengeti akijua wazi kuna madini huko ambako ni rasilimali za wanzania na si hao Waarabu. Teknologia inakuwa mwisho wa siku watoto wetu watakosa chochote na ujuzi wanao ni bora wangechimba hao watoto wetu kwa baadae kwa manufaa ya nchi yetu.

Huyo mama yenu hana uchungu na hii Tanzania, kwanza akimaliza kutawala anaenda kuishi huko Dudai na kutuacha watanzania masikini wa kutupwa plus mikodi anayokopa.

Binafsi hata simkubali ila ndio hivyo tuuu. Tutajikuta masikini wa kutupa.

Watawala wote wa Kiislam waliopita hapa Tanganyika walikuwa wanatupitisha kwenye kipindi kigumu sanaa, sijawahi kubali kuvushwa na huu utawala.

Niombe, tu watanganyika tuendelee tu kuomba juu ya nchi yetu, sisi ndio inayotuhusu,. Nina uchungu sana na nchi yangu kwa kweli
 
Nani amezuia? Sina habari.
 
Izo ni ndoto za kuota mchana, badala ya kuota usiku...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…