Kujitolea ni dhana pana.Ninaimani maana yake itajumuisha watu wote walio kwenye hali ya kujitolea bila kujali ni private au public kulingana na maslahi wanayoyapata watu pale walip😵pen Schools ni moja kati ya taasisi zinazojitolea moja kwa moja kwa kuisaidia serikali kuwarudisha kundini kondoo waliopotea.Wanaohudumu huko huwa ni watu wasiokuwa na mishahara isipokuwa posho zinazotegemea idadi ya wapokea huduma.Open Schools zinazomilikiwa na wadau binafsi ndizo zinazoongoza kutoa fursa ya kujitolea kwa vijana wengi wanaohitimu fani za ualimu kuliko hata shule za umma.
Rai yangu kwa Mh.Rais na Waziri (OR-TAMISEMI) hiki kigezo kama watakitumia ni muhimu kikawa na ukamilifu ndani yake ili kuondoa dhulma.
Ni muhimu servers za tamisemi zikawa updated ili kuingiza open schools zote vinginevyo kigezo hiki ni batili na hakina lengo lenye lengo.
Pia,maafisa elimu ngazi ya kata washirikishwe moja kwa moja na maafisa elimu wilaya ili kukusanya taarifa za wanaojitolea moja kwa moja kutoka kwenye shule za umma na open schools zote zilozo kwenye maeneo yao kwa kuwaona kwa macho wahusika wakitekeleza majukumu yao siyo hii ya ku-upload barua,ni ubatili na kujilisha upepo.