Kuna mchawi kakamatwa kunakofanyika Bunge la Katiba akiwa

Kuna mchawi kakamatwa kunakofanyika Bunge la Katiba akiwa

Uchawi' bungeni wafika Usalama wa Taifa, Polisi
Stella Nyemenohi, Dodoma
Daily News; Sunday,June 15, 2008 @00:01

Ofisi ya Spika imewasilisha taarifa kwa Polisi na Usalama wa Taifa ili washughulikie madai yaliyojitokeza hivi karibuni kuhusu Mbunge na Ofisa mmoja Mwandamizi wa Bunge kukutwa ndani ya Ukumbi wa Bunge wakifanya vitu vinavyodhaniwa kuwa ni ushirikina.

Tukio hilo lililoripotiwa jana na baadhi ya vyombo vya habari, linadaiwa kufanyika Jumatatu wiki iliyopita likimhusisha Mbunge na Ofisa wa Bunge, ambao hata hivyo, hawakutajwa ni akina nani.

Imedaiwa kuwa watu hao walinaswa wakinyunyizia vitu visivyojulikana katika kila kiti cha Mbunge na kuishia cha Spika. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuahirishwa semina ya

Wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi mjini hapa, Spika Samuel Sitta alisema Kamanda wa Polisi mkoani hapa na Usalama wameanza kufuatilia zaidi tangu juzi ili kubaini ukweli wa suala hilo .

Ingawa alisema bado suala hilo ni uvumi na kwamba halina budi kusubiri kukamilika uchunguzi wa vyombo hivyo vya usalama , Sitta alisema hata hivyo tahadhari zote zinachukuliwa katika Ukumbi wa Bunge.

Hata hivyo, alisema kwa upande mwingine, tahadhari zinaweza kuwa ngumu ikizingatiwa kuwa wanaohusishwa ni watu ambao hawana kipingamizi cha kuingia katika ukumbi huo.

Akizungumzia juu ya tukio hilo , Spika alisema, "Inashangaza. Lakini ni suala la uvumi, linachunguzwa. Tusubiri RPC na Usalama wa Taifa wakamilishe uchunguzi wao…tahadhari zote zinachukuliwa," alisema.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoandikwa na baadhi ya magazeti, tukio hilo la ushirikina, linadaiwa kufanyika siku moja kabla ya kikao cha kwanza cha Mkutano wa 12 wa Bunge kuanza Jumanne iliyopita.

Spika alisema wakati wa tukio hilo, kamera sita zilizokuwa katika ukumbi huo, hazikuwa zimewashwa. Isipokuwa inadaiwa, kamera moja ya studio ndiyo iliyoonyesha watu hao.

Hata hivyo, Sitta alisema kamera hiyo ilionyesha picha iliyofifia ambayo ni vigumu kubaini wahusika. Hata hivyo, alisema anaamini kuwa ikifikishwa kwa wataalamu, ndiyo watakaoweza kubaini wahusika.

Alipoulizwa na waandishi kuhusu mantiki ya kuhusisha tukio hilo la ushirikina na ugonjwa wa ghafla wa Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), Spika alisema halihusishwi ikizingatiwa kuwa taarifa za daktari, zilionyesha kuwa alikuwa na uchovu.

Kwa mujibu wa Spika, Dk. Mwakyembe alianza kujisikia anaishiwa nguvu Alhamisi dakika chache wakati akijaribu kuwasiliana na Spika ndani ya Bunge. Alitoka nje ya ukumbi kwa msaada wa Mbunge mwenzake na kupelekwa hospitalini.

Baada ya Mwakyembe kukabiliwa na maradhi hayo ya ghafla, kesho yake (juzi) ulienea uvumi kuwa amefariki. Wakati Sitta alisisitiza jana kuwa afya yake inaendelea vizuri, HabariLeo ilimshuhudia Mbunge huyo jana akiwa katika viwanja vya Bunge katika hali ya kawaida.

Wakati huohuo, semina ya NEC-CCM ilianza jana na inatarajiwa kumalizika leo mjini Dodoma. Kwa mujibu wa Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM John Chiligati alisema miongoni mwa waliotoa mada ni pamoja na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Beno Ndullu.

"Hatujamaliza semina. Inaendelea hadi kesho (leo). Kwa hiyo, maazimio yote yatakayofikiwa, tutatoa taarifa kesho saa 11," Chiligati aliwaambia waandishi na kusisitiza kuwa lengo la semina hiyo ni kuhusu masuala ya uchumi, hususan kilimo.
Huo ni mkusanyiko wa watu. Chance ya kuwapo wachawi ni kubwa tu
 
Kuna habari imenifikia mida hii kuwa kuna mtu anaesadikiwa akiwanga kwenye eneo kunapofanyika mkutano wa bunge lakatiba ,mwenyewe anadai ameanguka akitokea Zaire Congo akielekea Msumbiji ,amedai kuwa katika eneo hilo kuna mzunguko mkubwa wa nguvu za giza ,nguvu hizo ndio zilizosababisha kuingia kwenye mkondo na kumvuta hadi kuangukia hapo.

Baadhi ya mashuhuda wamedai sio kweli kama alikuwa akikatiza anga ya Tanzania kuelekea Mozambiki kwani ameonekana na vikoba akiwa na nakala ya rasimu ya katiba waliokuja nayo jamaa wa ccm ,iliyozua tafrani kiasi ya kuwafadhaisha CCM wenyewe ,hivyo amekuja kuwekeza vitu ili kuwazidii wale wanaoipinga rasimu ya katiba hiyo ya ccm yenye muelekeo mwengine ambaoni tofauti kabisa na ile rasimu ya Warioba iliyotokana na wananchi walio wengi.

Mwanga huyo ameshikiliwa na kusaidiwa kupewa nguo za kujisetiri.
Haya mashetani ya CCM bado yanaendelea! mtakumbuka Chengi alipatikana kwenye kamera za bunge akiwanga wakati wa bunge la Samwel Sitta? Hayo ndiyo mashatani yanayotuwangia ili tuwe mazezeta!! tuikubali rasimu yao ya majimarefu prof. Wako wapi wanashinyanga tuyakate mapanga kama wale vikongwe wa Magu wasio na hatia!!!
 
mambo ya kupika haya ku-divert attention to serious matters

mara posho, mara kura za siri, mara wizi wa simu, mara uchawi... typical politics of a small circus ya "the so called wenye nchi"

hapa ni chezo ili serious matters zipite kama tulivyozoea... i think it is high time someone get shot in the a$$ twice and it will stop forever
 
Serikali legelege kama hii tuliyonayo ndiyo faida yake hiyo bado tutaona na kusikia mengi muda si mrefu!
 
Sina uhakika kama kuna nchi nyingine duniani usalama wa taifa wanatumia ndumba pia. Kwa Tz nadhani zimeshatokea cases 2 au 3 za usalama wa taifa kuhusishwa na ndumba kwenye kutenda kazi zao...
 
Nakumbuka Chenge alivyobambwa Bungeni 'akiwanga' hahahaaaaaaaaaaaaaaaa! CCM na ushirikina ni DAMUDAMU!
 
[video=facebook;10151920403460060]https://www.facebook.com/photo.php?v=10151920403460060[/video]
 
Mh ina maana Kingunge alifanikiwa kuingia ndani ya Bunge ila mwenzie ndio akanaswa?
 
Sikieni nyie maccm,harogwi mtu hapa katiba mpya ya watanzania ni lazima mnataka au hamtaki ktk Jiiina la Yesu'
 
Kama huamini uchawi pale bungeni ndio hatari ,tena ,yaani wewe ulikuwa wapi ,kuna mtu alikamatwa anamwagilia unga viti vya bungeni ,mbona ilikuwa habari kuu magezetini ,!

Andrew Chenge huyo.
 
Haya mashetani ya CCM bado yanaendelea! mtakumbuka Chengi alipatikana kwenye kamera za bunge akiwanga wakati wa bunge la Samwel Sitta? Hayo ndiyo mashatani yanayotuwangia ili tuwe mazezeta!! tuikubali rasimu yao ya majimarefu prof. Wako wapi wanashinyanga tuyakate mapanga kama wale vikongwe wa Magu wasio na hatia!!!

Alinyunyizia unga hata kwenye kiti cha Harison Mwakyembe. Eti huyo Chenge awe Mwenyekiti wa bunge la katiba? Labda awe katibu wa kingunge.
 
Hakuna cha ajabu.

Chama cha waganga wa tiba asili ni moja ya kundi la watu 201 walioteuliwa.

Wapo kazini, wanaonyesha ushiriki wao kwa vitendo.
 
Kuna habari imenifikia mida hii kuwa kuna mtu anaesadikiwa akiwanga kwenye eneo kunapofanyika mkutano wa bunge lakatiba ,mwenyewe anadai ameanguka akitokea Zaire Congo akielekea Msumbiji ,amedai kuwa katika eneo hilo kuna mzunguko mkubwa wa nguvu za giza ,nguvu hizo ndio zilizosababisha kuingia kwenye mkondo na kumvuta hadi kuangukia hapo.

Baadhi ya mashuhuda wamedai sio kweli kama alikuwa akikatiza anga ya Tanzania kuelekea Mozambiki kwani ameonekana na vikoba akiwa na nakala ya rasimu ya katiba waliokuja nayo jamaa wa ccm ,iliyozua tafrani kiasi ya kuwafadhaisha CCM wenyewe ,hivyo amekuja kuwekeza vitu ili kuwazidii wale wanaoipinga rasimu ya katiba hiyo ya ccm yenye muelekeo mwengine ambaoni tofauti kabisa na ile rasimu ya Warioba iliyotokana na wananchi walio wengi.

Mwanga huyo ameshikiliwa na kusaidiwa kupewa nguo za kujisetiri.

Nahisi kuna mambo mengine huwa yanafanyika makusudi kutoa mwanya 'upepo upite'. Wananchi badala ya kufuatilia jambo fulani, basi akili zao huchotwa na tukio lisilo na miguu kama hili. Mchawi na rasimu ya katiba wapi na wapi??? Sina hakika na tukio hili na hata kama limetokea, halina uhalisia ndani yake, ninavyoamini mimi!!!!
 
wamuangalie vyema sio kiongoz wa maandamano ya chadema

Tony Gwanco, as a verified user I do advise you to think twice before you post any thing, otherwise you are highly undermining your personality. How could a witchman belonging to CHADEMA ranks be caught with a draft copy of the constitution prepared by CCM ranks? I have come across a your posts a number of time, most of them are rubbishes. Too sad, thanks that I do not know you, I would be ashamed to be associated with a person of small thinking capacity as yours, pretending to be a Great Thinker!

If you are one of CCM's fans, your contribution in destroying it is remarkable.
 
Back
Top Bottom