DOKEZO Kuna mchezo mchafu kwenye mfumo mpya wa kusajili madaktari (HPRS)

DOKEZO Kuna mchezo mchafu kwenye mfumo mpya wa kusajili madaktari (HPRS)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

ubelito

Senior Member
Joined
May 19, 2015
Posts
170
Reaction score
262
Mnamo tarehe 12 nilifanya malipo ya kuhuisha (renew) leseni yangu ya taaluma ili niweze kuendelea kufanya kazi kisheria kupitia mfumo mpya.

Nilitengeneza Control Number kupitia mfumo huo na nikafanya malipo kwa kutumia Airtel Money. Malipo yalifanikiwa bila tatizo lolote, kama inavyoonekana kwenye picha ya uthibitisho niliyoambatanisha.

Baada ya malipo kukamilika, nilipoingia kwenye mfumo nilikuta taarifa iliyosema:

"YOUR PAYMENT HAS BEEN RECEIVED BY COUNCIL, THANK YOU."

Hata hivyo, nilipojaribu kuendelea na mchakato wa CPD, mfumo ulinizuia na kunionesha kuwa bado sijafanya malipo.

Nilipoangalia sehemu ya Payment History, sikukuta kabisa kumbukumbu ya Control Number niliyolipia, licha ya malipo kukatwa kwenye akaunti yangu.

Kinachonishangaza zaidi ni kwamba wakati wa kufanya malipo, mfumo ulionesha wazi kuwa fedha zilikuwa zinalipwa kwenda Medical Council of Tanzania (MCT) pamoja na jina la mlipaji.

Jumatatu ya wiki hii niliwasiliana na MCT ili kupata ufafanuzi, lakini walinieleza kuwa kwenye mfumo wao hawaoni malipo yoyote yaliyofanyika kwa jina langu.

Naomba msaada wa kufuatilia tatizo hili na kufahamu fedha zangu zilipo, kwani nina ushahidi wa malipo yaliyofanyika. Nimeambatanisha picha za uthibitisho kwa rejea.

154759b9-6a2f-4d52-87b1-21acf5b04ef7.JPG

2d7c3048-65aa-4f33-88df-b86e7a6a3991.JPG

Screenshot 2026-07-14 at 20.22.15.jpg
 
Mwaka huu kila n'ganya basi n'ganya, ndo mana nasema awam hii mtu usipokuwa tajir hautakuja kuwa tena. Mana ni kujimegea tu kipande chako unapiga helq za wananchi
 
Back
Top Bottom