Kuna mgao wa maji unaendelea kimyakimya maeneo ya Tegeta?
Jamani hakuna mtu ambae haelewi umuhimu wa maji kwenye shughuli mbalimbali za kila siku. Sasa maji yanavyokosekana siku nzima bila taarifa yoyote wala tahadhari watu wajiandae mnataka watu tuishije?
DAWASA shida ni nini mpaka wakazi wa Tegeta maeneo ya Kibo, maeneo kuzunguka Hospitali ya Rabininsia, Nyaishozi, Namanga tunakosa maji, tena bila taarifa yoyote? Yaani toka jana asubuhi hola.
Mnatukwamisha.