Kuna Mgongano wa Katiba ya Zanzibar na ya Muungano, ufumbuzi wake tutake tusitake ni katiba mpya!

Na bado mtasoma katiba hadi nukta
Rais ni Samia S Hassan...mtake msitake
 
Nimekuelewa sana Mkuu. Kama ulivyosema tusiendelee kutegemea busara za viongozi ambazo ndio zinafanya kuonekana mambo yako sawa. Nakubaliana na wewe Katiba mpya ya JMT ndio itaimarisha Muungano zaidi
 
Hatuhitaji katiba mpya kwa sasa iliyopo inatosha,period. Nguvu zetu wote tuzielekeze kwenye kuwa-letea wananchi maendeleo.Tuungane wote katika hili.
After all mwananchi wa kawaida hana habari na katiba mpya,what he/she wants is a better life.
Watanganyika.nddio huwq hawana habari na Mambo hayo' Wazanzibar wanajua hili vizuri Sana na hawatanii katija hilli
 
Huu muungano ni feki, ulilazimishwa sana, chakushangaza hata baada ya miaka kadhaa kupita bado kuna mapungufu kwenye katiba ya JMT, kinachoonekana hapa wazanzibari wako busy kujipigania wakati huku bara tumesinzia tu, anyway labda tunasinzia kwasababu ya ubosi wetu kwasababu hata Rais wao tunawateulia sisi, hayo maneno waliyoweka kwenye Katiba yao ni urembo tu.
Tulijisahau tukadhani labda Marais wa Muungano kwa muda mrefu wataendelea kuwa ni watu kutoka Tanganyika na kwa hiyo watawadhibiti Wazanzibar kwa Majeshi kutoka Tanganyika, Tukasahau kuwa Mungu ana mipango yake maana hata hao Marais wa Tanganyika hawana guarantee ya Kumaliza terms zao madarakani na hivyo kutufanya tupate Marais kutoka Zanzibar kwa kustep in kwa mujibu wa katiba pindi lolote la kutokea likitokea.
Kwa hiyo kutegemea Rais Mzanzibari awafanyie Unyama Wazanzibari wenzie pindi wakilianzisha kule kwa kudai autonomy zaidi hilo sahau, sanasana atawapelekea FFU tu na siyo Wajeda kwenda kunyoosha mambo

Solution ya haya yote ili tusifike huko ni lazima tuandike katiba mpya ili kusolve haya mambo mapema. Tukiendelea kudhani eti Nia njema ya viongozi wa pande zote mbili ndiyo itaodoa hizi tofauti bila kufanya lolote la mabadiliko kwenye hizi katiba ni kujidnaganya kwelikweli!
 
Unaakili ndogo kama aliekuzaa
Ninyi mnaopanga mipango miovu nchi yetu iwe ya mashoga,mharibu familia na kuhamasisha wanawake watu-tawale wanaume ndio mna akili kubwa?Pumbafu kabisa,ungekuwa karibu yangu ningeku-toa ngeu.
 
Watanganyika.nddio huwq hawana habari na Mambo hayo' Wazanzibar wanajua hili vizuri Sana na hawatanii katija hilli
Mmelishwa matango mwitu na Wazungu hamuoni wala hamsikii.Ni mtindo wa ku-copy na ku-paste tu,originality zero.Sijui nani alituroga.Hivi aliyewaambia kila cha Mzungu ni kizuri nani,mngejua mmeingizwa mkenge!
 
Kwa katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, Wazanzibar walijipatia ushindi mkubwa sana katika lengo lao la kujichomoa kwenye makucha ya Tanganyika. Hapa Wazanzibar wanapaswa kuwashukuru Maalim Seif na Karume kwa kutumia Akili kubwa!

Naamini JK aliusoma huu mchezo ndo maana akakimbia harakaharaka kuleta katiba mpya ili kuilia denge move hii ya Wazanzibar, Unfortunately Magufuli hakuelewa gemu pana iliyokuwa inachezwa pale, akaamua kusitisha mpango wa Katiba mpya ile ya Chenge.

Naanza kushawishika lengo la Katiba ya Chenge siyo kuwapa wananchi katiba nzuri bali ilikuwa ni Kuondoa ukakasi wa move ya Wazanzibar ya mwaka 2010. Katiba halisi ya wananchi ilikuwa ni ya Warioba!

Pia ukichunguza kwa Makini kumbe kitendo cha Maalim kuingia kwenye SUK mwaka 2020 kunasaidia kulinda mafanikio ambayo Maalim Seif aliingia na Karume, Kama Maalim asingingia CCM walikuwa wanakwenda kubadili katiba ya Zanzibar na kuiondolea mafanikio amabyo Wazanzibar waliyapata katika move yao ya kujichomoa kutoka kwenye makucha ya Tanganyika kutokana na katiba yao ya 2010.

NYIE WATUNGA SERA , MSIBWETEKE, HUU MUUNGANO HAUKO SALAMA BILA KUSOLVE CONTRADICTION ZILIZOMO KWENYE KATIBA HIZI MBILI, HUU NI MUDA WA KATIBA MPYA ILI KUONDOA SINTOFAHAMU HIZI, MSITEGEMEE HISANI YA GOODWILL YA VIONGOZI WA PANDE HIZI MBILI KWA KUWA ETI WANATOKA CHAMA KIMOJA!, IPO SIKU TUTAPATA VIOGOZI WASIOSHIBANA WAKAZINGUANA KWA KILA MMOJA KUEGEMEA KATIBA YAKE AU IPO SIKU TUTAPATA VIONGOZI WOTE WAWILI NI WAZANZIBAR WAKASHIBANA SAANA NA WAKALINDA MASILAHI YA NCHI YAO YA ZANZIBAR KIKAMILIFU, HAPO HUU MUUNGANO UTAENDELEA KUWA WEAKENED!
 
Hukuona walivyoshiriki katika mchakato wa kutafuta Katiba mpya; hawa ni wananchi wa sasa siyo wa 1947!
How many out of 56 plus million?Acheni ku-cook taarifa.Na hata haoo.. hivi vi-NGO uchwara ndivyo vimewaghilibu.We know your motive,wala hamhangaikii katiba kwa ajili ya wananchi,it if for your evil motives.
 
Watanganyika.nddio huwq hawana habari na Mambo hayo' Wazanzibar wanajua hili vizuri Sana na hawatanii katija hilli
Kwani kila wanachokiona kizuri Wanzanzibari na sisi lazima tukione kizuri?Wewe vipi?We are not copy cats.Sisi tumesema katiba hapana,we have more important issues.
 
Kwa sasa inaonekana kama kila kitu kiko shwari katika muungano wetu lakini Ukweli ni kuwa kuna ufa mkubwa sana ambao ni hatari kwa muungano na nchi kiujumla.

Ukweli wenyewe ni kwamba Katiba mbili, yaani ya Muungano na ya Zanzibar (toleo la mwaka 2010)vinakinzana na hivyo kupelekea mkanganyiko ambao hauna afya kwa nchi na hivyo ili kuondoa jambo hili ambalo ni serious lazima mabadiriko katika Katiba ya Zanzibar au ya Muungano lazima yafanywe ili kurekebisha hili tatizo

Vifuatavyo ni vifungu katika katiba ya Zanzibar ambavyo vinapingana waziwazi na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1. Kipengele cha kwanza ni kuhusu Zanzibar kuwa ni nchi

Katiba ya Zanzibar ibara ya 1 imetamka kwa sauti kubwa kuwa ni NCHI na Imeainisha mipaka yake waziwazi

Ibara hiyo inasema hivi:

1. Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la
Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka
na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Kujitangaza huku kwa Zanzibar kuwa ni nchi haukuwemo kwenye toleo la kwanza la katiba ya mwaka 1984, Je ni kwa nini basi katika mabadiriko ya katiba hiyo toleo la 2010 Wazanzibar wakaamua kuiita Zanzibar kuwa ni nchi?

Wakati wazanzibar wakiutangaza Unchi wao na mipaka yao waziwazi kwenye katiba yao bado Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutambua uwepo wa nchi moja tu iitwayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mipaka ya hiyo Tanzania.

2. Ibara ya pili nayo ina contradiction, Katiba ya Zanzibar toleo la mwaka 2010 imetwaa Madaraka ambayo awali yalikuwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kumpa rais wa Zanzibar. Awali kabisa, katiba ya JMT ilikuwa ikimpa rais wa JMT uwezo wa kuigawa Zanzibar katika mikia na Wilaya kwa "kushauriana" na Rais wa Zanzibar lakini kwenye katiba ya Zanzibar, nguvu hizo kapewa rais wa Zanzibar kwa kufuata sheria zitakazotungwa na baraza la wawakilishi.

Ibara ya 2A ya Katiba ya Zanzibar toleo la 2010 inasema:

2A. Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais
aweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo
kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la
Wawakilishi

3. Katiba ya Sasa ya Muungano ibara ya 105(1)(b), Inatambua Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa Zamani, ambapo kuna cheo cha Wazairi kiongozi na siyo wa sasa wenye vyeo vya Makamu wa Kwanza na wa pili wa rais.

Hili siyo jambo dogo, maana ni ajabu uwe na kifungu cha katiba chenye kuelezea cheo ambacho hakipo!!. Kuacha ibara hii iendelee hivihivi kuwemo ndani ya katiba ja JMT wakati tayari Wazanzibar walisharekebisha muundo wa serikali yao maana yake inaweka hata question mark kwenye uhalali wa muundo mpya. Kunahitajika mabadiliko ya katiba ili kuweka jambo hili sawa!

4. Katiba ya Zanzibar ya toleo la 2010 inataka baraza la wawakilishi litunge sheria ya namna Wazanzibar watakavyoshiriki katika majeshi kwa ajili ya ulinzi wa Taifa

Kwanza tunajua kuwa kwa mujibu wa Katiba ya JMT, Suala la Majeshi ya Ulinzi wa Taifa ni suala la Muungano, Kwa muktadha huo, Sheria za Ulinzi wa JMT ni suala la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ninatambua wazi kuwa katiba ya Zanzibar haitumii neno Majeshi kuhusu vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, bali inatumia neno "Idara Maalumu". Wakati huohuo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitambui Mahali popote kuwa hizo Idara maalumu ni Majeshi ya Ulinzi wa Taifa!
Na Katiba ya nchi, yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepiga Marufuku kuanzisha Jeshi la Ulinzi kinyume cha Sheria ya bunge

Sasa swali la Msingi ni je?
(a). Hiyo katiba ya Zanzibar ilipotamka neno Majeshi ilimaanisha Majeshi gani?, kwa nguvu gani ambazo baraza la wawakilishi linazo juu ya majeshi hayo?

(b). Kama Kwa kutamka hilo neno "Majeshi" ilimaanisha idara Maalumu au vikosi Maalumu vya SMZ, Je Kamanda mkuu wa Vikosi hivyo ambaye kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ni rais wa Zanzibar sasa anaweza kuamuru vikosi hivyo kuingia vitani kuilinda Zanzibar?
Maana kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar toleo la 2010 rais wa Zanzibar ana mamlaka ya kuviagiza vikosi ya SMZ (idara maalum) kufanya mission yoyote atakayoona inafaa kwa ajili ya Maslahi ya Taifa (Zanzibar)

5. Katiba ya Zanzibar Imepoka Mamlaka ya Amiri Jeshi Mkuu.

Katiba Ya Zanzibar toleo la mwaka 2010 inatamka Vikosi Maalum ya SMZ kwa kutumia jina (Idara Maalum) na Imetaja Idara hizo kuwa Ni Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) na Jeshi la KMKM (Jeshi la Kuzuia Magendo) ba Idara ya Chuo cha Mafunzo(Magereza).
Na imetamka kwenye Ibara ya 123(1)Kuwa Rais wa Zanzibar atakuwa KAMANDA MKUU WA IDARA HIZO na Anaweza KUFANYA CHOCHOTE, pigia Msitari naneno KUFANYA CHOCHOTE kwa Ajili ya Maslahi ya Zanzibar, Sasa kama huu Siyo Uamiri jeshi mkuu ni nini?

Katiba hiyohiyo ibara ya 123(2) inasema kuwa Rais wa Zanzibar anaweza kuunda Idara nyingine yoyote atakayoona Inafaa na ANAWEZA KUIPA SHUGHULI YOYOTE ATAKAYOONA INAFAA KWA MANUFAA YA TAIFA. Pigia Msitari maneno "Shuguli yoyote", What if shughuli hiyo ikawa ni kupigana vita?
Sasa kama huu siyo uwezo wa Kuunda Majeshi kwa mgongo wa jina "Idara Maalum ni nini?"

6. Rais Wa Zanzibar akila Kiapo cha Kulinda Katiba ya Muungano (wakati wa kuapa kuwa mjumbe wa baraza la Mawaziri) na Akila Kiapo cha Kulinda Katiba ya Zanzibar anakuwa anaapa kufanya vitu vyenye contradiction

Tumeshaona, mahali ambapo katiba hizi mbili, Ya Zanzibar na ya Muungano zinapingana. Sasa ukiwa Rais wa Zanzibar ukaapa kulinda na kutetea vyote viwili, unakuwa unaapa viapo vyenye utata. Je utatekeleza kiapo gani kwanza maslahi ya pande mbili yakikwaruzana?
Mwisho Kabisa
Wazanzibar Katika katiba yao toleo la 2010 kuna Mambo wameyawekea Kinga yasibadiishwe kirahisi, Mojawapo ni ZANZIBAR KUWA NCHI, Ukitaka Kubadilisha hili ni lazima Uitishe kura ya Maoni ya Wazanzibar, Sasa Jiulize kama hili itawezekana?
Kwanza Kipengele hiki peke yake Kinaua Ndoto hata ya CCM ya Serikali mbili kuelekea kwenye Serikali Moja

Kwa hiyo Ndugu Zangu, ni lazima tukubaliane, Hatuwezi kuwa na katiba mbili nchini zinazokinzana, Hatuwezi kuwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotambua vyeo ambavyo Havipo, Hatuwezi kuwa na Katiba ya Zanzibar inayompa rais wa Sehemu moja ya Muungano uwezo wa Kuunda Vikosi na Akavipa "MISSION YOYOTE" atakayoona Inafaa kwa Masilihi ya Sehemu ya Nchi hiyo halafu tusiogope What If Mission hiyo ni Kutangaza Vita!

Kutokana na Hilo, TUNAHITAJI KATIBA MPYA itakayoondoa Mkanganyiko huu!

Hatuwezi kuendelea Kutegemea GOODWILL YA VIONGOZI kwenye kuudumisha huu Muungano,, Bali tunshitaji Mfumo wa Kikatiba na Kisheria Uliokaa sawa ili hsya mambo yaende vizuri, ili kesho na keshokutwa hata Marais wa Pande hizi mbili wasipotoka Chama Kimoja, Kila Rais ajue mipaka ya Majukumu yake Kikatiba.

KATIBA MPYA HAIEPUKIKI, TUNAWEZA KUJIFICHA KWENYE MCHANGA KAMA MBUNI TUKAJIAMINISHA KUWA KILA KITU KIKO SHWARI LAKINI SIYO KWELI.

TAIFA LINAHITAJI KATIBA MPYA!

Link ya Kupata katiba ya Zanzibar toleo la 2010 ni hii hapa chini:

Humu kuna ID zilupotea muda mrefu sana. Asantw Gamba la Joka
 
How many out of 56 plus million?Acheni ku-cook taarifa.Na hata haoo.. hivi vi-NGO uchwara ndivyo vimewaghilibu.We know your motive,wala hamhangaikii katiba kwa ajili ya wananchi,it if for your evil motives.
Dogo unaandika pumba kwa sababu ya tumbo lako. Ondoa aibu basi
 
Dogo unaandika pumba Mbkwa sababu ya tumbo lako. Ondoa aibu basi
Dogo?Temea mate chini Pythagoras,laiti ungenijua!

Any way,mimi sichumii tumbo,kama unavo dhani,I am self sufficient.Nipo JF ili kujaribu kunyoosha hoja potofu zinazo letwa humu na watu kama ninyi.

Nipo hapa pia kuleta hoja ambazo si rahisi kuzipata kwenye mainstream media, kwa sababu ya censorship.Nia ni kuelimisha na kuleta taarifa sahihi..
 
Kama weww sio mchumia tumbo ungeona haja ya kuboresha katiba yetu kwa maslahi ya taifa lakini kwa kuwa ni kinyume chako haya hicho unachosema uko self suffiecient ni kutokana na opportuniatic behaviour zako. You would have thought broadly.
 
Dogo unaandika pumba kwa sababu ya tumbo lako. Ondoa aibu basi
Hivi hivi vi-NGO vyenu si ndivyo vinaleta eti vilainishi na kutahiri wanaume!Hamna aibu kabisa,aliye-waambia hatuwezi kujitahiri nani.Huku ni kutuaibisha wanaume aisee.Yaani ninyi watu katika kuchumia tumbo na kufanya uovu hamna mwisho,you can do literally anything.
 
Kwani hiyo inatuzuia kuwaletea wananchi maendeleo?Mnashangazae...! Mmetumwa na mabwana zenu mtuletee choko choko nchini mwetu?Tumeshasema iliyopo inatosha.Tafuteni kazi nyingine mfanye,hapa hampati kitu.

Tunajua kwa nini mnang'ng'ania na kushupalia katiba mpya:mnataka kuchomekea mambo yenu ya kipuuzi kama ushoga,feminism,sheria za familia potofu nk.ili mharibu familia na jamii kwa ujumla.Hamta-pata nafasi ng'o.
Hicho kichwa kinankazi yake, usikitumie kubebea nywele tu!
 
Kwa sasa inaonekana kama kila kitu kiko shwari katika muungano wetu lakini Ukweli ni kuwa kuna ufa mkubwa sana ambao ni hatari kwa muungano na nchi kiujumla.

Ukweli wenyewe ni kwamba Katiba mbili, yaani ya Muungano na ya Zanzibar (toleo la mwaka 2010)vinakinzana na hivyo kupelekea mkanganyiko ambao hauna afya kwa nchi na hivyo ili kuondoa jambo hili ambalo ni serious lazima mabadiriko katika Katiba ya Zanzibar au ya Muungano lazima yafanywe ili kurekebisha hili tatizo

Vifuatavyo ni vifungu katika katiba ya Zanzibar ambavyo vinapingana waziwazi na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1. Kipengele cha kwanza ni kuhusu Zanzibar kuwa ni nchi

Katiba ya Zanzibar ibara ya 1 imetamka kwa sauti kubwa kuwa ni NCHI na Imeainisha mipaka yake waziwazi

Ibara hiyo inasema hivi:

1. Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la
Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka
na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Kujitangaza huku kwa Zanzibar kuwa ni nchi haukuwemo kwenye toleo la kwanza la katiba ya mwaka 1984, Je ni kwa nini basi katika mabadiriko ya katiba hiyo toleo la 2010 Wazanzibar wakaamua kuiita Zanzibar kuwa ni nchi?

Wakati wazanzibar wakiutangaza Unchi wao na mipaka yao waziwazi kwenye katiba yao bado Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutambua uwepo wa nchi moja tu iitwayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mipaka ya hiyo Tanzania.

2. Ibara ya pili nayo ina contradiction, Katiba ya Zanzibar toleo la mwaka 2010 imetwaa Madaraka ambayo awali yalikuwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kumpa rais wa Zanzibar. Awali kabisa, katiba ya JMT ilikuwa ikimpa rais wa JMT uwezo wa kuigawa Zanzibar katika mikia na Wilaya kwa "kushauriana" na Rais wa Zanzibar lakini kwenye katiba ya Zanzibar, nguvu hizo kapewa rais wa Zanzibar kwa kufuata sheria zitakazotungwa na baraza la wawakilishi.

Ibara ya 2A ya Katiba ya Zanzibar toleo la 2010 inasema:

2A. Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais
aweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo
kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la
Wawakilishi

3. Katiba ya Sasa ya Muungano ibara ya 105(1)(b), Inatambua Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa Zamani, ambapo kuna cheo cha Wazairi kiongozi na siyo wa sasa wenye vyeo vya Makamu wa Kwanza na wa pili wa rais.

Hili siyo jambo dogo, maana ni ajabu uwe na kifungu cha katiba chenye kuelezea cheo ambacho hakipo!!. Kuacha ibara hii iendelee hivihivi kuwemo ndani ya katiba ja JMT wakati tayari Wazanzibar walisharekebisha muundo wa serikali yao maana yake inaweka hata question mark kwenye uhalali wa muundo mpya. Kunahitajika mabadiliko ya katiba ili kuweka jambo hili sawa!

4. Katiba ya Zanzibar ya toleo la 2010 inataka baraza la wawakilishi litunge sheria ya namna Wazanzibar watakavyoshiriki katika majeshi kwa ajili ya ulinzi wa Taifa

Kwanza tunajua kuwa kwa mujibu wa Katiba ya JMT, Suala la Majeshi ya Ulinzi wa Taifa ni suala la Muungano, Kwa muktadha huo, Sheria za Ulinzi wa JMT ni suala la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ninatambua wazi kuwa katiba ya Zanzibar haitumii neno Majeshi kuhusu vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, bali inatumia neno "Idara Maalumu". Wakati huohuo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitambui Mahali popote kuwa hizo Idara maalumu ni Majeshi ya Ulinzi wa Taifa!
Na Katiba ya nchi, yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepiga Marufuku kuanzisha Jeshi la Ulinzi kinyume cha Sheria ya bunge

Sasa swali la Msingi ni je?
(a). Hiyo katiba ya Zanzibar ilipotamka neno Majeshi ilimaanisha Majeshi gani?, kwa nguvu gani ambazo baraza la wawakilishi linazo juu ya majeshi hayo?

(b). Kama Kwa kutamka hilo neno "Majeshi" ilimaanisha idara Maalumu au vikosi Maalumu vya SMZ, Je Kamanda mkuu wa Vikosi hivyo ambaye kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ni rais wa Zanzibar sasa anaweza kuamuru vikosi hivyo kuingia vitani kuilinda Zanzibar?
Maana kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar toleo la 2010 rais wa Zanzibar ana mamlaka ya kuviagiza vikosi ya SMZ (idara maalum) kufanya mission yoyote atakayoona inafaa kwa ajili ya Maslahi ya Taifa (Zanzibar)

5. Katiba ya Zanzibar Imepoka Mamlaka ya Amiri Jeshi Mkuu.

Katiba Ya Zanzibar toleo la mwaka 2010 inatamka Vikosi Maalum ya SMZ kwa kutumia jina (Idara Maalum) na Imetaja Idara hizo kuwa Ni Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) na Jeshi la KMKM (Jeshi la Kuzuia Magendo) ba Idara ya Chuo cha Mafunzo(Magereza).
Na imetamka kwenye Ibara ya 123(1)Kuwa Rais wa Zanzibar atakuwa KAMANDA MKUU WA IDARA HIZO na Anaweza KUFANYA CHOCHOTE, pigia Msitari naneno KUFANYA CHOCHOTE kwa Ajili ya Maslahi ya Zanzibar, Sasa kama huu Siyo Uamiri jeshi mkuu ni nini?

Katiba hiyohiyo ibara ya 123(2) inasema kuwa Rais wa Zanzibar anaweza kuunda Idara nyingine yoyote atakayoona Inafaa na ANAWEZA KUIPA SHUGHULI YOYOTE ATAKAYOONA INAFAA KWA MANUFAA YA TAIFA. Pigia Msitari maneno "Shuguli yoyote", What if shughuli hiyo ikawa ni kupigana vita?
Sasa kama huu siyo uwezo wa Kuunda Majeshi kwa mgongo wa jina "Idara Maalum ni nini?"

6. Rais Wa Zanzibar akila Kiapo cha Kulinda Katiba ya Muungano (wakati wa kuapa kuwa mjumbe wa baraza la Mawaziri) na Akila Kiapo cha Kulinda Katiba ya Zanzibar anakuwa anaapa kufanya vitu vyenye contradiction

Tumeshaona, mahali ambapo katiba hizi mbili, Ya Zanzibar na ya Muungano zinapingana. Sasa ukiwa Rais wa Zanzibar ukaapa kulinda na kutetea vyote viwili, unakuwa unaapa viapo vyenye utata. Je utatekeleza kiapo gani kwanza maslahi ya pande mbili yakikwaruzana?
Mwisho Kabisa
Wazanzibar Katika katiba yao toleo la 2010 kuna Mambo wameyawekea Kinga yasibadiishwe kirahisi, Mojawapo ni ZANZIBAR KUWA NCHI, Ukitaka Kubadilisha hili ni lazima Uitishe kura ya Maoni ya Wazanzibar, Sasa Jiulize kama hili itawezekana?
Kwanza Kipengele hiki peke yake Kinaua Ndoto hata ya CCM ya Serikali mbili kuelekea kwenye Serikali Moja

Kwa hiyo Ndugu Zangu, ni lazima tukubaliane, Hatuwezi kuwa na katiba mbili nchini zinazokinzana, Hatuwezi kuwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotambua vyeo ambavyo Havipo, Hatuwezi kuwa na Katiba ya Zanzibar inayompa rais wa Sehemu moja ya Muungano uwezo wa Kuunda Vikosi na Akavipa "MISSION YOYOTE" atakayoona Inafaa kwa Masilihi ya Sehemu ya Nchi hiyo halafu tusiogope What If Mission hiyo ni Kutangaza Vita!

Kutokana na Hilo, TUNAHITAJI KATIBA MPYA itakayoondoa Mkanganyiko huu!

Hatuwezi kuendelea Kutegemea GOODWILL YA VIONGOZI kwenye kuudumisha huu Muungano,, Bali tunshitaji Mfumo wa Kikatiba na Kisheria Uliokaa sawa ili hsya mambo yaende vizuri, ili kesho na keshokutwa hata Marais wa Pande hizi mbili wasipotoka Chama Kimoja, Kila Rais ajue mipaka ya Majukumu yake Kikatiba.

KATIBA MPYA HAIEPUKIKI, TUNAWEZA KUJIFICHA KWENYE MCHANGA KAMA MBUNI TUKAJIAMINISHA KUWA KILA KITU KIKO SHWARI LAKINI SIYO KWELI.

TAIFA LINAHITAJI KATIBA MPYA!

Link ya Kupata katiba ya Zanzibar toleo la 2010 ni hii hapa chini:

Nadhani katiba mpya sio suluhisho la tatizo, kwa sababu Zanzibar bado itapinga baadhi ya vipengele kama tulivyoona kwenye mchakato ulio pita. Suluhisho ni kuirudisha Tanganyika kama tuliifuta kimakosa, ama kama bado ipo basi itoke hadharani kama ilivyo Zanzibar badala ya kujificha nyuma ya JMT. Kwa kuwa wazanzibari walibaki na nchi yao kwa uwazi vivyo hivyo Tanganyika nayo iwepo kwa uwazi halafu tukae pamoja kuzungumzia namna ya muungano.
 
Hakuna haja ya kujitenga, tunaweza kupata muundo bora wa muungano.
Ikishindikana hiyo Katiba Mpya, basi wajitenge tu na hivyo kujitegemea kwa kila kitu! Natamani pia kuona siku moja na sisi tukijivunia Utanganyika wetu.
 
Back
Top Bottom