Kuna Mgongano wa Katiba ya Zanzibar na ya Muungano, ufumbuzi wake tutake tusitake ni katiba mpya!

Mmelishwa matango mwitu na Wazungu hamuoni wala hamsikii.Ni mtindo wa ku-copy na ku-paste tu,originality zero.Sijui nani alituroga.Hivi aliyewaambia kila cha Mzungu ni kizuri nani,mngejua mmeingizwa mkenge!
Vipi broo umepata Cha Meru au Tanangozi🥺🥺
 
2010 Zanzibar walipandisha bendera na kujitangaza kuwa ni nchi huru.
Sema tu walishindwa kupeleka nakala UN
Seif na Karume akili nyingi sana vichwani
Kwa move ile ya 2010 walitupiga kanzu huku tukikenua meno!
Sasa hivi Wazanzibar wana instruments zote za State in place, wanasubiri muda muafaka tu Tanganyika iwe dhaifu wafanye yao, na udhaifu huo unaweza kutokana na Vita (let say tuingie vitani na Malawi au nchi yoyote halafu hiyo vita ituache nyang'anyang'a), Uchumi kuyumba vya kutisha hadi tushindwe kuthibiti serikali, Machafuko ndani ya nchi ,etc

Ndiyo maana ni muhimu sana kusortout hizi issues la sivyo itakula kwetu
NI VIGUMU SANA KUTUMIA MAGUVU KUULINDA MUUNGANO, MAGUVU YANAWEZA KUTUMIKA MARA CHACHE LAKINI HUKU UKIBUY TIME KWA AJILI YA KUSORT OUT ISSUES KAMA HIZI, NJE YA HAPO UNAJIANDALIA DISASTER

Njia mojawapo ya kucleanup hii mess ni kuondoa migongano ya hizi katiba kwa Kuipa nchi katiba bora
 
Na bado mtasoma katiba hadi nukta
Rais ni Samia S Hassan...mtake msitake
Hakuna anayekataa kuwa rais ni Samia, hata hivyo Samia naye ni binadamu leo yupo kesho hayupo. Je tuendelee kufunikafunika haya mapengo ya katiba?
 
Why akija Rais Mzanzibari ndo kila mtanganyika anaona mapungufu ya Muungano?

Kipindi wazanzibari wanalalamika na Rais Mtanganyika mbona hamkuwa this vocal??
 
Ninyi mnaopanga mipango miovu nchi yetu iwe ya mashoga,mharibu familia na kuhamasisha wanawake watu-tawale wanaume ndio mna akili kubwa?Pumbafu kabisa,ungekuwa karibu yangu ningeku-toa ngeu.
Waombe ndugu zako wakusaidie ili upate matibabu mapema. Ukichelewa, unaweza kuishia kuokota makopo barabarani. Jilinganishe na wote wanaochangia humu ili uone ukubwa wa tatizo lako, lakini kwa bahati mbaya wenye magonjwa ya akili huwa hawana uwezo wa kutambua kuwa wanaugua. Waulize ndugu zako wa karibu kama wanakuona upo sawasawa.

Nakutakia uponywaji wa haraka.
 
Kwa sasa inaonekana kama kila kitu kiko shwari katika muungano wetu lakini Ukweli ni kuwa kuna ufa mkubwa sana ambao ni hatari kwa muungano na nchi kiujumla.

Ukweli wenyewe ni kwamba Katiba mbili, yaani ya Muungano na ya Zanzibar (toleo la mwaka 2010)vinakinzana na hivyo kupelekea mkanganyiko ambao hauna afya kwa nchi na hivyo ili kuondoa jambo hili ambalo ni serious lazima mabadiriko katika Katiba ya Zanzibar au ya Muungano lazima yafanywe ili kurekebisha hili tatizo

Vifuatavyo ni vifungu katika katiba ya Zanzibar ambavyo vinapingana waziwazi na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1. Kipengele cha kwanza ni kuhusu Zanzibar kuwa ni nchi

Katiba ya Zanzibar ibara ya 1 imetamka kwa sauti kubwa kuwa ni NCHI na Imeainisha mipaka yake waziwazi

Ibara hiyo inasema hivi:

1. Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la
Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka
na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Kujitangaza huku kwa Zanzibar kuwa ni nchi haukuwemo kwenye toleo la kwanza la katiba ya mwaka 1984, Je ni kwa nini basi katika mabadiriko ya katiba hiyo toleo la 2010 Wazanzibar wakaamua kuiita Zanzibar kuwa ni nchi?

Wakati wazanzibar wakiutangaza Unchi wao na mipaka yao waziwazi kwenye katiba yao bado Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutambua uwepo wa nchi moja tu iitwayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mipaka ya hiyo Tanzania.

2. Ibara ya pili nayo ina contradiction, Katiba ya Zanzibar toleo la mwaka 2010 imetwaa Madaraka ambayo awali yalikuwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kumpa rais wa Zanzibar. Awali kabisa, katiba ya JMT ilikuwa ikimpa rais wa JMT uwezo wa kuigawa Zanzibar katika mikia na Wilaya kwa "kushauriana" na Rais wa Zanzibar lakini kwenye katiba ya Zanzibar, nguvu hizo kapewa rais wa Zanzibar kwa kufuata sheria zitakazotungwa na baraza la wawakilishi.

Ibara ya 2A ya Katiba ya Zanzibar toleo la 2010 inasema:

2A. Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais
aweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo
kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la
Wawakilishi

3. Katiba ya Sasa ya Muungano ibara ya 105(1)(b), Inatambua Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa Zamani, ambapo kuna cheo cha Wazairi kiongozi na siyo wa sasa wenye vyeo vya Makamu wa Kwanza na wa pili wa rais.

Hili siyo jambo dogo, maana ni ajabu uwe na kifungu cha katiba chenye kuelezea cheo ambacho hakipo!!. Kuacha ibara hii iendelee hivihivi kuwemo ndani ya katiba ja JMT wakati tayari Wazanzibar walisharekebisha muundo wa serikali yao maana yake inaweka hata question mark kwenye uhalali wa muundo mpya. Kunahitajika mabadiliko ya katiba ili kuweka jambo hili sawa!

4. Katiba ya Zanzibar ya toleo la 2010 inataka baraza la wawakilishi litunge sheria ya namna Wazanzibar watakavyoshiriki katika majeshi kwa ajili ya ulinzi wa Taifa

Kwanza tunajua kuwa kwa mujibu wa Katiba ya JMT, Suala la Majeshi ya Ulinzi wa Taifa ni suala la Muungano, Kwa muktadha huo, Sheria za Ulinzi wa JMT ni suala la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ninatambua wazi kuwa katiba ya Zanzibar haitumii neno Majeshi kuhusu vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, bali inatumia neno "Idara Maalumu". Wakati huohuo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitambui Mahali popote kuwa hizo Idara maalumu ni Majeshi ya Ulinzi wa Taifa!
Na Katiba ya nchi, yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepiga Marufuku kuanzisha Jeshi la Ulinzi kinyume cha Sheria ya bunge

Sasa swali la Msingi ni je?
(a). Hiyo katiba ya Zanzibar ilipotamka neno Majeshi ilimaanisha Majeshi gani?, kwa nguvu gani ambazo baraza la wawakilishi linazo juu ya majeshi hayo?

(b). Kama Kwa kutamka hilo neno "Majeshi" ilimaanisha idara Maalumu au vikosi Maalumu vya SMZ, Je Kamanda mkuu wa Vikosi hivyo ambaye kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ni rais wa Zanzibar sasa anaweza kuamuru vikosi hivyo kuingia vitani kuilinda Zanzibar?
Maana kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar toleo la 2010 rais wa Zanzibar ana mamlaka ya kuviagiza vikosi ya SMZ (idara maalum) kufanya mission yoyote atakayoona inafaa kwa ajili ya Maslahi ya Taifa (Zanzibar)

5. Katiba ya Zanzibar Imepoka Mamlaka ya Amiri Jeshi Mkuu.

Katiba Ya Zanzibar toleo la mwaka 2010 inatamka Vikosi Maalum ya SMZ kwa kutumia jina (Idara Maalum) na Imetaja Idara hizo kuwa Ni Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) na Jeshi la KMKM (Jeshi la Kuzuia Magendo) ba Idara ya Chuo cha Mafunzo(Magereza).
Na imetamka kwenye Ibara ya 123(1)Kuwa Rais wa Zanzibar atakuwa KAMANDA MKUU WA IDARA HIZO na Anaweza KUFANYA CHOCHOTE, pigia Msitari naneno KUFANYA CHOCHOTE kwa Ajili ya Maslahi ya Zanzibar, Sasa kama huu Siyo Uamiri jeshi mkuu ni nini?

Katiba hiyohiyo ibara ya 123(2) inasema kuwa Rais wa Zanzibar anaweza kuunda Idara nyingine yoyote atakayoona Inafaa na ANAWEZA KUIPA SHUGHULI YOYOTE ATAKAYOONA INAFAA KWA MANUFAA YA TAIFA. Pigia Msitari maneno "Shuguli yoyote", What if shughuli hiyo ikawa ni kupigana vita?
Sasa kama huu siyo uwezo wa Kuunda Majeshi kwa mgongo wa jina "Idara Maalum ni nini?"

6. Rais Wa Zanzibar akila Kiapo cha Kulinda Katiba ya Muungano (wakati wa kuapa kuwa mjumbe wa baraza la Mawaziri) na Akila Kiapo cha Kulinda Katiba ya Zanzibar anakuwa anaapa kufanya vitu vyenye contradiction

Tumeshaona, mahali ambapo katiba hizi mbili, Ya Zanzibar na ya Muungano zinapingana. Sasa ukiwa Rais wa Zanzibar ukaapa kulinda na kutetea vyote viwili, unakuwa unaapa viapo vyenye utata. Je utatekeleza kiapo gani kwanza maslahi ya pande mbili yakikwaruzana?
Mwisho Kabisa
Wazanzibar Katika katiba yao toleo la 2010 kuna Mambo wameyawekea Kinga yasibadiishwe kirahisi, Mojawapo ni ZANZIBAR KUWA NCHI, Ukitaka Kubadilisha hili ni lazima Uitishe kura ya Maoni ya Wazanzibar, Sasa Jiulize kama hili itawezekana?
Kwanza Kipengele hiki peke yake Kinaua Ndoto hata ya CCM ya Serikali mbili kuelekea kwenye Serikali Moja

Kwa hiyo Ndugu Zangu, ni lazima tukubaliane, Hatuwezi kuwa na katiba mbili nchini zinazokinzana, Hatuwezi kuwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotambua vyeo ambavyo Havipo, Hatuwezi kuwa na Katiba ya Zanzibar inayompa rais wa Sehemu moja ya Muungano uwezo wa Kuunda Vikosi na Akavipa "MISSION YOYOTE" atakayoona Inafaa kwa Masilihi ya Sehemu ya Nchi hiyo halafu tusiogope What If Mission hiyo ni Kutangaza Vita!

Kutokana na Hilo, TUNAHITAJI KATIBA MPYA itakayoondoa Mkanganyiko huu!

Hatuwezi kuendelea Kutegemea GOODWILL YA VIONGOZI kwenye kuudumisha huu Muungano,, Bali tunshitaji Mfumo wa Kikatiba na Kisheria Uliokaa sawa ili hsya mambo yaende vizuri, ili kesho na keshokutwa hata Marais wa Pande hizi mbili wasipotoka Chama Kimoja, Kila Rais ajue mipaka ya Majukumu yake Kikatiba.

KATIBA MPYA HAIEPUKIKI, TUNAWEZA KUJIFICHA KWENYE MCHANGA KAMA MBUNI TUKAJIAMINISHA KUWA KILA KITU KIKO SHWARI LAKINI SIYO KWELI.

TAIFA LINAHITAJI KATIBA MPYA!

Link ya Kupata katiba ya Zanzibar toleo la 2010 ni hii hapa chini:

Ni kweli hizo ni chokochoko endelevu kwa sababu ya kutegemeana kiusalama. Hata hivyo hiyo katiba haifanyi kazi nje ya mipaka ya Zanzibar mpaka itambuliwe na Umoja wa Mataifa.

Katiba mpya sio suluhisho kamwe ila ndio mwanzo wa mianya mingi kukuzwa hatimaye kujitenga.

Dawa jina la Zanzibar lifutwe na iitwe Tanzania visiwani kama ilivyoanza baada ya kuungana na upande mwingine uitwe Tanzania bara. TZ visiwani iongozwe na Waziri kiongozi mwenye hadhi ya Waziri mkuu wakati TZ bara iongozwe na Waziri mkuu wote wakishughulika na serikali za mitaa. Pawepo na Rais mmoja tu wa Jamhuri ya muungano na makamu kutoka upande mwingine, hapo itakomesha kila mmoja kujidai.
 
Problem kubwa, ni kuwa Rais wa Zanzibar akiamua kuisimamia kikamilifu katiba ya Zanzibar aliyoapa kuilinda lazima atakwaruzana tu na rais wa JMT, kwa sababu katiba hizi mbili kuna vitu vya msingi sana zinapingana

Sasa huwezi kumtikisa rais wa Zanzibar kisha Muungano usipitie hali ya kuchafuka kwa hali ya hewa. Lazima Nguvu za Kijeshi zitatumika kurudisha hali sawa ikitokea situation kama hiyo na hilo halitaleta picha nzuri, na muungano wenyewe utageuka defacto occupation ambayo nayo haitodumu kwa sababu Wazanzibar wataikataa!

Ikitokea kwa mfano rais wa JMT akaamuru Majeshi ya Muungano kuingia Zanzibar Kutuliza hali, halafu rais wa Zanzibar naye akaamuru Vikosi Maalum vya SMZ viilinde Zanzibar unadhani nini kitatokea?, Kumbuka rais wa Zanzibar kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ana mamlaka za kuamuru vikosi vya SMZ kufanya LOLOTE kwa ajili ya Maslahi ya Zanzibar.
 
Why akija Rais Mzanzibari ndo kila mtanganyika anaona mapungufu ya Muungano?

Kipindi wazanzibari wanalalamika na Rais Mtanganyika mbona hamkuwa this vocal??
Hizi ishu za muungano watu walizihoji toka kipindi cha Nyerere, hata kipindi cha JK zilihojiwa sana.

By the way hoja ya msingi hapa siyo kupinga muungano, bali ni kuuboresha kupitia kuondoa mikanganyiko ya katiba hizi mbili za Zanzibar na JMT ambazo zinakinzana kwenye baadhi ya mambo ya msingi kwa kuja na katiba mpya
 
Hii katiba mpya CCM hawataki kwakua itawabana katika kuonea vyama vya upinzani.
Tatizo la wana CCM kuipenda CCM kuliko nchi, ipo siku wataamka watakuta mgogoro mkuubwa wa kikatiba baina ya pande hizi mbili za muungano unaoweza kuhatarisha hata muungano wenyewe, hapo ndipo watakapojua kuwa kukumbatia hii katiba ya Sasa kunaweza kuipa CCM madaraka ya muda mfupi tu(kwa kuwawezesha kuwachezea rafu wapinzani) LAKINI hakuimarishi huu muungano hasa baada ya move ya wazanzibar kuja na toleo la katiba yao la mwaka 2010 ambalo kuna vipengele ndani ya katiba hiyo vinapingana na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
 
Waombe ndugu zako wakusaidie ili upate matibabu mapema. Ukichelewa, unaweza kuishia kuokota makopo barabarani. Jilinganishe na wote wanaochangia humu ili uone ukubwa wa tatizo lako, lakini kwa bahati mbaya wenye magonjwa ya akili huwa hawana uwezo wa kutambua kuwa wanaugua. Waulize ndugu zako wa karibu kama wanakuona upo sawasawa.

Nakutakia uponywaji wa haraka.
Sijui unayemtumikia,lakini nadhani ni wale wale waliokulisha matango mwitu kwamba katiba ni muhimu.Katiba sio muhimu,kwa kuwa ziko nchi ambazo hazina written constitutions.Ningesema ujiongeze,lakini kwa kiwango ambacho wamesha
ku-brainwash,
indocrinate and enslave,sidhani kama una uwezo huo tena.Subiri the end game huku ukiendelea kuuchapa usingizi.

Kama katiba ingekuwa muhimu kwa kiwango unacho-fikiria wewe,Britain wangekuwa na a written constitution, lakini hawana! Don't you find this queer?Akili kichwani.Others with unwritten constitutions are Canada,
Israel, Libya, New Zealand, Oman and Saudi Arabia.
 
ni bora zanzibar wasichangie hata mia lakin tuendelee kuwa monitor kwa faida yetu. faida kuu za muungano wetu si hivi vitu vidogo kama bendera, mapato, na mgawanyo wa rasilimali. na faida si kwa tanzania bara tu bali usalama wa ukanda mzima. NI USALAMA WETU NA WASHIRIKA WETU! zanzibar peke yake haina nguvu ya kufanya ukanda wa bahar salama. hata yenyewe tu ni sehem ya hofu ya usalama wenyew. zanzibar wakiachwa wenyewe bara tutatumia gharama kubwa kulinda mipaka yetu ya bahari. usalama dhidi ya ugaidi, magendo na ushindan wa kibiashara na bandari.
kwahiyo, zanzibar tuwape vyote watakavyo kama ruzuku za umeme na kodi, hata wakope tu, miundombinu ya upendeleo, bendera, uwakilishi binafs kimichezo, wimbo, mifumo ya ndan ya kuongozana wenyewe, hata katika imani zao, ajira, ardhi, ndoa, biashara lakin si kwa ulinzi na usalama. La, ukanda mzima wa djibout had cape town hapatakuwa salama. lililokuwa tishio la ukommunist wakat ule na kupelekea muungano sasa tuna tishio la ugaid dhid ya watu na meli za mali.
hata kiuchumi hatuko tayar kupoteza mapato kwa njia rahis ya kuweka ushindan karib hiv sebulen. fikiria tu bandari yetu ya dsm tunayotegemea kuishi et iwekewe mshindan karib hivi pale Mangapwan unguja pawe international trade corridor!
Na bado kisiasa yan ccm ipoteze ruzuku nying tokana na seats za zanzibar kwa faida ya nan! (msinifokee nimewaza tu nje ya box).
 
Kwa sasa inaonekana kama kila kitu kiko shwari katika muungano wetu lakini Ukweli ni kuwa kuna ufa mkubwa sana ambao ni hatari kwa muungano na nchi kiujumla.

Ukweli wenyewe ni kwamba Katiba mbili, yaani ya Muungano na ya Zanzibar (toleo la mwaka 2010)vinakinzana na hivyo kupelekea mkanganyiko ambao hauna afya kwa nchi na hivyo ili kuondoa jambo hili ambalo ni serious lazima mabadiriko katika Katiba ya Zanzibar au ya Muungano lazima yafanywe ili kurekebisha hili tatizo

Vifuatavyo ni vifungu katika katiba ya Zanzibar ambavyo vinapingana waziwazi na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1. Kipengele cha kwanza ni kuhusu Zanzibar kuwa ni nchi

Katiba ya Zanzibar ibara ya 1 imetamka kwa sauti kubwa kuwa ni NCHI na Imeainisha mipaka yake waziwazi

Ibara hiyo inasema hivi:

"1. Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la
Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka
na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar."

Kujitangaza huku kwa Zanzibar kuwa ni nchi haukuwemo kwenye toleo la kwanza la katiba ya mwaka 1984, Je ni kwa nini basi katika mabadiriko ya katiba hiyo toleo la 2010 Wazanzibar wakaamua kuiita Zanzibar kuwa ni nchi?

Wakati wazanzibar wakiutangaza Unchi wao na mipaka yao waziwazi kwenye katiba yao bado Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutambua uwepo wa nchi moja tu iitwayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mipaka ya hiyo Tanzania.

2. Ibara ya pili nayo ina contradiction, Katiba ya Zanzibar toleo la mwaka 2010 imetwaa Madaraka ambayo awali yalikuwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kumpa rais wa Zanzibar. Awali kabisa, katiba ya JMT ilikuwa ikimpa rais wa JMT uwezo wa kuigawa Zanzibar katika mikoa na Wilaya kwa "kushauriana" na Rais wa Zanzibar lakini kwenye katiba ya Zanzibar, nguvu hizo kapewa rais wa Zanzibar kwa kufuata sheria zitakazotungwa na baraza la wawakilishi.

Ibara ya 2A ya Katiba ya Zanzibar toleo la 2010 inasema:

"2A. Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais
aweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo
kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la
Wawakilishi"

3. Katiba ya Sasa ya Muungano ibara ya 105(1)(b), Inatambua Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa Zamani, ambapo kuna cheo cha Waziri kiongozi na siyo muundo wa sasa wenye vyeo vya Makamu wa Kwanza na wa pili wa rais.

Hili siyo jambo dogo, maana ni ajabu uwe na kifungu cha katiba chenye kuelezea cheo ambacho hakipo!!. Kuacha ibara hii iendelee hivihivi kuwemo ndani ya katiba ja JMT wakati tayari Wazanzibar walisharekebisha muundo wa serikali yao maana yake inaweka hata question mark kwenye uhalali wa muundo mpya. Kunahitajika mabadiliko ya katiba ili kuweka jambo hili sawa!

4. Katiba ya Zanzibar ya toleo la 2010 inataka baraza la wawakilishi litunge sheria ya namna Wazanzibar watakavyoshiriki katika majeshi kwa ajili ya ulinzi wa Taifa

Kwanza tunajua kuwa kwa mujibu wa Katiba ya JMT, Suala la Majeshi ya Ulinzi wa Taifa ni suala la Muungano, Kwa muktadha huo, Sheria za Ulinzi wa JMT ni suala la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ninatambua wazi kuwa katiba ya Zanzibar haitumii neno Majeshi kuhusu vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, bali inatumia neno "Idara Maalumu". Wakati huohuo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitambui Mahali popote kuwa hizo Idara maalumu ni Majeshi ya Ulinzi wa Taifa!
Na Katiba ya nchi, yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepiga Marufuku kuanzisha Jeshi la Ulinzi kinyume cha Sheria ya bunge

Sasa swali la Msingi ni je?
(a). Hiyo katiba ya Zanzibar ilipotamka neno Majeshi ilimaanisha Majeshi gani?, kwa nguvu gani ambazo baraza la wawakilishi linazo juu ya majeshi hayo?

(b). Kama Kwa kutamka hilo neno "Majeshi" ilimaanisha idara Maalumu au vikosi Maalumu vya SMZ, Je Kamanda mkuu wa Vikosi hivyo ambaye kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ni rais wa Zanzibar sasa anaweza kuamuru vikosi hivyo kuingia vitani kuilinda Zanzibar?
Maana kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar toleo la 2010 rais wa Zanzibar ana mamlaka ya kuviagiza vikosi ya SMZ (idara maalum) kufanya shughuli(mission) yoyote atakayoona inafaa kwa ajili ya Maslahi ya Taifa (Zanzibar), pigia Msitari maneno SHUGHULI YOYOTE ATAKAYOONA INAFAA!

5. Katiba ya Zanzibar Imepoka Mamlaka ya Amiri Jeshi Mkuu.

Katiba Ya Zanzibar toleo la mwaka 2010 inatamka Vikosi Maalum ya SMZ kwa kutumia jina (Idara Maalum) na Imetaja Idara hizo kuwa Ni Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) na Jeshi la KMKM (Jeshi la Kuzuia Magendo) ba Idara ya Chuo cha Mafunzo(Magereza).
Na imetamka kwenye Ibara ya 123(1)Kuwa Rais wa Zanzibar atakuwa KAMANDA MKUU WA IDARA HIZO na Anaweza KUFANYA CHOCHOTE, pigia Msitari naneno KUFANYA CHOCHOTE kwa Ajili ya Maslahi ya Zanzibar, Sasa kama huu Siyo Uamiri jeshi mkuu ni nini?

Katiba hiyohiyo ibara ya 123(2) inasema kuwa Rais wa Zanzibar anaweza kuunda Idara nyingine yoyote atakayoona Inafaa na ANAWEZA KUIPA SHUGHULI YOYOTE ATAKAYOONA INAFAA KWA MANUFAA YA TAIFA. Pigia Msitari maneno "Shuguli yoyote", What if shughuli hiyo ikawa ni kupigana vita?
Sasa kama huu siyo uwezo wa Kuunda Majeshi kwa mgongo wa jina "Idara Maalum ni nini?"

6. Rais Wa Zanzibar akila Kiapo cha Kulinda Katiba ya Muungano (wakati wa kuapa kuwa mjumbe wa baraza la Mawaziri) na Akila Kiapo cha Kulinda Katiba ya Zanzibar anakuwa anaapa kufanya vitu vyenye contradiction

Tumeshaona, mahali ambapo katiba hizi mbili, Ya Zanzibar na ya Muungano zinapingana. Sasa ukiwa Rais wa Zanzibar ukaapa kulinda na kutetea vyote viwili, unakuwa unaapa viapo vyenye utata. Je utatekeleza kiapo gani kwanza maslahi ya pande mbili yakikwaruzana?
Mwisho Kabisa
Wazanzibar Katika katiba yao toleo la 2010 kuna Mambo wameyawekea Kinga yasibadiishwe kirahisi, Mojawapo ni ZANZIBAR KUWA NCHI, Ukitaka Kubadilisha hili ni lazima Uitishe kura ya Maoni ya Wazanzibar, Sasa Jiulize kama hili itawezekana?
Kwanza Kipengele hiki peke yake Kinaua Ndoto hata ya CCM ya Serikali mbili kuelekea kwenye Serikali Moja

Kwa hiyo Ndugu Zangu, ni lazima tukubaliane, Hatuwezi kuwa na katiba mbili nchini zinazokinzana, Hatuwezi kuwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotambua vyeo ambavyo Havipo, Hatuwezi kuwa na Katiba ya Zanzibar inayompa rais wa Sehemu moja ya Muungano uwezo wa Kuunda Vikosi na Akavipa "MISSION YOYOTE" atakayoona Inafaa kwa Masilihi ya Sehemu ya Nchi hiyo halafu tusiogope What If Mission hiyo ni Kutangaza Vita!

7. Katiba ya Zanzibar toleo la mwaka 2010 Imepoka mamlaka ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kuhusu uwezo wa Mzanzibari kukata rufaa katika mahakama ya Rufaa ya Tanzania kwa makosa yanayohusu uhuru na Haki za binadamu baada ya hukumu kuwa imetolewa na mahakama kuu ya Zanzibar.

Sote tunajua kuwa miongoni mwa mambo ya Muungano ni Mahakama ya Rufaa, hata hivyo katiba ya Zanzibar imemega mamlaka haya ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katiba ya Zanzibar inasema kwenye Ibara ya 24(3) kuwa:

"Rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahkama Kuu katika Shauri lililofunguliwa dhidi ya Masharti ya sura hii ya Katiba yatasikilizwa na Mahkama Kuu mbele ya Majaji watatu bila ya kujumuisha Jaji aliyeamua shauri hilo mara ya kwanza. Majaji hao watatu watateuliwa na Jaji Mkuu na uamuzi wao utakuwa ni wa mwisho na hautokatiwa rufaa kwenye Mahkama ya Rufaa ya Tanzania"

Kutokana na Hilo, TUNAHITAJI KATIBA MPYA itakayoondoa Mkanganyiko huu!

Hatuwezi kuendelea Kutegemea GOODWILL YA VIONGOZI kwenye kuudumisha huu Muungano,, Bali tunahitaji Mfumo wa Kikatiba na Kisheria Uliokaa sawa ili hsya mambo yaende vizuri, ili kesho na keshokutwa hata Marais wa Pande hizi mbili wasipotoka Chama Kimoja, Kila Rais ajue mipaka ya Majukumu yake Kikatiba.

KATIBA MPYA HAIEPUKIKI, TUNAWEZA KUJIFICHA KWENYE MCHANGA KAMA MBUNI TUKAJIAMINISHA KUWA KILA KITU KIKO SHWARI LAKINI SIYO KWELI.

TAIFA LINAHITAJI KATIBA MPYA!

Link ya Kupata katiba ya Zanzibar toleo la 2010 ni hii hapa chini:

Nimejaribu kwenda na mtiririko wako, lakini kuna vitu vya msingi vya kuangalia.
Mosi kuwa ni nchi au sio nchi kitu cha kuangalia ni nafasi yao katika UN, na AU, etc

Kuhusu waziri Kiongozi Vs Makamu wa Kwanza na wa pili hilo ni internal matters zao ambazo hazina madhara ktk Muungano wetu Mtukufu.

Kuhusu Majeshi, inajulikana wazi nani Amiri Jeshi Mkuu, na nani Mwenye kuweza kutangaza vita etc.

Kuhusu Mikoa n.k ni jambo dogo sana lisilo na impact, maana mwisho wa siku gharama ni zao na pale inapokuja kwenye Bunge la Muungano, ndio tunasema gharama za Muungano.
 
Ukweli ni kuwa hakuna kitu kidogo kinachokaa kwenye Katiba. Hata nukta, na koma iliyokaa kwenye katiba ina uzito wake, sembuse ibara nzima?

Huwezi kusema well ni kweli katiba hapa zinakinzana kwenye ishu ya kuteua wakuu wa mikoa lakini eti hicho ni kitu kidogo, Kitu kidogo kivipi?. Kingekuwa ni kitu kidogo kisingewekwa ndani ya katiba.

Unaposema inajulikana wazi kuwa Amiri Jeshi mkuu ni nani na ni nani anaweza kutangaza vita, Well huenda unafikiri hivyo na majority wanafikea hiyo ya Kimapokeo, lakini bahati mbaya ipo katiba ya Zanzibar ibayosema Rais wa Zabzibar anaweza kuunda Vikosi Vyovyote vya SMZ kadri arakavyoona inafaa na Anaweza kuviamuru kufanya Mission (Shughuli) yoyote atakayoona Inafaa kwa maslahi ya Zanzibar. Sasa siku akitokea rais akivituma hivyo vikosi kupiga mission za kijeshi kwa naslahi ya Zanzibar kinyume cha maslahi ya JMT ndo utajua mantiki ya kutaka kurekebisha hii kitu katika katiba ya Zanzibar

Kuhusu Waziri Kiongozi vs Makamo wawili, Hii nayo ni issue kubwa kwa sababu Katiba ya JMT ibara ya 105(1)(b) bado inatambua cheo cha Waziri Kiongozi wakati tuna vyeo vya Makamo walewawili. Sasa kwa mfano Iweje kuwepo na cheo tofauti na kikichotamkwa na Katiba?. Sasa hebu nisaidie IBARA hiyo ya katiba ya JMT inayotambua uwepo wa Waziri Kiongozi huko Zanzibar inakuwa enforced vipi?. Solution hapa ni either kuibadili katiba ya Zanzibar Iendane na ya Muungano au kuibadili ya Muungano ili iakisi changes zilizofanywa Zanzibar.

Sijaona Ukijibu hoja namba 7 ya Katiba ya Zanzibar kupoka Mamlaka ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, hili unalisemaje?

Kwa kuhitimisha nasema, kuwa Hakuna kitu kidogo kwenye katiba, Kila nukta, kila neno, kika koma iliyomo humo nilazime itekelezwe, Na viongozi wanaapa kuilinda, kuitetea na kuitekeleza!
 
Sasa hiyo katiba unayoizungumzia inatumika wapi ? Na madhara yake ni yapi
 
Usiangalie leo ambapo rais wa Zanzibar ni mtiifu kwa CCM na Powerbase ya nchi iliyoko Tanganyika

Chukulia Scenario ambapo unapata Rais wa Zanzibar asiye in good terms na viongozi wa bara halafu ana backup ya katiba ya nchi yake inayokinzana na katiba ya JMT, huoni mgogoro wa muungano hapo?.

Unakumbuka Scenario ya Jumbe?, Kule kuchafuka kwa hali ya hewa kungekuwa kubaya zaidi kama Jumbe asingekuwa mwana CCM na hivyo kudhibitiwa na vikao vya chama!

Pila ilikuwa rahisi kupunguza resistance ya Jumbe na haja ya kuweka majeshi mitaani kwa sababu baada ya kutegwa aje kikaoni bara, walimzuia kuondoka bara wakamfungia hukuhuku. Sasa fikiria scenario, Rais wa Zanzibar hayuko in good terms na rais wa Muungano halafu rais huyo kakomaa kuondoka Zanzibar, wakati huo ana sapoti kubwa ya wananchi wa Zanzibar na ana namlaka kwa mujibu wa katiba ya Zenji kutoa amri ya kuamuru vikosi vya SMZ kufanya "lolote" kwa maslahi ya Zanzibar. Itakuwaje?, Huoni Civil war hapo nchini?

Kuhusu Ishu ya Mahakama ya rufaa, wewe huoni Tatizo?, Mwalimu alikemea ishu ya Zanzibar kujiunga na OIC kwa sababu ya hoja za kikatiba tu, kuwa International relations ni issue ya muungano na hivyo katiba lazima iheshimiwe!, Likewise, Issue ya Mahakama ya rufaa ni issue ya Muungano, kwa hiyo katiba ya Zanzibar kupoka powers hizi za Mahakama ya rufaa ya TZ ni kubunja katiba ya JMT. Tatizo lipo, huwezi kuvunja katiba halafu ukasema maadamu hakuna athari unayoiona leo basi siyo big deal!
 
Ni kweli mkuu haya masuala yanaleta mkanganyiko sana! Pia mie naona ufumuzi usiishie kwenye kuwa na katiba moja ali pia kuwe na serikali moja tu ya jamhuri ya muugano wa Tanzania!
Hapa itaondoa utata wa serikali ya Tangayika kuvaa koti la serikali ya Muungano!
 
Back
Top Bottom