JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 2,118
- 4,863
Wakati viongozi wetu wako busy kununua madege ya kula bata na kizurula duniani badala ya kutengeneza mikakati ya kutengeneza ndege zetu za vita na mabomu ya nyuklia ya kujilinda dhidi ya vita ya tatu ya dunia waafrika tumejisahau sana ila tungejua tu kuwa bila mzungu kutukingia kifua hakuna race nyingine duniani ina hamu ya kuona waafrika tunaishi duniani hapa kabisa wakati hatuna mchango wowote katika maendeleo ya dunia hii ukizingatia idadi ya watu imeshafika billion 7 na mahitaji ya rasilimali zinazidi kupungua.
Corona ilikuwa jaribio lililofeli la wuhan bila mzungu kuingilia kati tusingetoboa.
Waafrika inabidi tuchague viongozi wenye akili ambao watajua kuwa kuweza kuendelea kubakia duniani hapa ni kuwa mbabe kwenye teknolojia na silaha za kivita wala siyo kununua madege ambayo unatumia mzungu akipenda.
Waafrika tuamke tuache starehe za mzungu kuna watu wanatamani watupige nyuklia tuondoke sema tu mzungu mstaarabu ila ustaarabu utawashinda nao maana kuna wairani hawatutaki kabisa sisi waafrika , pia wa Asia nao hawatutaki kabisa imagine warabu hadi leo wanatuita watumwa.
Ifike wakati tujikite kwenye teknolojia tuache kudhani kwamba kilakitu tunachokitumia lazima kitoke nje hata toothpick tutakuja kupigwa vibaya sana, tunakoelekea ni giza baya sana kwetu waafrika.
Kama hatuna viongozi wa kuweza kutuongoza kujisimamia kitechnolojia sisi wafrika hatuna tofauti na mifugo basi tusubiri kuchinjwa kama kuku au kitimoto siku ikifika