Kuna mimba kweli hapa au ndo najazwa kwenye mfumo

Ni ile sogea tukae sijamttolea mahari na hata huo mpango sina maana nilimkuta na mtoto ingawa mtoto yupo kwa bibi yake
Duuh kumbe mke wa mtu kabsaa
Kwa hiyo mechi inaanza 1-0
Tayar mwezako ameingia na goli moja uwanjani
Tafuta mke wako uoe kijana acha kudandia wake za watu
 
Single mother mtaani ndo wengi ukilinganisha na wale ambao hawajazalishwa maana hao ambao siyo single mother wengi wanafunzi ko kwa nanmna yoyote mtego wa kudate na single mother ni ngumu kuukwepa ,, maana unaweza kuikuta pisi na ukasema hii nimeopoa halafu baadae inakuja kukwambia ina watoto wawili
 
Mkuu kuna redflag ambazo tayar zimeonekana lakini unajipa moyo kwamba hakuna kitu,unafeli big time

Password kila sehemu inamaana kuna mambo mazito sana hapo

Simu anapigiwa saa nne usiku na hapokei,hapo unafikir kuna nini

Ikapigwa tena asubuhi hakupokea,ndio ukapokea wewe

Moja wapo ya dalili ya kupungua kwa mapenzi ni kukosekana kwa mawasiliano baina yenu,unasema ukisafiri huwa hana mpango wa kukucheki kabisa,aisee huyo yupo kwako kimwili ila kihisia yupo kwingine kabisa

Tunza hii risiti utakuja kuikumbuka baadae
 
Kwa nini ikuambie baadae
Kwani unaoa kwenye giza au siku hiyo hiyo ukitongoza usiku unabeba usiku huo huo
Duuh vijana wa mwendo Kasi ndiyo maana mnalia lia hadi wanawake wanawazidi akili

Acha mpigwe tuu akili mmefungia stoo yaan unashidwa kujua mwanamke mwenye mtoto
Hayo ndiyo madhara ya kutoenda jandoni
 
Mkuu kuna redflag ambazo tayar zimeonekana lakini unajipa moyo kwamba hakuna kitu,unafeli big time

Password kila sehemu inamaana kuna mambo mazito sana hapo

Simu anapigiwa saa nne usiku na hapokei,hapo unafikir kuna nini

Ikapigwa tena asubuhi hakupokea,ndio ukapokea wewe

Moja wapo ya dalili ya kupungua kwa mapenzi ni kukosekana kwa mawasiliano baina yenu,unasema ukisafiri huwa hana mpango wa kukucheki kabisa,aisee huyo yupo kwako kimwili ila kihisia yupo kwingine kabisa

Tunza hii risiti utakuja kuikumbuka baadae
Sasa amekuta mwanamke ana mtoto unategemea nini
Lazima awasiliane na baba wa mtoto usiku
 
Huyo mwanamke hajitambui,hata kama ndio baba mtoto kuna mipaka ambayo inatakiwa iwekwe

Apige muda ambao ni rafiki,na sio usiku mkubwa yupo na mwanaume wake

Ila nahisi kuna mambo ambayo ni zaidi ya baba mtoto hapo
 
Salam wakuu. nisiwachoshe moja kwa moja kwenye mada

Wakuu kuna binti nimekuwa nae karibia miezi sita

Sasa miezi kama miwili iliyopita aliniambia mara nyingi amekuwa ni mtu wa kujisikia hovyo, nikamuuliza anijisikia hovyo kivp

Akasema amekuwa ni mtu kuhisi kichefuchefu, muda mwingine anatapika, pamoja na kuhisi kizunguzungu mi nikaelewa kwa sabab hizo huwa ni dalili za mimba , hasa nikamwambia aende akapime aone anasumbuliwa na nini

Kweli akaenda kupima ni ikabainika ana mimba ya miezi miwili,

Lakini mimi kulingana na siku ambazo tulikuwa tumekutana nikapata kigugumizi kwamba inawezekanaje iwe mimba yangu basi nikaamua kumuuliza hiyo mimba ni ya nani, akadai mimba yako hii yaani mimba yangu

Mimi nikawa na wasiwasi na nikamwambia hiyo mimi siyo mimba yangu kama vp katafute baba wa hiyo mimba

Baada ya kumwambia vile akaanza kulalamika sana lakini mimi nikasimamia msimamo huo huo

Sasa baadae akadai kwa vile mimba nimeikataa acha tu akaitoe

baadae nikakaa chini nikafikiria nikaona labda kweli inawezekana ni mimba yangu, nikakubali kishingo upande ila nikawa bado nina wasiwasi

Tumeenda enda baada ya kama mwezi mmoja nikaanza kuona mabadiliko

Kwanza simu yake akaiwekea pasword kila sehem, hilo nikapotezea wala sikumuuliza chochote, maana sinaga utaratibu wa kumchunguza

Baadae likaibuka jambo jingine, akawa ni mtu wa kuongea na simu kuliko kawaida

Haipiti dakika mbili yuko na simu sikion hilo sikufatilia sana

Siku moja ikapiga namba ngeni hakupokea akapiga mara ya pili hakupokea ,muda huo ni saa nne usiku nikaamuuliza akawa na majibu hayaeleweki nikapotezea

Siku ya pili namba ile ile ikapiga nikaiwahi nikaipokea ikasikika sauti ya kidume baada ya mimi kuitika huku simu ikakatwa, tukio hilo likazua ugomvi mkubwa baadae tukasuluhisha yakaisha

Mbali na hivyo ikitokea nimesafiri amekuwa ni mtu ambae hajali chochote kunihusu yaani hutoona amepiga simu hadi mimi nipige ndo atajifanya anauliza maendeleo yako

Sasa kwa mtiririko huu na kwa uzoefu wenu nyinyi unahisi hapa kuna mimba au nimepigwa

Maana mimi kama mimi naona kuna kila dalili ya kulea mimba ya msela

Kitu ambacho naona kama kinaweza kuja kuleta maafa huko mbeleni

Yapi maoni yenu karibuni
Pole sana kaka.
Maelezo haya yanatosha ku conclude kuwa hapo umepigwa kaka, siyo mimba yako hiyo Believe me or not.

My Take: Baki kwenye msimamo uleule kuwa mimba siyo yako, na drop her.
 
Komaa hadi mtoto atoke anafana na wewe, sisi hapa tuko pamoja na wewe.....
 
N mimba tuu hiyo mkuu, akijifungua atakaa sawa

Huyo jamaa anayeongea nae n kaka yake 😂
 
Huyo mwanamke hajitambui,hata kama ndio baba mtoto kuna mipaka ambayo inatakiwa iwekwe

Apige muda ambao ni rafiki,na sio usiku mkubwa yupo na mwanaume wake

Ila nahisi kuna mambo ambayo ni zaidi ya baba mtoto hapo
Huwez jua pengine ni afisa utelezi
 
Ni ile sogea tukae sijamttolea mahari na hata huo mpango sina maana nilimkuta na mtoto ingawa mtoto yupo kwa bibi yake
We nae unaishije na single maza?yani jitu limepiga umalaya huko,wewe ndio unakuja kulizoa?
 
Mwambie huyo mwanamke huyo mtoto atapimwa vinasaba (DNA) akizaliwa...

Kama ikibainika mtoto sio wa kwako utaachana nae,

Lazima atajiongeza..

Unatakiwa kuwa na msimamo,,usipende kihivyooo..ukipenda sana utaruhusu mwanamke aku cheat, akuletee watoto sio wako kila siku..

Wala usiwe na presha mkuu, hivyo vitu siku hizi vinapimwa, mimba sio yako au yako itajulikana tu ukiamua..
 
Salam wakuu. nisiwachoshe moja kwa moja kwenye mada

Wakuu kuna binti nimekuwa nae karibia miezi sita

Sasa miezi kama miwili iliyopita aliniambia mara nyingi amekuwa ni mtu wa kujisikia hovyo, nikamuuliza anijisikia hovyo kivp

Akasema amekuwa ni mtu kuhisi kichefuchefu, muda mwingine anatapika, pamoja na kuhisi kizunguzungu mi nikaelewa kwa sabab hizo huwa ni dalili za mimba , hasa nikamwambia aende akapime aone anasumbuliwa na nini

Kweli akaenda kupima ni ikabainika ana mimba ya miezi miwili,

Lakini mimi kulingana na siku ambazo tulikuwa tumekutana nikapata kigugumizi kwamba inawezekanaje iwe mimba yangu basi nikaamua kumuuliza hiyo mimba ni ya nani, akadai mimba yako hii yaani mimba yangu

Mimi nikawa na wasiwasi na nikamwambia hiyo mimi siyo mimba yangu kama vp katafute baba wa hiyo mimba

Baada ya kumwambia vile akaanza kulalamika sana lakini mimi nikasimamia msimamo huo huo

Sasa baadae akadai kwa vile mimba nimeikataa acha tu akaitoe

baadae nikakaa chini nikafikiria nikaona labda kweli inawezekana ni mimba yangu, nikakubali kishingo upande ila nikawa bado nina wasiwasi

Tumeenda enda baada ya kama mwezi mmoja nikaanza kuona mabadiliko

Kwanza simu yake akaiwekea pasword kila sehem, hilo nikapotezea wala sikumuuliza chochote, maana sinaga utaratibu wa kumchunguza

Baadae likaibuka jambo jingine, akawa ni mtu wa kuongea na simu kuliko kawaida

Haipiti dakika mbili yuko na simu sikion hilo sikufatilia sana

Siku moja ikapiga namba ngeni hakupokea akapiga mara ya pili hakupokea ,muda huo ni saa nne usiku nikaamuuliza akawa na majibu hayaeleweki nikapotezea

Siku ya pili namba ile ile ikapiga nikaiwahi nikaipokea ikasikika sauti ya kidume baada ya mimi kuitika huku simu ikakatwa, tukio hilo likazua ugomvi mkubwa baadae tukasuluhisha yakaisha

Mbali na hivyo ikitokea nimesafiri amekuwa ni mtu ambae hajali chochote kunihusu yaani hutoona amepiga simu hadi mimi nipige ndo atajifanya anauliza maendeleo yako

Sasa kwa mtiririko huu na kwa uzoefu wenu nyinyi unahisi hapa kuna mimba au nimepigwa

Maana mimi kama mimi naona kuna kila dalili ya kulea mimba ya msela

Kitu ambacho naona kama kinaweza kuja kuleta maafa huko mbeleni

Yapi maoni yenu karibuni
Una oneshwa hadi picha bado huoni
 
Back
Top Bottom