Kuna mimba kweli hapa au ndo najazwa kwenye mfumo

Kuna mimba kweli hapa au ndo najazwa kwenye mfumo

Nikiwa nina mshkaji kama wewe huwa napiga makofi akili zikae sawa
 
Salam wakuu. nisiwachoshe moja kwa moja kwenye mada

Wakuu kuna binti nimekuwa nae karibia miezi sita

Sasa miezi kama miwili iliyopita aliniambia mara nyingi amekuwa ni mtu wa kujisikia hovyo, nikamuuliza anijisikia hovyo kivp

Akasema amekuwa ni mtu kuhisi kichefuchefu, muda mwingine anatapika, pamoja na kuhisi kizunguzungu mi nikaelewa kwa sabab hizo huwa ni dalili za mimba , hasa nikamwambia aende akapime aone anasumbuliwa na nini

Kweli akaenda kupima ni ikabainika ana mimba ya miezi miwili,

Lakini mimi kulingana na siku ambazo tulikuwa tumekutana nikapata kigugumizi kwamba inawezekanaje iwe mimba yangu basi nikaamua kumuuliza hiyo mimba ni ya nani, akadai mimba yako hii yaani mimba yangu

Mimi nikawa na wasiwasi na nikamwambia hiyo mimi siyo mimba yangu kama vp katafute baba wa hiyo mimba

Baada ya kumwambia vile akaanza kulalamika sana lakini mimi nikasimamia msimamo huo huo

Sasa baadae akadai kwa vile mimba nimeikataa acha tu akaitoe

baadae nikakaa chini nikafikiria nikaona labda kweli inawezekana ni mimba yangu, nikakubali kishingo upande ila nikawa bado nina wasiwasi

Tumeenda enda baada ya kama mwezi mmoja nikaanza kuona mabadiliko

Kwanza simu yake akaiwekea pasword kila sehem, hilo nikapotezea wala sikumuuliza chochote, maana sinaga utaratibu wa kumchunguza

Baadae likaibuka jambo jingine, akawa ni mtu wa kuongea na simu kuliko kawaida

Haipiti dakika mbili yuko na simu sikion hilo sikufatilia sana

Siku moja ikapiga namba ngeni hakupokea akapiga mara ya pili hakupokea ,muda huo ni saa nne usiku nikaamuuliza akawa na majibu hayaeleweki nikapotezea

Siku ya pili namba ile ile ikapiga nikaiwahi nikaipokea ikasikika sauti ya kidume baada ya mimi kuitika huku simu ikakatwa, tukio hilo likazua ugomvi mkubwa baadae tukasuluhisha yakaisha

Mbali na hivyo ikitokea nimesafiri amekuwa ni mtu ambae hajali chochote kunihusu yaani hutoona amepiga simu hadi mimi nipige ndo atajifanya anauliza maendeleo yako

Sasa kwa mtiririko huu na kwa uzoefu wenu nyinyi unahisi hapa kuna mimba au nimepigwa

Maana mimi kama mimi naona kuna kila dalili ya kulea mimba ya msela

Kitu ambacho naona kama kinaweza kuja kuleta maafa huko mbeleni



Yapi maoni yenu karibuni
Leta mzunguko wake na siku uliopiga mshindo wazee wa nongwa tukokotoe
 
Ni ile sogea tukae sijamttolea mahari na hata huo mpango sina maana nilimkuta na mtoto ingawa mtoto yupo kwa bibi yake

Kama ni hivyo basi si mali yako jivyo anaweza akafanya vyovyote anavyojisikia...

Huna mamlaka juu yake...
 
Single mother mtaani ndo wengi ukilinganisha na wale ambao hawajazalishwa maana hao ambao siyo single mother wengi wanafunzi ko kwa nanmna yoyote mtego wa kudate na single mother ni ngumu kuukwepa ,, maana unaweza kuikuta pisi na ukasema hii nimeopoa halafu baadae inakuja kukwambia ina watoto wawili
Sina cha kusema hapa. Ila naomba kuuliza Kwani akishakwamvia kuwa ana watoto 2 au 3 anakuwa amekufunga pingu ushindwe kuondoka?.
Naulizia tu usinijibu Kwa hasira.
 
Back
Top Bottom