Kuna mitaa imelaaniwa

Kuna mitaa imelaaniwa

Ulishawahi kukuta mtaa fulani hali ya maisha ya kaya zoote hapo choka mbaya? Mtaa wote umejaa makahaba! Mtaa umejaa walevi! Watoto au kizazi ndani ya huo mtaa hawamalizi darasa la saba au kidato cha nne!

Ndani ya huo mtaa hakuna mtumishi wa umma mwenye mshahara unaoeleweka! Hakuna familia yenye gari na kama lipo ni mkweche! Wanawake ni kupiga majungu na wanaume vijiwe vya kahawa na draft!.

Ndo nikagundua sio tu kuwepo kwa familia zilizolaaniwa, lakini pia kuna mitaa iliyolaaniwa! Kuna vijiji/kata zimelaaniwa! Kuna wilaya zimelaaniwa (kama wilaya ya kisarawe)!

Kuna miji imelaaniwa miji mingi katika mikoa ya pwani, Tabora na kigoma! Unapokuwa unatafuta maisha fanya uchunguzi wa mitaa/kata/wilaya/miji unayoenda vinginevyo hutoboi! Mwisho wa siku lazima hali yako ya maisha iendane na wao!

Nikagundua nyuma ya pazia kuna wachawi wanakaa katika malango ya njia kuratibu kila anayekuja na kuishi hapo na kumpiga tukio! Haya mambo magumu sana kuelewa!
Una hoja mkuu, Kuna mitaa ukiishi maisha yatakuchapa balaa.

Mtumishi Rabbon Mfalme Sulemani ongezeni neno...
 
Tatizo letu ni kuhusianisha kila kitu na ushirikina. Inachekesha kuona kwamba nchi zilizoendelea hua zinaliona bara zima la Afrika ni kama limelaaniwa kwa jinsi lilivyo nyuma, wakati huo huo eti na sisi humu ndani tunanyoosheana vidole kwamba eneo fulani limelaaniwa..[emoji38][emoji38]

Wakati kiuhalisia sisi wote ni giza tupu tofauti ni ndogo sanaa..
Hitabia ya kusema umasini laana imeanzishwa na wachungaji kuwadanganya wafuasi wao hili wapige hela
 
Hizo sehemu ulizosema hazina maendeleo ndio Zina uzinzi, ukahaba, madawa, wizi, uchawi etc na hivyo siyo rahisi kupata maendeleo. Hivyo vitu na roho ya maendeleo ni maji na mafuta. Niambie mtu anayetumia madawa au mwasherati mwenye maendeleo. Refer wasanii wetu
Nchi nyingi zinaongoza kwa ukahaba na ushoga tena zinaongoza kwa maendeleo ya kila kitu tatizo lako ukiona mtu tajiri unadhi kabalikiwa na ukimuona masikini unamuona kalaniwa basi kuanzia baba babu zako mpaka wewe mwenyewe mnayo laana
 
Hizo Imani tu ukizipa Nguvu na zenyewe zinakupa Nguvu

Mtu kama haunywi Pombe ,bangi wala sigara na unajitenga na uasherati Uzinzi hata Kama unaendesha bodaboda tu lazima ufanikiwe hatua kubwa SANA.

Watu wanwekeza katika Uzinzi ,pombe Umalaya then wakikwama wanasema laana au kurogwaa .

Hii mitaa ya Uswahilini Mimi ndo naishi wapo wapemba wanamaisha. Safi Sana na watu waswahili wapo vizuri ila Hawa wanawake na vijana wanaoendekeza tabia mbaya ndo Maisha yanawatoa mchezoni Mapema.
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Naunga mkono hoja, mitaa waliokaa waarabu ndiyo inaongoza. Sijui hao jamaa walituachia kitu gani. Chunguza vizuri palipokuwa na miarabu huwezi toboa.
 
Ulishawahi kukuta mtaa fulani hali ya maisha ya kaya zoote hapo choka mbaya? Mtaa wote umejaa makahaba! Mtaa umejaa walevi! Watoto au kizazi ndani ya huo mtaa hawamalizi darasa la saba au kidato cha nne!

Ndani ya huo mtaa hakuna mtumishi wa umma mwenye mshahara unaoeleweka! Hakuna familia yenye gari na kama lipo ni mkweche! Wanawake ni kupiga majungu na wanaume vijiwe vya kahawa na draft!.

Ndo nikagundua sio tu kuwepo kwa familia zilizolaaniwa, lakini pia kuna mitaa iliyolaaniwa! Kuna vijiji/kata zimelaaniwa! Kuna wilaya zimelaaniwa (kama wilaya ya kisarawe)!

Kuna miji imelaaniwa miji mingi katika mikoa ya pwani, Tabora na kigoma! Unapokuwa unatafuta maisha fanya uchunguzi wa mitaa/kata/wilaya/miji unayoenda vinginevyo hutoboi! Mwisho wa siku lazima hali yako ya maisha iendane na wao!

Nikagundua nyuma ya pazia kuna wachawi wanakaa katika malango ya njia kuratibu kila anayekuja na kuishi hapo na kumpiga tukio! Haya mambo magumu sana kuelewa!
Ndioo
 
Mitaa ambayo haijalaaniwa ni ipi?? Fikira za namna hii ndio chanzo cha kuwepo imani kama zile zinzopelekea kuua binaadamu wenzetu wenye albinism. Jitume kwa bidii kwenye kila ufanyacho utafanikiwa, hakuna miujiza. Hakuna mtaa wenye laana, ila kuna mitaa yenye watu wenye asili ya uvivu wengi na wamekutana na mazingira yanayo support utamaduni wao wa uvivu
 
Una hoja mkuu, Kuna mitaa ukiishi maisha yatakuchapa balaa.

Mtumishi Rabbon Mfalme Sulemani ongezeni neno...
Pwani, bagamoyo,Tanga, tabora bukoba, lindi na mtwara, in short, mkoa au wilaya au nchi iliyokaliwa na waswahili na waarabu kwanini Ina Ujinga na Umaskini wa umekithiri?

Tatizo ni IBADA za sanamu, na Kutoa sadaka Kwa mashetani, waarabu na waswahili na Dini Ile huambatana na majini, na kutegemea Waganga na majini na miungu yule wa Baharini lazima Nchi ilaaniwe, lazima watu walaaniwe,

Kutoa sadaka Kwa shetani, lazima afunge kipato, lazima akupe magonjwa, lazima awaambukize chuki na Roho mbaya, lazima umalaya ukithiri, wizi nk nk.

Majini, shetani, waendaji Kwa Waganga na Kutoa sadaka huko, lazima wawe maskini wa kutupa, sababu shetani ni mlaaniwa,

KAZI ya shetani ni wizi, UOVU, uharibifu, uuaji na UOVU wote,

Likewise, sehemu zote, walipopita missionaries na kuhubiri INJILI na Neno la Mungu, Ujinga ulidondoka, magonjwa yaliondoka na Umaskini ulidondoka, sababu Mungu anayehubiriwa kwenye INJILI, ni Mungu wa Kweli Yesu mwenye baraka, Upendo na Amani,HAKI.

Likewise, hata katika uongozi, akitawala wa Dini Ile, lazima Hali iwe ngumu Kwa wananchi,lazima wizi uongezeke, ufisadi,uvivu uongezeke nk nk, sababu kuu ni IBADA ya sanamu Kwa ibilisi na makafara.

Mungu atusaidie, maana nyota njema imeonekana juu ya nchi yetu, Mlawi anakwenda kuwa Ajaye,

Baraka lazima zitatamalaki juu ya nchi, na LAANA kutuondoka.

Amen
 
Kuna mtaa mmoja maeneo ya buguruni, wanaofungua biashara mitaa ile kama ni mgeni sio mzawa wa pale ukitoboa miezi 4 wewe ni kigume na wenyewe wanasema .
Kuna mwamba mmoja/mshikaji kutoka Zenji alifungua biashara amedumu pale kama miaka 2 anasema kuna mzee alimfuata akamwambia "Wewe ni kidume kweli"
 
Huu uzi umenikumbusha mtaa wa Mtupie eneo la Chumbageni Tanga mjini...

Ulozi nje nje hapo, hata kwa kusikia tu jina la mtaa...
 
Kuna sehemu inaitwa kibera au Kibra, kule watu wanaishi Kama wanyama. Kuna jamaa aliwahi kunipitisha pale nilihuzunika Sana.
 
Back
Top Bottom