Kuna mitaa imelaaniwa

Kuna mitaa imelaaniwa

Swala la MAFANIKIO linahitaji Mambo Mengi Sana na sio laana au baraka

Mitaa ya Uswahilini ni ngumu kufanikiwa au kufika hatua kubwa ya MAFANIKIO kutokana na uhaba Mdogo wa MAARIFA na kutokuwa na ile inaitwa money literacy.

Hiyo hiyo Sehemu unayoona huwezi ndo WATU wengine wamefanikiwa.
 
Ulishawahi kukuta mtaa fulani hali ya maisha ya kaya zoote hapo choka mbaya? Mtaa wote umejaa makahaba! Mtaa umejaa walevi! Watoto au kizazi ndani ya huo mtaa hawamalizi darasa la saba au kidato cha nne! Ndani ya huo mtaa hakuna mtumishi wa umma mwenye mshahara unaoeleweka! Hakuna familia yenye gari na kama lipo ni mkweche! Wanawake ni kupiga majungu na wanaume vijiwe vya kahawa na draft!.
Ndo nikagundua sio tu kuwepo kwa familia zilizolaaniwa, lakini pia kuna mitaa iliyolaaniwa! Kuna vijiji/kata zimelaaniwa! Kuna wilaya zimelaaniwa (kama wilaya ya kisarawe)! Kuna miji imelaaniwa miji mingi katika mikoa ya pwani, Tabora na kigoma! Unapokuwa unatafuta maisha fanya uchunguzi wa mitaa/kata/wilaya/miji unayoenda vinginevyo hutoboi! Mwisho wa siku lazima hali yako ya maisha iendane na wao! Nikagundua nyuma ya pazia kuna wachawi wanakaa katika malango ya njia kuratibu kila anayekuja na kuishi hapo na kumpiga tukio! Haya mambo magumu sana kuelewa!
Ni life style tu na mifumo hakuna Cha laana.Kisarawe inatoa mawaziri nchi hii toka uhuru itakuwaje ilaaniwe?
 
Umasikini na ujinga ni hatari sana kuanzia ngazi ya kaya, ukoo, mtaa, kijiji, kata, tarafa hadi taifa.
Kwa leo ni hayo tu
Tatizo letu ni kuhusianisha kila kitu na ushirikina. Inachekesha kuona kwamba nchi zilizoendelea hua zinaliona bara zima la Afrika ni kama limelaaniwa kwa jinsi lilivyo nyuma, wakati huo huo eti na sisi humu ndani tunanyoosheana vidole kwamba eneo fulani limelaaniwa..😆😆

Wakati kiuhalisia sisi wote ni giza tupu tofauti ni ndogo sanaa..
 
Uko sahihi,inabidi uzame sana kwenye maombi na toba ili uvunje hizo laana ili na wewe mwenyewe pia uweze kubaki salama...
Hizo sehemu ulizosema hazina maendeleo ndio Zina uzinzi, ukahaba, madawa, wizi, uchawi etc na hivyo siyo rahisi kupata maendeleo. Hivyo vitu na roho ya maendeleo ni maji na mafuta. Niambie mtu anayetumia madawa au mwasherati mwenye maendeleo. Refer wasanii wetu
 
Ulishawahi kukuta mtaa fulani hali ya maisha ya kaya zoote hapo choka mbaya? Mtaa wote umejaa makahaba! Mtaa umejaa walevi! Watoto au kizazi ndani ya huo mtaa hawamalizi darasa la saba au kidato cha nne! Ndani ya huo mtaa hakuna mtumishi wa umma mwenye mshahara unaoeleweka! Hakuna familia yenye gari na kama lipo ni mkweche! Wanawake ni kupiga majungu na wanaume vijiwe vya kahawa na draft!.
Ndo nikagundua sio tu kuwepo kwa familia zilizolaaniwa, lakini pia kuna mitaa iliyolaaniwa! Kuna vijiji/kata zimelaaniwa! Kuna wilaya zimelaaniwa (kama wilaya ya kisarawe)! Kuna miji imelaaniwa miji mingi katika mikoa ya pwani, Tabora na kigoma! Unapokuwa unatafuta maisha fanya uchunguzi wa mitaa/kata/wilaya/miji unayoenda vinginevyo hutoboi! Mwisho wa siku lazima hali yako ya maisha iendane na wao! Nikagundua nyuma ya pazia kuna wachawi wanakaa katika malango ya njia kuratibu kila anayekuja na kuishi hapo na kumpiga tukio! Haya mambo magumu sana kuelewa!

NAUNGA MKONO HOJA!
 
Back
Top Bottom