Kuna mitaa imelaaniwa

Kuna mitaa imelaaniwa

Ulishawahi kukuta mtaa fulani hali ya maisha ya kaya zoote hapo choka mbaya? Mtaa wote umejaa makahaba! Mtaa umejaa walevi! Watoto au kizazi ndani ya huo mtaa hawamalizi darasa la saba au kidato cha nne!

Ndani ya huo mtaa hakuna mtumishi wa umma mwenye mshahara unaoeleweka! Hakuna familia yenye gari na kama lipo ni mkweche! Wanawake ni kupiga majungu na wanaume vijiwe vya kahawa na draft!.

Ndo nikagundua sio tu kuwepo kwa familia zilizolaaniwa, lakini pia kuna mitaa iliyolaaniwa! Kuna vijiji/kata zimelaaniwa! Kuna wilaya zimelaaniwa (kama wilaya ya kisarawe)!

Kuna miji imelaaniwa miji mingi katika mikoa ya pwani, Tabora na kigoma! Unapokuwa unatafuta maisha fanya uchunguzi wa mitaa/kata/wilaya/miji unayoenda vinginevyo hutoboi! Mwisho wa siku lazima hali yako ya maisha iendane na wao!

Nikagundua nyuma ya pazia kuna wachawi wanakaa katika malango ya njia kuratibu kila anayekuja na kuishi hapo na kumpiga tukio! Haya mambo magumu sana kuelewa!
Kuna wakati eneo kama waanzilishi wa mitaa walikuwa na tabia za kichawi na wizi kuna uwezekano mkubwa sana mtaa huo kutoendelea na kuwa na crime rate kubwa.

Siyo mitaa tu ipo miji pia iliyoanzishwa na wahalifu au yalikuwa makazi ya wahalifu wengi miji hiyo lazima iwe na hali duni kwa sababu hakuna mtu mwenye pesa zake atataka kuishi mtaa huo.
 
Leo kisalawe ni wilaya ya viwanda wachina kama wote watu watu wanatoka dar wanahamia kisalawa mijengo ya nguvu huyu jamaa kisalawa hakujui pengine analake jambo tu
Kisalawe na Kisalawa ndio wapi mkuu
 
Nchi nyingi zinaongoza kwa ukahaba na ushoga tena zinaongoza kwa maendeleo ya kila kitu tatizo lako ukiona mtu tajiri unadhi kabalikiwa na ukimuona masikini unamuona kalaniwa basi kuanzia baba babu zako mpaka wewe mwenyewe mnayo laana
Mbona kama unaandika kwa hasira mkuu? Wewe naona unalenga tu utajiri wa kipato, haya unajua Mimi nina kipato gani?
 
Ulishawahi kukuta mtaa fulani hali ya maisha ya kaya zoote hapo choka mbaya? Mtaa wote umejaa makahaba! Mtaa umejaa walevi! Watoto au kizazi ndani ya huo mtaa hawamalizi darasa la saba au kidato cha nne!

Ndani ya huo mtaa hakuna mtumishi wa umma mwenye mshahara unaoeleweka! Hakuna familia yenye gari na kama lipo ni mkweche! Wanawake ni kupiga majungu na wanaume vijiwe vya kahawa na draft!.

Ndo nikagundua sio tu kuwepo kwa familia zilizolaaniwa, lakini pia kuna mitaa iliyolaaniwa! Kuna vijiji/kata zimelaaniwa! Kuna wilaya zimelaaniwa (kama wilaya ya kisarawe)!

Kuna miji imelaaniwa miji mingi katika mikoa ya pwani, Tabora na kigoma! Unapokuwa unatafuta maisha fanya uchunguzi wa mitaa/kata/wilaya/miji unayoenda vinginevyo hutoboi! Mwisho wa siku lazima hali yako ya maisha iendane na wao!

Nikagundua nyuma ya pazia kuna wachawi wanakaa katika malango ya njia kuratibu kila anayekuja na kuishi hapo na kumpiga tukio! Haya mambo magumu sana kuelewa!
Maswa nasikia kuna Mtaa unaitwa "Mtaa wa dhambi"
 
Hizo Imani tu ukizipa Nguvu na zenyewe zinakupa Nguvu

Mtu kama haunywi Pombe ,bangi wala sigara na unajitenga na uasherati Uzinzi hata Kama unaendesha bodaboda tu lazima ufanikiwe hatua kubwa SANA.

Watu wanwekeza katika Uzinzi ,pombe Umalaya then wakikwama wanasema laana au kurogwaa .

Hii mitaa ya Uswahilini Mimi ndo naishi wapo wapemba wanamaisha. Safi Sana na watu waswahili wapo vizuri ila Hawa wanawake na vijana wanaoendekeza tabia mbaya ndo Maisha yanawatoa mchezoni Mapema.
Ulevi, uzinzi, umalaya, uasherati, uvivu n.k. ni malango ya laana! Laana lazima zipitie pale na kujitokeza katika mikosi, nuksi, mabalaa, majanga, kukataliwa, madeni n.k na baada ya hapo magonjwa, kesi, jera na kifo. Kizazi kinachobaki kinakuw ni kizazi cha mitaani (homeless)
 
Keko magurumbasi kule bondeni , maisha ya kule yanafurahisha usione ajabu mtu kubisha hodi abaomba umsaidie kijiko kimoja cha sukari .

Wao wanakula ugali na kichwa cha kuku walichonunua kwa bibi mzuri .

Wanachuo wa chuo cha DUCE wanapigwa vizinga na wanakeko mpaka boom haliwatoshi lakini finally umbea maeneo hayo ni tabu tupu hata ulete mchuchu usiku wa manane asubuhi taarifa wanazo .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Umasini sio laana wewe hapo ulipo ni masikini ndio kusema umelaniwa?nusu ya watanzania ni masikini robo fukara matajiri awafiki hata robo ninacho kiona kwako ujui masikini ni mtu wa aina gani hata tajiri ujui wala laana ujui maana yake
25000q mimi sio masikini! Niko vizuri na ninaweza kukuajiri! Nina watu wanaendesha familia zao kupitia ajira zangu! Huna adabu! 25000q
 
Back
Top Bottom