Kuna mitaa zaidi ya 20 duniani inakwenda kwa jina la Patrice LUMUMBA, Nadhani Distinction iwepo kabla ya kutoa jina

Kuna mitaa zaidi ya 20 duniani inakwenda kwa jina la Patrice LUMUMBA, Nadhani Distinction iwepo kabla ya kutoa jina

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
Natambua majina ya maeneo, mitaa, Taasisi au uwekezaji mara nyingine huja yenyewe kutokana na matukio au waanzilishi na mambo mengine mengi hapa nazungumzia haya ya kupewa sio hayo ambayo automatically yanakuwa hivyo .

Duniani kote kuna mitaa na maeneo zaidi ya 20 inayokwenda kwa jina LUMUMBA ,hii ni kutokana na upigania haki , misimamo yake na utendaji kazi wake mkubwa .

Nchi kama Serbia, Ukraine, Nigeria, Morocco, Ghana , Egypt, Iran, South Africa, Morocco, Uganda, Burundi, Kenya, Ethiopia, Haiti, Zambia, Zimbabwe, Germany, Iran, Mozambique na Tanzania ukipita utakutana na jina lake .

Hata Belgium tunaohisi walihusika na kuondoka kwake lipo

China na Russia waliandamana baada ya kifo Chake 17/1/1961 ,na kuna chuo Russia kilipewa jina lake .

Historia ya Lumumba ndio ilifanya wanaharakati kutambua Russia ndiye Rafiki wa kweli wa Afrika .​
images (28).jpegimages (29).jpeg

Nacho taka kusema hapa hizi mali na uwekezaji wa Nchi ni pesa za wananchi hivyo kitu cha kwanza kabla ya kutoa jina tajiulize aliiifanyia au ameifanyia nini nchi au Taasisi husika mpaka ipewe jina hilo ?

Au hilo jina linatukumbusha nini au lina maana gani katika jamii ? hasa kwa mali au uwekezaji wa umma .


Zamani ulikuwa ukipita mitaa ya sokoine ,Samora , Nyerere,Lumumba ,Bibi titi, Karume ...etc hata ukipewa history ya hilo jina kuna kitu unapata .

Kuwa Mwenyekiti wa mtaa ,diwani ,mbunge, lecturer, Waziri au kiongozi au mtu maarufu yoyote haitoshi lakini kikubwa umeifanya nini jamii au kuna utofauti gani na wengine .



 
Acha roho mbaya
Mashujaa wa bara la Africa walioweka juhudi zao kulitetea mmoja wapo ni Lumumba, Kwame Nkuruma, Samora Masheli, Julius Nyerere,

Au unakataa?
Nadhani hujamuelewa huyu jamaa, anachojaribu kuelezea ni hawa viongozi wa miaka ya hivi karibuni kutaka majina yao yaishi milele wakiwa hawajafanya la maana kama walivyofanya hao akina LUMUMBA, NYERERE n.k
 
Kwa Sasa TZ wanatoa majina ya ajabuajabu sana ambayo hayana mchango wowote Kwa Nchi zaidi ya kutumia Kodi za wananchi.
 
Back
Top Bottom