Hii ni taarifa iliyovujishwa na baadhi ya wazalendo waliochoshwa na uonevu wa kishamba , kwamba viongozi hao wa Upinzani wakamatwe ili kuwatisha na kuwavunja moyo , wanyimwe dhamana angalau kwa wiki moja au mbili ili kuwakomoa .
Hii ni amri iliyosambazwa nchi nzima , huku ikidaiwa kuwa chanzo chake ni kufeli kwa Mkakati wa kuwashawishi masikini kukikimbilia kitambulisho cha wamachinga ambacho sasa kimepewa jina jipya la KODI YA KICHWA , inaaminika kwamba kufeli kwa mkakati huo wa kukamua kila masikini Tsh 20,000 kumesababishwa na wanasiasa wa Upinzani wanaonekana kutumia kila nafasi ndogo wanayopata , ikiwemo mitandao ya kijamii kuwaamsha wananchi na kuwaelimisha kuhusu haki zao.
Tutaendelea kuwahabarisha kila ovu wanalopanga kwa kadri wasamalia wema waliojaa uzalendo watakavyokuwa wanavujisha habari zao.
Naomba kuwasilisha