Tetesi: Kuna mkakati wa kukamata angalau kiongozi mmoja wa upinzani kila wiki , imeagizwa wanyimwe dhamana

Tetesi: Kuna mkakati wa kukamata angalau kiongozi mmoja wa upinzani kila wiki , imeagizwa wanyimwe dhamana

Nadhani lengo ni kuzima issue ya vitambulisho vya machinga (Kodi ya Umasikini - Poverty Levy) na issue ya kushuka kwa thamani ya shilingi
 
Wakamatwe tu, hawana jipya zaidi ya kueneza chuki na uvunjifu wa Amani. Fyeka wote ndani . Nchi hii ni yetu sote.
 
Ok, Lets say wakafunga na kuua wote, je utadhani upinzani utaisha? Tutajenga upinzani wa kimya kimya ambao utakua mbaya sana, watu watalipiza visasi kimya kimya. Sidhani kama CCM wangependa watufikishe huko, siamini kabisa. Siamini kama CCM hakuna mtu mwenye uwezo wa kukemea jambo hili, siamini kabisa.
.
tapatalk_1550015282592.jpeg
 
Hamna cha sadist wala nini, unaleta emotions kwenye siasa! Wewe hujui kuwa hao wanaokamatwa pia ni turufu kwao kisiasa na inaendana na hoja za mzee wa harambee.
Acha hoja za kitoto kwenye masuala muhimu. Hapa hatupo kupunguza stress, tupo kujadiliana mambo muhimu ya kijamii.
 
Tumeshakuzoe wewe bwege na habari zako zisizo na miguu wala kichwa!
Mahala popote, ISIPOKUWA KWA WATUKANAJI PEKEE, matusi ni alama ya walioshiwa HOJA....

Like aliyokupa huyo uliyemtukana, jifikirie mara mbilimbili
 
Kamata kamata yaendelea nchi nzima , na sasa imetua Makambako !
 
Acha hoja za kitoto kwenye masuala muhimu. Hapa hatupo kupunguza stress, tupo kujadiliana mambo muhimu ya kijamii.
Siku nyingine usome vizuri comment za wenzako sio kuwa occupied na mawazo potofu kuwa hapa ni ukumbi wa agenda za kundi fulani.Nilisema, “ Hapa tuko kubadilishana mawazo, na ikibidi kuondoa stress....”
 
unatafsiri vibaya sana azimio la Zanzibar , nadhani unayo masilahi kwenye hii kamata kamata , bali unachotakiwa kufahamu ni kwamba ANAYEKULA NYAMA YA MTU HAACHI , akimaliza hawa chadema unayefuatia ni wewe , mwangalie Nape kama somo

Lile Azimio la Zanzibar liko wazi kabisa. Kila mpinzani anayewekwa rumande au jela kwa kosa lolote lile atatangazwa kwa nchi za nje kuwa ni mfungwa wa kisiasa. Haihitaji tafsiri. Ili TZ ionekane ina wafungwa wa kisiasa lazima wapinzani wafanye mambo ya kuwekwa ndani. Na wameanza. Nina hakika wataendelea.
 
Je hata kwa akili ya kuazima hivi kweli unaamini viongozi wa Chadema akiwemo Mbowe anayesota gerezani ndio walimuua Akwilina ?

ccm inaagiza watu wakamatwe ipendavyo tu wala si kwa sababu ya azimio la Zanzibar au azimio lolote
 
Ok, Lets say wakafunga na kuua wote, je utadhani upinzani utaisha? Tutajenga upinzani wa kimya kimya ambao utakua mbaya sana, watu watalipiza visasi kimya kimya. Sidhani kama CCM wangependa watufikishe huko, siamini kabisa. Siamini kama CCM hakuna mtu mwenye uwezo wa kukemea jambo hili, siamini kabisa.

Acha kuamini kila neno linaloandikwa hapa. Yote haya ni kutafuta kiki. Utaanza vipi kukamatwa bila kutenda kosa? Assume kila kiongozi wa upinzan yupo bizeee na kazi binafsi ataanza vipi kukamatwa? Akiharib atakamatwa.
All in all ni siasa za kuchafuana tu. Hakuna kuvuja wala kutoboka.
 
Hii ni taarifa iliyovujishwa na baadhi ya wazalendo waliochoshwa na uonevu wa kishamba , kwamba viongozi hao wa Upinzani wakamatwe ili kuwatisha na kuwavunja moyo , wanyimwe dhamana angalau kwa wiki moja au mbili ili kuwakomoa .

Hii ni amri iliyosambazwa nchi nzima , huku ikidaiwa kuwa chanzo chake ni kufeli kwa Mkakati wa kuwashawishi masikini kukikimbilia kitambulisho cha wamachinga ambacho sasa kimepewa jina jipya la KODI YA KICHWA , inaaminika kwamba kufeli kwa mkakati huo wa kukamua kila masikini Tsh 20,000 kumesababishwa na wanasiasa wa Upinzani wanaonekana kutumia kila nafasi ndogo wanayopata , ikiwemo mitandao ya kijamii kuwaamsha wananchi na kuwaelimisha kuhusu haki zao.

Tutaendelea kuwahabarisha kila ovu wanalopanga kwa kadri wasamalia wema waliojaa uzalendo watakavyokuwa wanavujisha habari zao.

Naomba kuwasilisha
Inahusisha kuwateka?
Maana naona wimbi nalo limezidi kushika kasi,
Reference: Kule babati, mafinga etc.................
 
Je hata kwa akili ya kuazima hivi kweli unaamini viongozi wa Chadema akiwemo Mbowe anayesota gerezani ndio walimuua Akwilina ?

ccm inaagiza watu wakamatwe ipendavyo tu wala si kwa sababu ya azimio la Zanzibar au azimio lolote

Kwa nini mtu uazime akili? Kwa muda huu Mbowe yuko mahabusu kwa kosa la kukiuka masharti ya dhamana. Haijalishi ni kesi ya namna gani. Yeye alipewa masharti ya kuwa nje kwa dhamana na akaamua makusudi kuyakiuka. Sasa mahakama ifanye nini? Kuhusu kifo cha Akwinina hakuna ubishi kuwa kifo chake kilitokana na risasi iliyopigwa na askari polisi. Kwa nini ikapigwa hiyo risasi? Ilikuwa kuzuia maandamano ambayo kwa mtazamo wa polisi hayakuwa halali. Ndiyo kesi iliyopo mahakamani ikimhusisha Mbowe kuwa hayo maandamano ambayo hayakuwa halali aliratibu yeye. Mahakama inaweza kuamua kuwa yalikuwa halali au hayakuwa halali.
 
ukishakuwa na masilahi binafsi huwezi kujadili kwa uhuru
 
Back
Top Bottom