Kuna mkatoliki amewahi kujiuliza kwanini mapadre wanawafungisha ndoa ila wao mapadiri hawafungi ndoa?

Kuna mkatoliki amewahi kujiuliza kwanini mapadre wanawafungisha ndoa ila wao mapadiri hawafungi ndoa?

Mume wa mtu anaweza kuwa available 24/7 kama padri anavyotakiwa kuwa available muda wote? Mume wa mtu na baba wa familia akiambiwa sasahivi aende Sudan Kusini kupeleka Injili ataenda bila kujiuliza mara mbili na bila kuathiri afya ya akili na ustawi wa familia yake? Mume wa mtu anaweza kuamka saa kumi za alfajiri kila siku ili aweze kusalisha Misa ya kwanza saa kumi na moja alfajiri Kila siku bila kuathiri majukumu yake kama baba wa familia na mume wa mtu? Mume wa mtu akihitajika muda wowote kwenda kusoma nje ya nchi eg Italia kwa ajili ya Kanisa je ataweza kwenda ? Mume wa mtu tena kwenye mazingira ya Afrika na Bongo, endapo wakwe zake wana mahitaji, hatashawishika kuiba yale mamilioni ya sadaka za waumini ili asaidie ukweni? Mapadri wanahamishwa vituo vya kazi mara kwa mara, mume wa mtu na baba wa familia ataweza kuhama kituo cha kazi kila baada ya miaka 2 au 3 pasipo kusababisha usumbufu kwa familia?
Lakini wanapata muda wa kula watawa na kuharibu watoto
 
Tujitafakari,

Inawezekanaje mapadiri wawe sawa kuwaozesha waumini wenzao lakini wao hawaoi,hata hili waafrika hamlioni kuwa ni ujinga uliopitiliza na kama ni imani je siyo ujinga wa kutokuhoji?

Wazazi wao wasingeoana jea hao mapadiri wangezaliwa?

Niliuliza hilo sawali nikafukuzwa, nikahamia kwa walokole, Nako nikafukuzwa kutokana na tabia yangu ya unywa pombe nilijizoesha tangu nikiwa RC.

Huu ndio mwanzo wa mimi kuwa atheist . Sasa subabaishwi na yeyote wala chochote.
Nini chanzo cha watu kuishi na wanyama wa kufuga nyumbani bila kudhuriwa na wanyama pori kuishi pekeyao porini? Yani kipi kilichoumba na kuweka mipaka ya mazingira ya viumbe hivi kuelewana na kutoelewana kwa pamoja?

Ubinadamu ni kazi - the humanity is work.
 
Swali zuri sana! Mimi huwa najiuliza, je, bado Kuna mbuzi ng'ombe, kondoo au, punda ambao wako porini, yaani hawajawa domesticated?
 
Swali zuri sana! Mimi huwa najiuliza, je, bado Kuna mbuzi ng'ombe, kondoo au, punda ambao wako porini, yaani hawajawa domesticated?
Hatari sana mkuu, vitu vingine vinashangaza sana kama tulivyovuvikuta baada ya kuzaliwa duniani.

Mkuu hebu post uzi kupitia hili swali huenda Atheists kama wewe wakatupatia majibu mazuri.
 
Kwani wanalazimishwa?
Sasa mtu ameshatekwa tangu ubatizo(utotoni),komunio mbili,kipaimara n.k halafu ghafla awe na msimamo wa kukataa kufungishwa Ndoa?.

Mkuu jipe muda kisha tafakari kwa kina utabaini hii michezo ya wenye dini katika harakati za kuwafanya watu kuwa mateka wao wa kiroho!
 
Hayo ni mawazo su fikra zako tu.Kwani akibatizwa ndiyo akili hutoroka hadi ashindwe kufikiri na kuamua/kuchagua alitakalo?Sasa,kwa taarifa yako,walokole wengi wa kileo ndiyo walikuwa wakatoliki.
 
Hayo ni mawazo su fikra zako tu.Kwani akibatizwa ndiyo akili hutoroka hadi ashindwe kufikiri na kuamua/kuchagua alitakalo?Sasa,kwa taarifa yako,walokole wengi wa kileo ndiyo walikuwa wakatoliki.
Wanaotoka ni wachache kuliko wanaobaki.Je,unadhani hao waliobaki madudu ya huko Ukatolikini hawayaoni?. Kama wanayaona ni nini kinawafanya wasiachane nayo?
 
Sasa mtu ameshatekwa tangu ubatizo(utotoni),komunio mbili,kipaimara n.k halafu ghafla awe na msimamo wa kukataa kufungishwa Ndoa?.

Mkuu jipe muda kisha tafakari kwa kina utabaini hii michezo ya wenye dini katika harakati za kuwafanya watu kuwa mateka wao wa kiroho!
Kila jambo kama sio la lazima kabisa kama kula, kupumua huwa linamshangaza mtu mwingine asiyelifuata.

Hata wewe ni mateka kwa watoto wako kuna mtu anakuona punguwani kuwa nao.
 
Kila jambo kama sio la lazima kabisa kama kula, kupumua huwa linamshangaza mtu mwingine asiyelifuata.

Hata wewe ni mateka kwa watoto wako kuna mtu anakuona punguwani kuwa nao.
Uzuri ni kwamba Ubaya au Uzuri wa jambo lolote hujieleza kupitia outcome yake!
 
Umeyaita "madudu" na sijui umemaanisha nini na kiasi gani!Tuoneshe walio wasafi wasio na "madudu"!
Nimeyaita madudu kwa sababu kadiri nilivyokuwa nayashika ndivyo nilivyozidi kuwa mbali na Mungu muumba wangu. In fact ni mradi wa wajanja wachache wakitumia jina la Mungu vibaya!

Kwa nyakati za sasa kukuta mahali hakuna madudu kabisa kabisa ni ngumu

Jambo la msingi ni mtu yeye kama yeye kuwa ndani ya Kristo Yesu ili Kristo awe taa na mwanga wa Njia zake zote!. Bwana Yesu ndiye mwenye uwezo wa kutusaidia kuviona vilivyojificha!

YOHANA 8
12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
 
Outcome yake ni ipi mbaya? Wewe unahisi unawazidi nini hao unawaona hawana akili?
Ukitaka kuujua Uzuri au Ubaya wa Jambo lolote usihadaike na promo. Chunguza impact(outcome) yake!.

Bahati nzuri huwa sifanyi mambo ili kushindana wala kutafuta umwamba bali nafanya kwa sababu ni wajibu wangu muhimu!
 
Kuna mkatoliki amewahi kujiuliza kwanini mapadre wanawafungisha ndoa ila wao mapadiri hawafungi ndoa?
Hilo halihitaji kujiuliza, lipo kwenye neno na mafundisho ya imani.

Mt 19:9-10
Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa. 11Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.

1Wakorinto 7: 8-10
Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo. Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa. Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;
 
Back
Top Bottom