Kuna mkatoliki amewahi kujiuliza kwanini mapadre wanawafungisha ndoa ila wao mapadiri hawafungi ndoa?

Tujitafakari,

Inawezekanaje mapadiri wawe sawa kuwaozesha waumini wenzao lakini wao hawaoi,hata hili waafrika hamlioni kuwa ni ujinga uliopitiliza na kama ni imani je siyo ujinga wa kutokuhoji?

Wazazi wao wasingeoana jea hao mapadiri wangezaliwa?
Neno la Mungu halihojiwi mkuu. Na hilo ndilo neno la Bwana.
 
Neno la Mungu halihojiwi mkuu. Na hilo ndilo neno la Bwana.

Ukisema "Neno la Mungu halihojiwi," nakubaliana.

Lakini swali ni hili: Je, unachokitaja ni kweli Neno la Mungu, au ni tafsiri yako ya Neno la Mungu?

Biblia yenyewe inasema:

"Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike; walilipokea lile neno kwa utayari wa moyo, wakayachunguza Maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo."
(Matendo 17:11)
Kama Neno la Mungu halikupaswa kuchunguzwa, kwa nini Waberoya walimsikiliza hata Paulo kisha wakachunguza Maandiko kuona kama aliyosema yalikuwa kweli?

Na mtume Yohana anaandika:

"Wapenzi, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na Mungu."
(1 Yohana 4:1)
Hata Yesu alisema:

"Mwayachunguza Maandiko..."
(Yohana 5:39)
Kwa hiyo, si Neno la Mungu linalohojiwa; tafsiri ya mwanadamu ndiyo inayopimwa kwa Neno la Mungu.

Nimeuliza swali rahisi sana la kibiblia:

Ni wapi Yesu alisema: "Padre asioe"?

Ukileta aya hiyo nitakubali. Lakini ukisema "hili ndilo neno la Bwana" bila kuonyesha maandiko, basi huo si ushahidi wa kibiblia, bali ni madai tu.

Biblia inatuagiza tuthibitishe mambo yote:

"Jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema."
(1 Wathesalonike 5:21)
Kwa hiyo, kuomba ushahidi wa maandiko si kulikataa Neno la Mungu; ni kulitii Neno la Mungu.
 
Mkuu haya yote uliyouliza hapa yanafanywa na maaskofu wa makanisa mengine, ambao wameoa au kuolewa, na hawajawahi kupinga. Pia waume za watu wenye familia ambao ni wachungaji na wainjilisti wa makanisa mengine pia wanahama. Katika umri wako hujawahi kushuhudia mfanyakazi anahamishwa kutoka Mwanza kwenda Songea anaiacha famili yake huko Mwanza na anapiga kazi vizuri tu bila wasiwasi? Unawajua TAMISEMI kweli mkuu?
 
 
Mkuu naona umeuliza swali na kujijibu mwenyewe. Hata mimi nawashangaa sana wakatoliki kwa kuwazuia mapadre kuoa na kupelekea mapadre kuwageuza masista kuwa wake zao. Nimewahi kumshuhudia rafiki yangu mmoja aki-DATE na sista hadi akamjaza mimba. Kiu yangu ni kuona masista wanaolewa na mapadre wanaoa ili kuepuka kuwatia hawa watu majaribuni.
 
Kwa nini wawe wakwe, hawezi kuiba kwa ajili ya ndugu zake wa damu?
 
Mkuu naona unajibu hoja kwa kutumia maneno uliyokaririshwa. Ungekuwa na uwezo wa kutathmini mambo hata kidogo tu, ungegundua kwamba kanisa katoliki limepotoka sana kwa kutowaruhusu mapadre kuoa na masista kuolewa. Unyumbu wa waumini ndio unawafanya mshindwe kuhoji mambo. Kwanza unapaswa kuelewa kwamba agizo la mapadre kutokuoa ni la kibinadamu, sio la kiMungu. Ni kama ilivyo sikukuu ya krismasi. Hii ni sikukuu ya kipagani lakini wakatoliki mnavyoishadadia utadhani ni agizo kutoka kwa Mungu.
 
 

Ahsante sana Mkuu , Hata mimi nilishuhudia sister akiwa amepewa mimba na Padri huku Wete Pemba , miaka ya 1970s . Baadaye nilisikia yule Padri alihamishiwa Biharamulo
 
Haya ni mawazonyako kulingana na uelewa na iman yako au ni uhalisia?
 
Hili la kanisa katoliki kwamba wanajua Biblia kuliko madhehebu mengine sina uhakika, japo sio hoja. Hoja ni kama wanafundisha na kufuata inavyopaswa kilichoandikwa ndani ya Biblia.

Hakuna mahali Yesu amefundisha mitume wake wawaache wake zao kwa ajili ya kumtumikia Mungu, utume wao ni kazi kama kazi zingine wanaweza kumtumikia Mungu huku wakiwa na wake zao. Mfano Yesu kuna wakati alienda kumponya mama mkwe wa Petro MARKO 1:29-30.

Hakuna mahali Mungu ameagiza watumishi wake wasioe, kuoa au kutokuoa ni takwa la mtu binafsi. Kuoa kunaweza kuwa na advantage kwenye utumishi kama ambavyo kutokuoa kunaweza kuwa disadvantage kwenye utumishi. Kama ukipata muda utasoma vizuri 1 WAKORINTHO 7 yote.

Kama ingekuwa ni maagizo watumishi wa Mungu wasioe basi kusingekuwa na huu mstari kwenye Biblia.
1 TIMOTHEO 3:2 Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;

Halafu kuna utofauti wa huduma na karama za Mungu. Padre ni huduma ya kichungaji ambayo mtu anakuwa stationary kwenye location Fulani, Utume au umisheni is a non stationary gift. Huwezi kufananisha kazi ya Padre na kazi za mitume
 
Ahsante sana Mkuu , Hata mimi nilishuhudia sister akiwa amepewa mimba na Padri huku Wete Pemba , miaka ya 1970s . Baadaye nilisikia yule Padri alihamishiwa Biharamulo
Hawa jamaa ni wanafiq sana. Wanafahamu fika hawawezi kuvumilia kukaa bila kut0mb@ au kut0mbw@ lakini wanajitoa ufahamu huku wakiendelea kudinyana kisirisiri.
 
Tujitafakari,

Inawezekanaje mapadiri wawe sawa kuwaozesha waumini wenzao lakini wao hawaoi,hata hili waafrika hamlioni kuwa ni ujinga uliopitiliza na kama ni imani je siyo ujinga wa kutokuhoji?

Wazazi wao wasingeoana jea hao mapadiri wangezaliwa?
Hilo mbona ni dogo sana kati ya maswali ya msingi kuyauliza kwenye theolojia.

Mitume kina Paulo, Peter na wengine walipewa mamlaka ya kufungisha ndoa. Lakini wao hawakuoa ili kuutumikia kisawasawa utume wao.

RC walirithi na kuendeleza hiyo. Upadre ni wito ndio maana sio kila anayesomea huko anafanikisha, na sio kila anayetunukiwa anafanikiwa kudumu milele. Wao kufungisha ndoa ni kutekeleza majukum yao waliyopewa, kutooa ni wito ili wabaki katika usafi wa kiroho.

Sijaona kama Yesu alioa ila alifungisha ndoa
 
Kwangu mimi huo ni Ubinafsi mkubwa,Uvivu wa kufikiri na kupelekea kuwa na hitimisho la kuchagua Maisha ya Ukwepaji wa Majukumu halali ya Kibinadamu na Utu.Kwa kujificha kwenye vazi la kanzu Nyeupe.

Mungu hawezi kubariki huo ujing..ndiyo maana wengi huko wanakuwa ni wahanga wa Magonjwa ya hatari kama Kisukari,Presha,UKIMWI,Vifo vya Ujanani na Mapema,Ajali za vyombo vya moto na hata kutekwa na ma CCM yawapoteze.

Yote haya ni Mungu wa Kweli alishawapatiliza, wawe wanatoweka mapema kwenye uso wa Dunia hii...Maana anawaona kabisa ni Useless ever..
 
Wakatoriki sidhani kama walisema ni amri ya Mungu kuwa watumishi wasioe. Bali ni utaratibu wa kanisa tu kama ambavyo makanisa mengine yana taratibu zake.

Mtume Paulo 1 Wakorinto 7:25... alisema "sina amri ya Mungu bali ni shauri langu" akishauri kwamba ukiona ni vyema bora husioe ili upate kutumikia Mungu kisawasawa kama yeye, na akasema ukioa pia hakuna shida ila husifanye uasherati.

RC wao wameweka huo utaratibu kupitia tafsiri hiyo kutokana na kwamba waliona kuchanganya masuala ya ndoa na utume yanaweza kuleta shida pengine.

RC hawalazimishi kila RC awe padre, ila wao wameamua kutafsiri hivyo tu. Wao walienda na ushauri wa mtume Paulo.

Mathauo 19:12 inasema pia kuna matowashi waliozaliwa hivyo tangu tumboni kwa kusudi la kumtumikia bwana kisawasawa, na wapo walioamua wao wenyewe.
 
Una uhakika kwamba Mungu ndio anawafanyia hayo yote, au ni imani inayochagizwa na chuki na hasira binafsi juu yao ?
 
Una uhakika kwamba Mungu ndio anawafanyia hayo yote, au ni imani inayochagizwa na chuki na hasira binafsi juu yao ?
Ni nani sasa Mkuu!!?
Maana machache niliyoyataja hapo Makao Makuu ni Maparokiani na Uaskofuni huko..

Hata COVID-19.tena wimbi la kwanza iliwavuruga sana hawa watu..Ndani na Nje ya Nchi hii!?
Why!!?Na wala sina chuki wala udini dhidi yao..maana hawana Maisha yao hayana faida wala hasara kwangu.
 
Wanaathirika kama wanadamu wengine tu. Maradhi, magonjwa, kifo nk ni kwa mwanadamu yeyote tu bila kujalisha nafasi yako, hata wewe yanaweza kukupata tu 🙄
 
Wanaathirika kama wanadamu wengine tu. Maradhi, magonjwa, kifo nk ni kwa mwanadamu yeyote tu bila kujalisha nafasi yako, hata wewe yanaweza kukupata tu 🙄
Kuugua natambua..Ajabu wao maradhi yao ni ya mfanano mkubwa..
Presha,Kisukari ..tena katika umri mdogo sana.
Kwanza hakuna Askofu Mkatoliki asiye kuwa na Presha mfano ndani ya Tanzania hii..Big No.tutabishana milele.
Na kurogwa wanarogeka sana na yapo matukio ya Mapadri kulazwa nje Uchi kimazingara mengi tu...!!
Kwa wenzao Walokole utasikia Mchawi ameanguka na ungo Kanisani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…