Kuna mkatoliki amewahi kujiuliza kwanini mapadre wanawafungisha ndoa ila wao mapadiri hawafungi ndoa?

Sio aneyeenda kwenye upadre ana wito wa upadre. Sio ukiwa Padre umeondolewa utu.

Hata maprdre bado wana hisia, wana utashi kama kawaida. RC wanaweza kukosea tu labda pale ambapo wanachukua mtu ambaye sio sahihi jambo ambalo nalo lina ugumu wake pia.

Kigezo chakuwa padre kipo clear, mtu anajiunga akijua hatooa, hatozaa. Kinyuma na hapo anakuwa amekiuka taratibu za kanisa.

Hakuna anayeshikiwa mkuki kulazimishwa awe prdre au sista
 
Dini ni imani, hakuna anayekushikia kiboko kuamini hiyo imani, muda unaotumia kukosoa ungejiondoa kwenye hiyo imani na kufata unayoona inafaa ungekuwa umefanya jambo jema.
 
Ukiwa mkatoliki huwez jiuliza swali kama hilo kwa sababu mafundisho yapo wale wanaish kama Yesu hakuoa mzee
 
Tujitafakari,

Inawezekanaje mapadiri wawe sawa kuwaozesha waumini wenzao lakini wao hawaoi,hata hili waafrika hamlioni kuwa ni ujinga uliopitiliza na kama ni imani je siyo ujinga wa kutokuhoji?

Wazazi wao wasingeoana jea hao mapadiri wangezaliwa?
Shida ni kuwafungisha ndoa wengine halafu wao hawaoi au shida ni nini hasa?

Pili, unavyosema "ujinga wa waafrika kutohoji" unamaanisha mapadri wasio waafrika wao wanaoa?

Kwa akili yako, umejaribu hata kutafakari upadri umeanza karne ya ngapi?

Kwa akili yako umejaribu kuwaza kwamba hapa duniani jambo la msingi ni kuoa tu?

Kwa akili yako umejaribu kuwaza kwamba ndoa ni utume na si lazima kila mtu atumikie utume huo?
 
kwenye kuelewa atakua kaelewa
 
ushaduona wap askofu kaoa viongoz wa kanisa katoliki hawaoi kuanzia papa askofu na padri anayeoa katksta pekee hao wengne cjui mashehe wachungaji tunatakiwa kuwauliza kwanini wanaoa
 
Dini ni imani, hakuna anayekushikia kiboko kuamini hiyo imani, muda unaotumia kukosoa ungejiondoa kwenye hiyo imani na kufata unayoona inafaa ungekuwa umefanya jambo jema.
Kwanini wakatoliki mmeshikilia hiyo imani ya ajabu kwa muda mrefu bila kuhoji mkuu? Mmekuwa kama nyumbu?
 
Kuhoji kuhusu nini?

Kama ni hilo swala la mapadre kutooa, halina msingi. Kuna mambo mengi ya kuangaika nayo ila sio hilo.
Kwanini wakatoliki mmeshikilia hiyo imani ya ajabu kwa muda mrefu bila kuhoji mkuu? Mmekuwa kama nyumbu?
 
Y
Tujitafakari,

Inawezekanaje mapadiri wawe sawa kuwaozesha waumini wenzao lakini wao hawaoi,hata hili waafrika hamlioni kuwa ni ujinga uliopitiliza na kama ni imani je siyo ujinga wa kutokuhoji?

Wazazi wao wasingeoana jea hao mapadiri wangezaliwa?
Yesu hakuoa Mkuu, ila alizaliwa
 
Tujitafakari,

Inawezekanaje mapadiri wawe sawa kuwaozesha waumini wenzao lakini wao hawaoi,hata hili waafrika hamlioni kuwa ni ujinga uliopitiliza na kama ni imani je siyo ujinga wa kutokuhoji?

Wazazi wao wasingeoana jea hao mapadiri wangezaliwa?
Sasa mapadre kutooa kumeharibu kitu gani? Mbona bado watu wanazaa na dunia imejaa?
 
Mkuu,taja Kanisa lolote hapa Bongo ambalo kiongozi wake ana ratiba zifuatazo na zote anatakiwa atimize yeye :
1. Kwenda kusalisha misa ya alfajiri Kila siku.
2. Kwenda Sudan Kusini kila mwaka
3. Kwenda kusoma pale anapohitajika
4. Kutoa mpako wa wagonjwa pale anapohitajika muda wowote hata iwe usiku wa manane.
Taja Kanisa ambalo viongozi wake wanasoma kwa miaka mingi kama viongozi wa Kanisa la RC, taja Kanisa ambalo maaskofu wake wote wana PhD kama maaskofu wa RC. Nitajie Kanisa moja tu.
Halafu hao watumishi / wafanyakazi wanaohama, je familia zao zinakuwa sawa kisaikolojia? Hilo ndo swali la msingi. Baba anaweza kuwa mbali na akapiga kazi, vipi je hii familia anayoiacha huku nyuma? mke na watoto wanafurahi baba yao kuwa mbali? . Hata humu jukwaani kumejaa nyuzi wafanyakazi wanaofanya kazi mbali na wenza wao wanavyolalamika hiyo hali inavyowakera na kuwaumiza kisaikolojia. Huwezi kuwa mbali na mke/ watoto wako mara kwa mara halafu familia yako isiathirike na Kanisa halitaki familia iathirike kisa baba anatakiwa aende kuhudumia waumini Kanisani,familia zikiwa mbovu na Kanisa litadondoka maana familia ndo Kanisa la Kwanza.
 
Namhusisha vipi na jambo ambalo hakulisema ilihali kaandika hapo juu kwamba kutoa mafundisho ya ndoa ilihali hujaishi maisha ya ndoa ni unafiki ??πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚. Usipunguze ukali wa maneno ya mtu bila ruhusa yake.

Halafu kuhusu amri, hakuna mahali Paulo amelazimisha, alipendekeza tu watu wawe kama yeye ( kwa atakayeweza) na mapadri wamefata hilo pendekezo kwa hiari yao, hawashikiwi bunduki kwamba wasioe wanaamua wenyewe wasioe ili wajitoe kikamilifu kutumikia Kanisa. Kama unataka kuoa na ukawa kiongozi Kanisani unaweza kuwa Katekista, unaweza kuwa mwenyekiti wa Parokia,etc. Nafasi za kutumika Kanisani huku ukiwa umeoa/ umeolewa bado zipo. Hakuna mtu anazuia Padri asioe,ni mtu anaamua kutooa ili awe Padri, akijiskia ameshindwa hayo maisha ya kutooa anarudi uraiani kuoa, mfano Dr Wilbroad Slaa, alivyoamua kuacha Upadri na kuoa kwani alilazimishwa aendelee kuishi bila mke? ,watu wanaamua kwa hiari yao.
Mimi nimeolewa kwa hiari yangu, lakini ningeamua kutokuolewa pia isingekuwa dhambi . Mapadri wameamua kutooa watumikie Kanisa kama mimi nilivyoamua kuolewa ili nitumikie familia yangu. Uamuzi wa mtu kama sio dhambi una tatizo? Au Biblia yako inafundisha kutooa/ kutoolewa ni dhambi?
Lastly , Yesu hakutamka neno Padri kwenye mafundisho yake labda kama wewe Biblia yako ina neno Padri, kwahiyo hilo neno " "atakayekuwa Padri asifunge ndoa" halipo kwenye Biblia. Sema neno lingine nikutafutie.
 


Umebadilisha hoja bila kutambua.

Mwanzoni ulijaribu kuonyesha kwamba kutooa kwa mapadri ni jambo la kibiblia. Sasa unakiri kuwa ni uamuzi wa hiari wa Kanisa, si amri ya Yesu wala ya Paulo. Hapo tayari umethibitisha hoja yangu.

Hakuna ninaposema kuwa kutooa ni dhambi. Biblia haifundishi hivyo, na hata mimi sijasema hivyo.

Hoja ni hii:

Je, Mungu aliweka sharti kwamba mtu akitaka kuwa kiongozi wa Kanisa lazima asioe?

Mpaka sasa hujaleta aya hata moja.

Badala yake, Paulo anasema kiongozi wa Kanisa awe "mume wa mke mmoja" (1 Timotheo 3:2; Tito 1:6). Kama kutooa ndiyo ilikuwa sharti la utumishi, kwa nini Paulo hakusema: "Askofu asiwe na mke"?

Unasema mapadri wanaamua kwa hiari yao. Sawa. Lakini je, mwanaume Mkatoliki aliyeoa anaweza baadaye kupewa daraja la upadre wa kawaida katika Kanisa la Kilatini? Jibu ni hapana, kwa sababu sheria ya Kanisa inazuia. Hivyo si suala la hiari pekee, bali kuna sharti la kikanisa.

Kuhusu mfano wa Dk. Wilbroad Slaa, huo haujibu hoja. Kwamba mtu anaweza kuacha upadre na kuoa hakubadilishi ukweli kwamba akiwa bado ni padre haruhusiwi kuoa. Hilo ndilo swali.

Halafu unasema Yesu hakutaja neno "Padri". Hilo ndilo nilikuwa nakusisitizia. Kama Yesu hakutoa amri hiyo, na Paulo hakutoa amri hiyo, basi ni nani aliyeiweka? Jibu ni Kanisa, si Mungu.

Ndiyo maana nilikuuliza niletee aya moja tu inayosema kwamba mtu anayekwenda kuwa kiongozi wa Kanisa lazima asioe. Siyo kwa sababu neno "padri" lipo au halipo, bali kwa sababu ulidai msimamo huo unatoka kwa Mungu. Mpaka sasa hujaonyesha maandiko yanayounga mkono hilo.

Na kuhusu 1 Timotheo 4:1–3, Paulo anaonya juu ya watu "watakaokataza watu wasioe." Sasa swali linabaki palepale: ikiwa Mungu hakutoa katazo hilo, kwa mamlaka gani Kanisa liliweka sharti hilo kwa wanaotaka kuwa mapadri?
 
Mkuu, Mungu hajakataza mtu kuoa/ kuolewa na hajalazimisha pia. Mtu akiamua kutokuoa/ kutokuolewa na atoe muda wake kumtumikia Mungu asilimia 100 ni dhambi? Nioneshe mahali ambapo Biblia imesema ni dhambi mtu kuamua kutokuoa/ kutokuolewa.
 
Mkuu, Mungu hajakataza mtu kuoa/ kuolewa na hajalazimisha pia. Mtu akiamua kutokuoa/ kutokuolewa na atoe muda wake kumtumikia Mungu asilimia 100 ni dhambi? Nioneshe mahali ambapo Biblia imesema ni dhambi mtu kuamua kutokuoa/ kutokuolewa.


Tena umehama kutoka kwenye hoja.

Sijasema popote kwamba mtu akiamua kutooa ni dhambi. Biblia haijasema hivyo, na hata Paulo alisema kutooa ni karama kwa baadhi ya watu:

"Natamani watu wote wangekuwa kama mimi nilivyo; lakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu." (1 Wakorintho 7:7)
Na Yesu pia alisema wako wanaochagua kutooa kwa ajili ya Ufalme wa Mungu:

"Wako waliojifanya matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili na alipokee." (Mathayo 19:12)

Kwa hiyo, hakuna ubishi kwamba mtu anaweza kuamua kutooa kwa hiari. Hilo si dhambi.

Lakini hiyo siyo hoja yangu.

Hoja yangu ni hii:

Je, Mungu aliagiza kwamba mtu akitaka kuwa padre au kuhudumu katika nafasi fulani za uongozi wa Kanisa ni lazima awe hajaoa?

Ukileta aya moja tu nitakubaliana na wewe.

Lakini Biblia yako inaonyesha kitu tofauti.

Paulo alipoweka sifa za askofu alisema:

"Basi imempasa askofu awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja..." (1 Timotheo 3:2)

Na tena:

"Mzee awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja..." (Tito 1:6)

Kama kutooa ilikuwa ni sharti la Mungu kwa viongozi wa Kanisa, kwa nini Paulo hakusema: "Askofu asiwe na mke"?

Zaidi ya hapo, Paulo alionya:

"...watawazuia watu wasioe..." (1 Timotheo 4:1–3)

Hakusema, "watashauri kwa hiari." Alisema "watakataza."

Kwa hiyo swali langu bado halijajibiwa:

Je, Kanisa likimwambia Mkristo, "Huwezi kuwa padre isipokuwa ukubali kutooa," hilo ni ushauri wa hiari au ni sharti?

Kama ni sharti, ni wapi Yesu au mitume waliliweka katika Maandiko?

Ukishindwa kuonyesha andiko hilo, basi ukubali kwamba hiyo ni sheria ya Kanisa, si amri ya Mungu. Hilo ndilo nimekuwa nikisema tangu mwanzo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…