Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 753
- 1,699
Kwa namna kesi ilivyoendeshwa kuanzia kumkamata, kumfikisha mahakamani, mpaka mashahidi wa mchongo kwenda kutoa ushahidi wao, ni wazi kuwa hata mtoto mdogo anaona hapo tunapotezewa muda tu, hakuna kesi wala nini, hivyo hawawezi kumkuta na hatia.
Lakini kumuachia Lissu nayo ni risk nyingine ambayo hawako tayari kuichukua. Kadri walivyozidi kumshikiria ndio umaarufu wa Lissu umezidi kuongezeka, lakini pia wamezidi kuwapa Watanzania sababu za kuzidi kumuonea huruma Lissu na hivyo kuongeza fanbase yake. Wanahofia akitoka haitachukua muda raia "wakakinukisha kweli", lakini pia kumbakisha ndani nako kunazidi kuwapa wananchi sababu ya kudai hali. Yaani pote pagumu.
Kwakuwa Lissu pekee yake hawezi kutenda uhaini na mashahidi wamezidi kumpa kete kwa kuonesha ni namna gani ni mazuzu waliojaza hewa vichwani, lazima watuhumiwa wengine waongezwe ili kujenga tuhuma za uhaini, ndo maana tumeona kamatakamata ya viongozi wa CHADEMA imekuwa kubwa! Sitashangaa nikisikia Heche na wenzake waliobaki wamekatwa, kundi zima la CHADEMA likiwa ndani hapo wataweza kuhalalisha hukumu yake ya kunyongwa wakisema ameshirikiana na wezake kutaka kumpindua Rais.
Hukumu hiyo ni...
1. Ama Lissu akutwe na hatia na viongozi wengine wa CHADEMA waongezwe kwenye list, au
2. Wasimkute Lissu na hatia yoyote, lakini upande wa serikali utakuwa tayari na rufaa mkononi, na hapo Lissu atarejeshwa tena rumande mpaka pale mahakama itakapokaa tena na kusikiliza rufaa hiyo ambapo inaweza kuchukua hata mwaka mwingine tena.... hapo watakuwa na muda wa kutosha wa kujipanga kumshikilia zaidi.
Kumbakisha ndani ni ngumu, lakini kumuachia ni ngumu zaidi, wanajua atawachachafya. Na vile friji la Lissu haligandishi wanajua atakuja kusema yoteee kama walijaribu kumhonga au njia yoyote waliotumia kuingia maridhiano ya mchongo ili wamzibe mdomo!