Kuna mpasuko unafumwa kisayansi ndani ya CCM na wamefanikiwa kwa 100%. Rais amechelewa kusoma mchezo

Kuna mpasuko unafumwa kisayansi ndani ya CCM na wamefanikiwa kwa 100%. Rais amechelewa kusoma mchezo

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Kama kawaida si kila kitu lazima kiandikwe Ila kuna ya msingi ya kuandikwa ambayo yana toa ushauri na kuwezesha kurekebisha panapotakiwa kurekebishwa.

Wengi tuliamini na kuamini kwamba kuna Mpasuko ndani ya Upinzani, hii ni Kwakuwa tuliamini upande wa Mbowe na Lissu hazipatani, Lakin nikakaa chini hasa kwa wale watu waliosomea intelligence na psychology watanielewa , mpasuko uko CCM.

Mpasuko ndani ya CCM usabababishwa na kambi za chaguzi kuu, kwa bahati mbaya 2015 Uchaguzi ule uliiacha CCM ilogawanyika sana na ikashindwa kurejea kuwa moja, na hata kama walirejea ni kwa unafiki wa juu juu tu! Ndo maana hata leo hii haya mnayoyaona anayakoroga Samia ni matokeo ya kambi za ccm

Naeleza sasa!

Kuna kundi linalosababishwa na kuumizwa Mwaka 2015, na wengine wamerejeshwa kuokoa jahazi muda huu Ila mbaya zaidi nao wameanza kubezwa na toto pendwa!

Balozi alikuwa kambi ya Lowassa na Toto pendwa alikuwa ni mmoja wa watu waliopinga sana Lowassa kwa mgongo wa JK, na sasa hivi wote wako pamoja japo hawapikiki. Mtoto pendwa kapika ushahidi feki wa mambo mbali mbali na kumpelekea Rais kwamba kuna mpango fulan na Fulan na wewe unaondoka muda si mrefu! Na mheshimiwa akapanik sana akaagiza Polisi waingie barabarani.

Wanaomshauri Rais ndo wanafuma vema Mpasuko kisayansi sana ili apuyange kwa wananchi na kwenye chama chao ili kutimiza lengo lake kuwekwa pembeni,

Samia amekosea wapi?
1. Baada ya kurithi kiti hakupaswa kuwa social sana kwa anaowateua na Kama hajui wanaomwangusha soon si mbowe wala lissu bali ni walioko ndani ya CCM ambao walishamdharau akiwa makamu, Alipaswa baada ya kurithi kiti angetaka nguvu asingekimbilia kufanya teuzi muda huo huo, angevunja Baraza la Mawaziri alafu akakaa Kama mwezi bila kufanya teuzi, ili kisaikolojia hawa wabunge wawe attention kuwa na adabu kwa Katiba na President na pia angechukua muda huo kujua nani Anafaa wapi na Nani hafai wapi! Hivo zile dharau walizokuwa wamejenga kwake akili zingewakaa Sawa kwanza hawa wanasiasa kwa kusibiria kwa shahuku Nani anateuliwa Nani hateuliwi. Ingempa heshima sana, na pia angejenga nguvu ya KAULI YA KIMAMLAKA, kwa sasa Rais anategemea na hao watoto pendwa ndo wamwambie sema hiki sema kile.

Nilitegemea kwenye masuala ya mauaji angetoa kauli ya KIMAMLAKA Lakin haikuwa hivo Aliishia kulaani tu!

Pili angetaka atawale vema asingekataza maandamano ya CHADEMA ya leo! Swali la kwanza je wakiandamana wanaelekea wapi? Uoga wa nini? Aliyemshauri jambo hili anausuka mpasuko vema sana ndani ya CCM, maandamano ya CHADEMA yangefanyika yangeimarisha zaidi CCM kuliko CHADEMA, na yangempa credit Samia kuliko mbowe au lissu.

Ninamlaumu Mbowe kwa kutoa tarehe ya mbele sana ya maandamano badala ya maandamano kuanza siku hiyo Hiyo!

Watanzania ni watu wa kuvaa suala likiwa hot sana!

Ushauri kwa CHADEMA NA UPINZANI
1. Maandamano inabidi yawe organized tofauti , fanya Kama akina Nyerere walivyojificha katika shughuli fulan kumbe ndo wanaandamana hivo!

2. Viongozi wasiwe wanatoa location zao wanapojua kesho au keshokutwa kuna jambo la ku organize, wasiwe rahis kukamatwa ili ku destabilize mipango.

3. Maandamano yasitangazwe Kama ya chama Bali ya wanamchi! Ili imguse kila mtu.

Nitaandika Tena sijapangilia vema Bali ntaeleweka.

Britanicca
 
 
Kama kawaida si kila kitu lazima kiandikwe Ila kuna ya msingi ya kuandikwa ambayo yana toa ushauri na kuwezesha kurekebisha panapotakiwa kurekebishwa



Britanicca
Your pain
Yet more my pain
Shall suffocate oppression

Your eyes
Yet more my eyes
Shall be speaking of revolt

Your scars
Yet more my scars
Will be remembering the whip

My hands
Yet more your hands
Will be lifted fully armed

My strength
Yet more your strength
Shall overcome imperialism

My blood
Yet more your blood
Shall irrigate our victory
 
Kama kawaida si kila kitu lazima kiandikwe Ila kuna ya msingi ya kuandikwa ambayo yana toa ushauri na kuwezesha kurekebisha panapotakiwa kurekebishwa
samia amani.png
 
Kama kawaida si kila kitu lazima kiandikwe Ila kuna ya msingi ya kuandikwa ambayo yana toa ushauri na kuwezesha kurekebisha panapotakiwa kurekebishwa




Nitaandika Tena sijapangilia vema Bali ntaeleweka

Britanicca
Kwani wakati anakabidhiwa kijiti hakuambiwa kuwa mwisho ni 2025, au aliambiwa tatizo amenogewa na Asali?
 
Huu mchezo nimeusoma na kuelewa sana, kuna wakati wanasiasa wao kwa wao wanakuwa wajinga ukiangalia hata kiongozi wa nchi naye anashindwa kujiongeza kwa vitu vidogo ambavyo vinaenda kumuharibia.

CCM huko ndani wanaogopana na mbaya zaidi ni kutokana na nafasi ya mwenyekiti kuwa na nguvu kubwa sana, kisiasa na kiserikali, kisheria na kitamaduni.

Na hatimaye nyani anarukia miti ingawa kila anaorukia unateleza!.
 
Back
Top Bottom