Anasikia vizuri sana, mpaka vishindo vya miguu kusogelea kaburi na kuondoka anasikia! Dua na maombi anasikia! Asichoweza kufanya ni kusogea, kuongea, kuvuta pumzi!
Dua/Maombi hata kama anafanyiwa kilometa 1,000 au kilometa 6,000 kutoka alipozikwa yeye, anaambiwa na malaika fulani anakufanyia dua/maombi fulani!
Na kama ulikua hujui, hata pindi watu waliokua hai, aliowaacha hai wakimsahau kumfanyia dua/maombi, huwa anahuzunika sana kwanini amesahauliwa!! Na kwa waislamu ndio maana huwa na ratiba kila baada ya muda fulani (Miezi au kila mwaka/miaka) huwafanyia dua/maombi wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki (Utaskia; Juzi tulifanya khitma ya wazee wetu au wapendwa wetu waliotangulia mbele ya haki, tulijisahau miaka bana)!!