Kuna mtu huwa anaelewa Kingereza cha Nigeria?

Hivi kuna mtu tofauti na raia wa Nigeria wenyewe huwa anaelewa English ya Nigeria? Mimi huwa sielewi Kingereza wanachozungumza Wa Nigeria hasa wa mtaani au wanamuziki na comedians wao wengi.
View attachment 3578391
Nilikuwa na Mwingereza mmoja,sasa rikakutana na Mnaijeria atupe maelezo flani, anamaliza kuongea jamaa ananiuliza huyo jamaa alikuwa anaongea lugha gani? Nikamwambia kingereza, alishangaa sana maana yeye hakuelewa chochote
 
Kinaeleweka sana ila kimejaa Yoruba na Igbo accent and words.
Are you soppozd (support) to ...,
Soni (son), I no sabi, moni (money), wetin, dey.

Kipo cha Ghana pia karibu Tema.
 
Hata kiswahili, mimi niko chuo marafiki zangu waZanzibar Kiswahili changu wanaita kiswahili Cha Dar wanaona kigumu na Kuna mmoja kutoka Pemba ndio ilikuwa hatari napata tabu kumuelewa Bora hata wa Unguja.
 
Hata huko Uingereza wanatofautiana kulingana na maeneo na miji kama ilivyo Arusha, Dar na Kigoma. Kwa kifupi hakuna viwango vya lugha, lugha ni MAWASILIANO kwenye jamii husika ambapo kila jamii huwa na aina ya matamshi kutokana na aina ya msemo waliozaliwa nao.
 
Tulikuwa na mhadhiri mhindi aisee, yaani Hadi kuja kuelewa inabidi uwe makini Sana halafu Pepa zake anatoa papo Kwa papo, akimaliza kufundisha Tu anatoa mtihani, Hana cha kuandika zaidi ya title ya anachokifundisha basi, yaani utafikiri Tupo Mumbai, alikuwa kichwa Sana Yule ticha hasa masomo ya hesabu, mshenzi Sana Yule Jamaa maana vichwa panzi walipata Sana sifuri...
 
Kiswahili cha Zanzibar kwa 90% kinaeleweka, Kuna maneno machache huwa yanaweza kuwa mapya lakini bado ni rahisi kuyaelewa ukivuta picha kidogo mfano skuli, tunguja, marikiti, ushanifahamu n.k
Ongezea mfereji (Bomba), kipolo (Kiroba).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…