GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Ni Watanzania Sisi ( GENTAMYCINE ) nikiwemo wakati wa Uongozi wa Hayati Rais Dkt. Magufuli tulikuwa tunalalamika Mzunguko wa Hela ni mgumu na hata Kumlaumu Hayati kwa kutokupenda Kwake ' Kujichanganya ' na Mataifa Jirani na hata Makubwa ili Maendeleo ya haraka yapatikane na Ustawi wetu uwepo.
Haya hivi sasa tuna Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan ambaye taratibu anaanza ' Kujjtanua ' kwa Kushirikiana na Mataifa Jirani na Makubwa hadi Kuwavutia Wawekezaji wakubwa ili aweze kurudisha Mzunguko wa Pesa nchini, Miradi mingi itakayochochea upatikanaji wa Fursa za Ajira ili akina GENTAMYCINE tuondokane na Umasikini ( Unyonge ) wa Kipesa tulionao tumeanza tena ' Kumzodoa ' na ' Kumzoza ' Mama wa Watu kuwa sijui anauza nchi na anaipeleka nchi kubaya.
Hivi Watanzania tunataka nini? Tunajitambua kweli? Hizi Nongwa na huu Unafiki wetu ' uliotutukuka ' zina Faida gani? Ni kwanini tunakuwa ni Watu tu wenye Majungu, Visununu, tusiokuwa na Uvumilivu wala Shukrani? Tumelorogwa na nani ili tuwaombe Viongozi wa Kidini watuombee au tufunge tumlilie Mwenyezi Mungu?
Mama wa Watu masikini ( Rais Samia Suluhu Hassan ) hana hata Siku 100 tu Ofisini tayari kuna Mifalme Njozi ' Mipopoma ' inajifanya imeshajua kule ambako anatupeleka wakidai kuwa anatupoteza na kwamba hawezi Kuongoza kama ilivyokuwa kwa Mtangulizi wake Hayati Rais Dkt. Magufuli.
Leo hii baadhi yetu tunamsema kwanini Mama ( Rais Samia Suluhu ) ana ukaribu mno na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na kwamba ndiyo anamuongoza Kiuongozi kitu ambacho hata hivyo Mimi GENTAMYCINE sioni tatizo lolote lile juu ya hilo.
Mbona wakati Hayati Rais Dkt. Magufuli alivyokuwa Madarakani alikuwa na ukaribu sana na Rais Mstaafu Hayati Benjamin Mkapa na ndiyo alikuwa akimuongoza na tulikuwa hatusemi?
Kama Great Thinkers, Academicians na Think Tanks wa Tanzania tunaacha Kumsaidia Mama ( Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ) kwa Ushauri na Mawazo ' very Constructive ' ya kuitoa Tanzania yetu hapa ilipo na ikimbizane na Mataifa mengine Kutwa tu tunakalia Majungu, Umbea, Wivu na Unafiki.
Kwako Mheshimiwa Rais wangu ( wetu ) Mama Samia Suluhu Hassan tafadhali nakuomba Ongoza nchi kwa ' Style ' yako na kamwe usitusikilize Sisi ' Wanafiki Wakomavu ' wa Kitanzania tusio na hata chembe ya Uvumilivu na Shukrani ndani ya Mioyo yetu na Roho zetu pia.
Kitabu cha Rais Hayati Dkt. Magufuli kimeshafungwa na sasa ni wakati wa Kuandika Kitabu chako na Wewe ukiingia tu katika Mtego wa Kusikiliza ' Majungu ' yetu Sisi ' Waswahili ' utapoteza Dira yako na ndiyo utakosea na Kuongoza nchi vibaya kisha utakuwa umeshawapa ' Waswahili Wanafiki ' cha Kusema na ' Nongwa ' zao ( zetu ) kuzidi.
Chapa Kazi Mama yetu ( Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ) TUNAKUPENDA na tutakuombea MAFANIKIO kwa Mwenyezi Mungu ( Allah ) na Binafsi kama GENTAMYCINE wala sina Shaka nawe kwani najua unaweza, una uzoefu na una bahati na kupata Washauri wazuri ambao Ndoto zao ni Kuona Watanzania wanafurahi Kiuchumi, Kiustawi na Kimaendeleo pia.
Dozi hii 'Mujarab' iwaingieni vizuri mno.