Ni wale wanaojiona wajanja wa mjini, maneno kibao na ujuaji Mwingi.. ila ni mpuuzi Mmoja tu hivi kuhusu akili Hana kabisa.Ni mzima wa akili?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni wale wanaojiona wajanja wa mjini, maneno kibao na ujuaji Mwingi.. ila ni mpuuzi Mmoja tu hivi kuhusu akili Hana kabisa.Ni mzima wa akili?
Ndiyo. Uko vizuri. Hata yule mzee wa nchi aliwahi kusema"Akili za kupewa, ongeza na za kwako" Kinachofuata hapo sasa ni wewe kuwa makini na mwangalifu sana e.g. acha kuongea hovyo na uwe makini sana kwenye utendaji wako wa kila siku ili wanoko wasije wakakushtukia.Imenibidi kuandika huu uzi ili kubadililishana ujuzi wa kukabiliana na changamoto za hapa na pale kwenye hili life
Kuna kipindi nilikuwa nafukuzia mchongo kwenye kampuni fulani.
Ilifikia hatua nimepata huo mchongo lakini nilihitajika kupeleka license ya udereva,ndani ya week moja niwe nimewapelekea leseni.
Kila nikiwaza sana kichwa kilikuwa kinauma,leseni sina wala cheti cha veta sina halafu natakiwa nipeleke leseni ndani ya week moja.
Veta penyewe mafunzo si chini ya siku 30 mpaka nikabidhiwe na leseni nitakuwa late sana.
Nikaanza kuwacheki wadau tunafanyeje?
Mwisho wa siku niliunganishwa na jamaa anaitwa lukaku ambaye mpaka sasa ni jamaa yangu sana maana huwa tunasaidiana kwenye hizi kero ndogondogo.
Jamaa aliniambia nimpe 320,000,tin,majina matatu na namba yangu ya nida then ataniletea cheti cha veta mpaka leseni ambazo ni original kabisa ndani ya siku 8,nikaona sio mbaya sana.
Japo mwanzo nilisita nikiogopa ntapoteza pesa lakini nikasemaa liwalo naliwe.
Nachoshukiru jamaa alikuwa mwaminifu na issue ikawa solved.
Kuna kipindi tena nilianza biashara ya kuuzq ubuyu kutoka vijijini kupeleka kiwandani.
Hii nayo ilinibidi kupita shortcut maana tuliokuwa tunafanya hii issue tulikuwa wengi mno halafu kuna wakati bei inakuwa sio kafiki wakati mwingine bidhaa inakuwa nyizidi mahitaji
Ilibidi nimtafute afisa manunuzi tuongee
Tukakubaliana ubuyu atakuwa ananunua kwangu kwa bei fulani na mimi nitakuwa nampa 7% kwa kila gunia,
Kilichofanyika wale wauzaji wengine walikuwa wananiuziq mimi kwa bei ya kawaida halafu mimi ndio napeleka kuuza kiwandani huku yule afisa akila 7% zake
Hizo ni baadhi ya shortcuts chache ambazo nimewahi kupitia. Lengo la kushare nanyinyi ni kuonesha jinsi gani shortcut inalipa kwenye hizi nchi zetu hasa Tz hasahasq kwa sisi vijana tusiokuwa na connection na wakati huohuo unataka mambo yakuendee.
Sio lazima wakati wote upite njia iliyonyooka wakati mwingine unapita mkato ili mambo yakuendee, kuna kipindi cha nyuma nilikuwa nimenyooka sana ikafika hatua baadhi ya mambo yangu yalikuwa hayaendi kabisa, nikaona nibadili mtazamo ili kwendana na uhalisia wasasa.
Asanteni
Ongeza hizi:Shortcut ilinitoa keko _ magereza .
Shortcut _imenitoa wizara moja kwenda wizara nyingine .
Shortcut _naiona ikinipa boss awe mke wangu mpya .
Shortcut _inanifanya nisipende kuishi mjini tena napaona Kama jehanum
Ongeza na hili .Ongeza hizi:
Shortcut_ inakufanya uwe ni mtu mwenye wasiwasi na kutojiamini kwani utakuwa na hafu kwamba siri yaweza kubumburuka wakati wowote.
Shortcut _inakuweka kwenye nafasi ya kuwa kama mateka fulani kwa "wawezeshaji" wako kwani wanaweza wakakudai malipo magumu ambayo kwako sio rahisi kuyatekeleza e.g. rushwa ya ngono.
Shortcut _mara nyingi mwisho wake sio mzuri e.g. yaliyotokea kipindi cha mzee Magu.