Kuna muda itakubidi upitie shortcut ili mambo yako yaende

Kuna muda itakubidi upitie shortcut ili mambo yako yaende

Imenibidi kuandika huu uzi ili kubadililishana ujuzi wa kukabiliana na changamoto za hapa na pale kwenye hili life

Kuna kipindi nilikuwa nafukuzia mchongo kwenye kampuni fulani.

Ilifikia hatua nimepata huo mchongo lakini nilihitajika kupeleka license ya udereva,ndani ya week moja niwe nimewapelekea leseni.

Kila nikiwaza sana kichwa kilikuwa kinauma,leseni sina wala cheti cha veta sina halafu natakiwa nipeleke leseni ndani ya week moja.

Veta penyewe mafunzo si chini ya siku 30 mpaka nikabidhiwe na leseni nitakuwa late sana.

Nikaanza kuwacheki wadau tunafanyeje?

Mwisho wa siku niliunganishwa na jamaa anaitwa lukaku ambaye mpaka sasa ni jamaa yangu sana maana huwa tunasaidiana kwenye hizi kero ndogondogo.

Jamaa aliniambia nimpe 320,000,tin,majina matatu na namba yangu ya nida then ataniletea cheti cha veta mpaka leseni ambazo ni original kabisa ndani ya siku 8,nikaona sio mbaya sana.

Japo mwanzo nilisita nikiogopa ntapoteza pesa lakini nikasemaa liwalo naliwe.

Nachoshukiru jamaa alikuwa mwaminifu na issue ikawa solved.

Kuna kipindi tena nilianza biashara ya kuuzq ubuyu kutoka vijijini kupeleka kiwandani.

Hii nayo ilinibidi kupita shortcut maana tuliokuwa tunafanya hii issue tulikuwa wengi mno halafu kuna wakati bei inakuwa sio kafiki wakati mwingine bidhaa inakuwa nyizidi mahitaji

Ilibidi nimtafute afisa manunuzi tuongee

Tukakubaliana ubuyu atakuwa ananunua kwangu kwa bei fulani na mimi nitakuwa nampa 7% kwa kila gunia,
Kilichofanyika wale wauzaji wengine walikuwa wananiuziq mimi kwa bei ya kawaida halafu mimi ndio napeleka kuuza kiwandani huku yule afisa akila 7% zake

Hizo ni baadhi ya shortcuts chache ambazo nimewahi kupitia. Lengo la kushare nanyinyi ni kuonesha jinsi gani shortcut inalipa kwenye hizi nchi zetu hasa Tz hasahasq kwa sisi vijana tusiokuwa na connection na wakati huohuo unataka mambo yakuendee.

Sio lazima wakati wote upite njia iliyonyooka wakati mwingine unapita mkato ili mambo yakuendee, kuna kipindi cha nyuma nilikuwa nimenyooka sana ikafika hatua baadhi ya mambo yangu yalikuwa hayaendi kabisa, nikaona nibadili mtazamo ili kwendana na uhalisia wasasa.

Asanteni
Ndiyo. Uko vizuri. Hata yule mzee wa nchi aliwahi kusema"Akili za kupewa, ongeza na za kwako" Kinachofuata hapo sasa ni wewe kuwa makini na mwangalifu sana e.g. acha kuongea hovyo na uwe makini sana kwenye utendaji wako wa kila siku ili wanoko wasije wakakushtukia.
 
Shortcut ilinitoa keko _ magereza .

Shortcut _imenitoa wizara moja kwenda wizara nyingine .

Shortcut _naiona ikinipa boss awe mke wangu mpya .

Shortcut _inanifanya nisipende kuishi mjini tena napaona Kama jehanum
Ongeza hizi:
Shortcut_ inakufanya uwe ni mtu mwenye wasiwasi na kutojiamini kwani utakuwa na hafu kwamba siri yaweza kubumburuka wakati wowote.
Shortcut _inakuweka kwenye nafasi ya kuwa kama mateka fulani kwa "wawezeshaji" wako kwani wanaweza wakakudai malipo magumu ambayo kwako sio rahisi kuyatekeleza e.g. rushwa ya ngono.
Shortcut _mara nyingi mwisho wake sio mzuri e.g. yaliyotokea kipindi cha mzee Magu.
 
Ongeza hizi:
Shortcut_ inakufanya uwe ni mtu mwenye wasiwasi na kutojiamini kwani utakuwa na hafu kwamba siri yaweza kubumburuka wakati wowote.
Shortcut _inakuweka kwenye nafasi ya kuwa kama mateka fulani kwa "wawezeshaji" wako kwani wanaweza wakakudai malipo magumu ambayo kwako sio rahisi kuyatekeleza e.g. rushwa ya ngono.
Shortcut _mara nyingi mwisho wake sio mzuri e.g. yaliyotokea kipindi cha mzee Magu.
Ongeza na hili .
Yakishambumburuka inabidi uwe ulishajiweka sawasawa ili ueze kuendana na mazingira .

Shortcut inategemea ni nani alikubeba ,Ila usikubali saana kubebwa na watu Baki maana wanapenda malipo yasiyoisha
 
Back
Top Bottom